Kocha wa Makipa Simba SC na wengine 8 wakamatwa na Dawa za Kulevya
Hawa jamaa wa kuitwa kambiaso sio mara ya kwanza inaonekana hata huko nyuma walishadakwa wakaachiwa tena kipindi ambapo vita vya sembe vilikuwa na nguvu na tena mzigo mzito ulilipotiwa,kwa kiasi hiki watawafanya nini?
============================
Screenshot_20221116-151311_Chrome.jpg

Tuesday, 20 December 2016​

KINARA DAWA ZA KULEVYA MBARONI​

KINARA wa mtandao wa biashara za dawa za kulevya, Kambi Zubeir Seif, maarufu kwa jina la Cambiasso, ametiwa mbaroni, kufuatia msako mkali uliofanywa na Polisi Kikosi Maalumu cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, katika nyumba yake ya kifahari aliyokuwa amejificha iliyoko Tuangoma, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.
Cambiasso, pia inadaiwa mwaka 2011, alikamatwa na kilo 179, za dawa za kulevya aina ya heroine, akiwa na wenzake watatu, Fredy Chonde, ambaye ni Mtanzania, Muhammad Shahbaz na Abdulghan Gulam, ambao ni raia wa Pakistan.
Mfanyabiashara huyo anayemiliki nyumba za kifahari pamoja na magari, anayedawa kuwa kinara muunganishaji wa mitandao ya dawa za kulevya, alikamatwa usiku wa kuamkia Desemba 10, mwaka huu, katika operesheni kali ya kuwasaka wafanyabiashara wa dawa za kulevya nchini.
Wengine waliokamatwa kwenye msako huo ni Marashi Zuberi Seif, ambaye ni dada wa mtuhumiwa namba moja na rafiki wa kike wa Cambiasso, Grace Aseasisye, ambaye alipangiwa nyumba eneo la Yombo Buza.
Imeelezwa kuwa polisi inaendelea na msako mkali baada ya watuhumiwa wengine kukimbia, ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu, operesheni hiyo ni mwanzo wa operesheni kubwa zitakazoendeshwa na polisi kuumaliza mtandao huo unaohatarisha nguvu kazi ya vijana.
Akizungumzia kukamatwa kwa kinara huyo, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Dawa ya Kulevya Tanzania, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP), Mihayo Msikhela, alisema Cambiasso alikamatwa Ijumaa, iliyopita na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
“Huyu ni kiunganishi wa mitandao hiyo. Polisi walifanikiwa kumtia nguvuni baada ya kuweka mtego nyumbani kwake na Ijumaa alishafikishwa mahakamani kujibu moja ya kesi inayomkabili,” alisema Kamanda Msikhela.
Kwenye kesi hiyo, mtuhumiwa huyo aliunganishwa katika kesi namba PI 23/2016 ya raia wa Nigeria, Bede Eke, aliyekamatwa Juni, mwaka huu, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, akiwa na kilo tano za dawa za kulevya.
Anakabiliwa na kosa la kula njama (conspiracy) na kusafirisha dawa za kulevya pamoja na raia huyo wa Nigeria.
Msako huo ni hatua za mapambano dhidi ya mtandao huo, ambao serikali ya awamu ya tano imeahidi kuutokomeza.
Katika mkesha wa kuliombea Taifa, Desemba 31, mwaka jana, Rais Dk. John Mafuguli, alisema Taifa kwa kipindi kirefu lilikabiliwa na vigogo wauza dawa za kulevya, watumishi na vigogo wakwepaji wa kodi pamoja na wizi wa dawa hospitalini, hivyo viongozi wa dini na Watanzania wote wanapaswa kumuombea ili aweze kutumbua majipu ya mafisadi hao.
Dk. Magufuli, ambaye aliwakilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alisema viongozi wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea Taifa na kuwaombea watu wabaya wasiopenda maendeleo waweze kubadilika ili nchi iweze kusonga mbele.
“Viongozi wa dini tunapaswa kuendelea kumuombea rais wetu (Dk.Magufuli), aendelee kutumbua majipu haya, ambayo yanasababisha maendeleo ya Taifa letu kurudi nyuma,” alisema Lukuvi.
 
Hawa jamaa wa kuitwa kambiaso sio mara ya kwanza inaonekana hata huko nyuma walishadakwa wakaachiwa tena kipindi ambapo vita vya sembe vilikuwa na nguvu na tena mzigo mzito ulilipotiwa,kwa kiasi hiki watawafanya nini?
============================
View attachment 2418550

Huyo Fred chonde alikuwa anafanya kazi clearing agent...km sijakosea
Hao wenzake walinyolewa miaka 30
Yeye cambiaso aluchomowa kesi
Jamaa alijuwa kucheza na jj kwenye kesi hiyo....sasa sjui huyo jj bd yupo au [emoji1]
Ngoja tuone sahvi itakuwaje je atatusua au
Sema huu msala unaonekana ni maagizo toka juu,maana kama walijaribu kuwapa pesa wazee na wakachomoa jua hiyo mission ilikuwa nzito

Ova
 
Hao wanacheza na system kwisha habari,jaji ni kupewa tu maelekezo.
 
Mmh inategemea na connection yako sasa....
Ila issue hii inaonekana ina msukumo kutoka nchi za nje [emoji848]

Ova
Aisee! Ngoja tuone,yetu macho na masikio ingawa huwa kwenye kundi wachache wanatolewa sadaka,mmoja au wawili wanachomoka kuendeleza ajenda.
 
Wauza ngada wanapenda kujifanya wacha Mungu jamaa ni alhaji kabisa kila mara kwenda hija kumbe ni janja janja....

Japo sio wote lakini baadhi wanaojifanya ni watu wa dini hasa ambao ukiwanagalia kwa karibu hawana uhalisia huo ni dalili ya kuficha baishara haramu wamo poa ma fake pastor...
 
Sio kushangilia tukio hili.Simba ni taasisi inawadau wengi ndani na nje hivyo viongozi wanaoteuliwa wawe na weledi.Timu zinawakilisha nchi zinabeba benders mambo ya hovyo lazima yaepukwe
 
Kocha wa magolikipa ..kwani si katambulishwa jana jamani??
 
Juzi nilipohudhuria Live band hapo DSM na kuona sijui Mapendeshee yanatajwa Tena kwenye nyimbo zile nilianza kuhisi hii biashara ya Madawa Haina muda mrefu inaanza.

Hongereni Mamlaka kuweza kuwakamata hao Wahusika ila muhimu wasije kuhonga pesa na kuachiliwa.

Kwa hyo unadhani hii biashara itakuja kuisha???acha kujidanganya mkuu,viongozi wa serikali wenyewe ndo ma taikun wa mchongo hao kina mwarami ni punda tuu
 
Najua Mkuu haiwezi kuisha lakini ikidhibitiwa itapungua kabisa.

Mkuu Vijana ambao ndiyo nguvu kazi inazidi kupotea kwenye utumiaji.
 
Na wanamichezo hawakaguliwi...... ukiona wamebeba mipira mingi wakishuka tu airport mipira wakubwa wanaichukua fasta.....
Nani amekudanganya kuwa hawakaguliwi? Acheni ushamba, tafuteni passport msafiri walau hata mfike hapo Dubai, labda ndio utajua nani anakaguliwa na nani hakaguliwi
 
Back
Top Bottom