Kodi kwa 'watoto' wa miaka 18?

Mnh,Labda nimeelewa sivyo,ila kama mtoto analipia kwenye manunuzi hio ni kodi tayari,

I still maintain mtoto wa Miaka 18 hapaswi kulipa Kodi yeyote huu ni uonevu, sababu Mzigo unarudi kwa wazazi. Ni sawa na kusema wazazi walipe kodi twice as much, ya kwake na ya hela anayompa mwanae kwa matumizi...huu ni wizi wa mchana kweupeeee
 
Ni hivi
Kila huduma ufanyayo unakatwa kodi ila hautambuliki kama mlipa kodi. VAT hulipwa na mtumiaji wa mwisho ambao ni sisi.
Hivyo basi ili tuonekane ni walipaji, kila mtu itambidi awe na TIN ambayo itasajiliwa kwenye Number za Simu na Bank, kwamba ikitokea umefanya malipo kwa njia tajwa basi ile VAT itaenda kwenye acc yako kule TRA na utajulikana kama mlipakodi
 
Usiseme wa kwangu peke yangu, wakati Majority ya wazazi kibao tanzania wana watoto wenye miaka 18!, labda useme peke yako kuwa mtoto wa miaka 18 ni mtu mzima mwenzio
Povu la nini, mtoto ni mtoto kwa kila mzazi, haijalishi miaka yake. Ila kijana wa miaka 18 siyo mtoto tena, ni mtu mzima ndiyo maana yenyewe.
 
Mapato- manunuzi= faida
Hiyo faida ndio inaangaliwa kiasi gani ipigwe Kodi.

Sasa mtoto au wanyonge ( in maguu voice) kwaomanunuzi yatazidi mapato so hamna Kodi
Ila hii itasaidia kulazimisha utoaji risiti yaan utamlazimisha muuzaji au mtoa huduma akupe risiti hata serikali ya mtaa nakwa mjumbe tutapelekana ili tini zetu zioneshe hasara
 
Povu la nini, mtoto ni mtoto kwa kila mzazi, haijalishi miaka yake. Ila kijana wa miaka 18 siyo mtoto tena, ni mtu mzima ndiyo maana yenyewe.
Mnhh naona huelewi ngoja nikuache mkuu, utamwitaje mtoto wa miaka 18 ambaye bado tegemezi yuko kwa wazazi ni mtu mzima?!
 
Miaka 18 ni mtoto Huyo?
 
Mkuu unaeleweka sana ila miaka 18 ndiyo age of majority. Hivyo, TRA's jurisdiction ndiyo inaanzia hapo notwithstanding huyo kijana atalipa kodi ama la, lazima wamtambue kama potential tax payer na aingie kwenye data base yao. Just in case ikitokea anafanya activities which attracts tax payments iwe rahisi kupata kodi kutoka kwake.
 
I agree with you 100%
 
 
Waziri alimaanisha kwamba kama wana shughuli inayowaingizia kipato basi walipe kodi ...hakuwa na maana kwamba kijana yoyote tu mwenye miaka 18 kwa maana umri huo wengine ndiyo wanamaliza Form four na wengine ndiyo wanaendelea na Advance....

Lakini kuna wengine katika umri huo wa mika 18 wanafanya Biashara na Shughuli za kuwaingizia kipato
 
This time they're going for kill... 18 yrs old alipe tax huku wawekezaji wanasamehewa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…