Kama kuna mahali Mh. Rais alikosea ni kuendeleza baraza la yule mtangulizi wake.
Waziri wa Fedha sio Mbunifu.
Tanzania bila mfumo bora wa uongozi hatuwezi kutoboa bila serikali kuwaibia wananchi wengi na kunufaisha wachache.
Wengi wataumia sana kama Farasi dume wa mkoloni. Mkoloni alikua na Farasi dume lisilo na jike wala msaidizi. Muda wote mzungu yupo mgongoni mpaka alipowapata waafrika wa kumbeba mgongoni.
Watawala wasio na mbinu mbadala wanawatumia wananchi kujinufaisha wao kwa madaraka tuu huku wananchi wakiumia.
Kwa sasa ni vikao na semina elekezi kila sehemu.
Utasikia pesa za Tasaf lakini ukijiuliza hiyo Tasafu kwa nini isingekua na ubunifu tu wa kuwatafutia hao maskini ardhi kule Bagamoyo ,Chato, Mkuranga, Mtwara ,Lindi Arusha ,Namanga, Manyara, Dodoma , Mwanza n.k. ikawamilikishia viwanja kama rasilimali zao na familia zao maskini ?
Au kumwapa Hati za umiliki wa maeneo yao bure ili wazitumie kuwekeza badala ya kufanya ujanja ujanja wa kuwapa watu elfu kumi za kununulia kuku mmoja wa kienyeji ambao zamani tulikua tunakwenda kwa mjomba na babu na bibi unapewa kuku unaenda kufuga unapata vifaranga unarudisha kuku wa watu.
Ujanja ujanja ni mwingi unalenga kujinufaisha tu.
Chunguzeni hao wanatumia madaraka yao kuwaumiza wanyonge kwa kujifanya wazalendo ,wao ni mabilionea, wanalindana ,wanaogopa maisha magumu kwenye familia zao. Wanamatumizi makubwa kwa kodi za umma.
Hivi ni nchi gani maskini inaweza kuendelea kwa serikali kuwa na matumizi makubwa kwa kodi ya maskini?
Nchi inaendelea kwa kupunguza matumizi na kuongeza mapato kwenye rasilimali za asili sio kukusanya vipesa vya madafu.
Leo tulitakiwa tuwe Taifa linalouza gesi mpaka Afrika kusini .
Gesi isiyo na suala la Korona kama wanavyofanya Urusi kwa nchi za ulaya.
Badala yake tunawekeza kwenye usafri wa ndani kwa gharama za wanyonge wenyewe huku Rasilali zao za asili zikiwa zimeshikiliwa na watawala wanaosubiri wawekezaji watakaowatumia kuweka hisa zao zinazotokana na mapesa wanayowaibia wanyonge.
Ndio maana Watawala wa awamu ya tano walikua wanaua mitaji ya wafanyabiashara ili baadae wao ndio wawe wawekezaji kwa fedha walizokwapua kwenye maofisi na tenda za kupeana kwenye miradi mikubwa.
Tanzania tumekua na mamlaka nyingi za kukaa ofisini huku zikilipwa mamilioni ya Pesa kwa kodi za kuwaumiza wananchi. Hizi kazi yake ni kuongeza tozo ili wao waishi maisha mazuri na kuwaumiza walaji wa mwisho.
Ewura wakati TBS ipo.
Tozo za miamala wakati VAT ipo.
Sumatra wakati Jeshi la polisi lipo.
Suma JKT wakati JKT na JKU iliundwa kwa ajili ya kujenga nchi na uchumi wa nchi bara na visiwani.
REA wakati Tanesco ipo.
Tarura wakati Halmashauri zipo na Tanroad.
Sijui Tanapa ,Sijui Mamlaka ya Bandari,Sijui ,mawakala wa kukusanya ushuru ,Sijui .
Kila sehemu ni Mamlaka Mamlaka na ukiangalia wao wanajilipa Mishahara mikubwa kuliko wazalishaji na watendaji wanaowajibika moja kwa moja.
Sumatra mfano wapo mikoani tu na hawana uwezo wa kufanya kazi bila Polisi lakini polisi wana mishahara duni kuliko wao. Polisi wana magari Duni kuliko wao. Faini za polisi ni ndogo kuliko zao. Yote ni kuongeza wigo wa rushwa na kujinufaisha na kundi dogo huku kundi kubwa likiumizwa.
Nchi hii inahitaji mjadala mpana na Katiba Mpya ili tupate wawakilishi wa wananchi kwenye Bunge badala ya Bunge la wawakilishi wa kulinda maslahi ya watawala na familia zao.
Bunge la marafiki na familia zao.
Bunge la sasa lipo kwa ajili ya kukutana na kula hata kwa kodi za watanzania huku likipitisha maumivu kwa watanzania.
Tunataka katiba itakayoweka bayana maslahi ya wanyonge ni yapi na haki zao ni zipi na miiko ya uongozi. Utawala bora unaotokana na kura za wananchi ni nguzo kubwa sana.
Watu wanatozwa kodi na tozo nyingi lakini wanaambiwa wajenge shule ,hospitali, wachimbe mitaro ya mabomba ya maji kwa nguvu zao tena ,yani waache kwenda shambani kujitafutia riziki waende kujenga shule lakini shule ikiisha ni mtaji wa mkuu wa wilaya ,mkurugenzi mbunge wa kuteuliwa na diwani wa kuteuliwa. !!
Katiba katiba katiba.