Kosa kubwa tunalofanya wanaume ni kuwa na mke mmoja

Uhuru wa mawazo mkuu,,, hivo hajakosea kuleta hii mada hapa
Hata mimi sijasema amekosea kwa mujibu wa mawazo yake, nilikuwa najaribu kuonyesha upande wa pili, utakuwa na wake wanne let say kila mke akakuzalia watoto wawili hapo unawatoto sita, kumbuka ukiwa na hao wake wanne sahau kuhusu uzazi wa mpango hakuna mwanamke atakubali azae mtoto mmoja tu ili uwe na wanne, Kisa cha Yakobo kuwa na watoto wengi ni kwa sababu wake zake wawili(Recho na Lea) walikuwa wanashindana kumzalia watoto, sasa kwa nyakati hizi una watoto 6 vipi ustawi wa hao watoto?

Au Mada(mawazo) ya mtoa hoja yanalenga kistarehe zaidi ya ngono tu kwamba mwanaume atajiamulia ale wapi na saa ngapi?
 
Uko sahihi maana mumedanganywa na dini za Wazungu
 
Haujatufikiria kwamba tunaoshabikia uzi ni matajiri?Think,and think twice boss!
 
Tatizo kipato linatosha kuacha kodi ya meza 50000 ya matumizi kila nyumba kila siku?
 
Haujatufikiria kwamba tunaoshabikia uzi ni matajiri?Think,and think twice boss!
😂😂😂😂😂 sawa matajiri, nilikuwa sijajua,. Lakini hebu tuulizane matajiri

Mwanaume akiwa na wanawake wanne; usaliti wa kuwa na michepuko utaisha? maana waswahili wanasema ukila nyama ya binadamu hautaacha ndo maana utaona hata mfalme Daudi pamoja na kuwa na wake zaidi ya mmoja bado akamnyatia mke wa mtu.
 
Wewe tumekuambia kama huwezi waachie wanaoweza hili sio la wote. Tofautisha mwanaume suruali na mwanaume wa familia ambao ndo wengi tupo kusapoti hili maana Lina tija.

Ustawi wa Watoto ni afya njema tu vingine ni ziada.

Ushauri wako hatujauzingatia maana hakuna sehemu tutakuomba Hela ulishe familia zetu. kwanza hatukujui na hatujuani
 
Hilo lisitusumbue kwa sasa.Tutaganga yajayo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…