Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KUAMINI NDOA NI MPAKA IFUNGWE KANISANI AU MSIKITINI NI DALILI YA UTUMWA NA UELEWA MDOGO KWA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Acha Dotto Magari adharau Wasomi. Ingawaje naamini hawadharau kwa mambo mazuri bali kwa baadhi ya ishu walizonazo. Hasa kifikra.

2. Fikiria binti aliyehitimu degree akiwa na ufaulu wa juu. Anaamini ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au Msikitini.

3. Au kijana wa kiume anaamini Ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au msikitini.

4. Ukiona mwanaume au mwanamke wanaishi pamoja kwa makubaliano ya kuwa mke na mume hiyo tayari ni ndoa.

5. Hakuna haja ya kwenda Kanisani
6. Hakuna haja ya kwenda Msikitini.

7. Mchungaji au Sheikhe hawachangii wala kuongeza chochote kwenye ndoa yenu. Chochote kile.

8. Oooh kubariki ndoa, sijui kuombea ndoa. Hakuna kitu kama hicho.

9. Ukipata kijana/binti, ukampenda, mkakubaliana. Mkaona mnaweza kufanya maisha pamoja.

10. Nenda kwa wazazi wake na wazazi wa mwenza wako kwa lengo la kuwashirikisha, kuwapata taarifa na kuwatambulisha.

11. Kama kuna zawadi toa. Kama hakuna sio lazima kutoa.

12. Lazima ni kuishi na mkeo/mumeo Kwa upendo, heshima, na Amani. Na sio vinginevyo.

13. Binti Yangu, ukipata mwanaume wakukuoa. Ukampenda. Achana na mambo ya kufikiri Sijui ndoa kanisani, au misikitini huko. Watibeli hatupo hivyo.

14. Mlete kijana huyo kwa wazazi wako. Mtambulishe tumfahamu. Aje akiwa huru sio mpaka ajipange. Ajipange nini? Ujingaujinga tuu.

15. Sisi Watibeli tunachohitaji ni Mpendane kama ulivyoniona mimi Babaako nilivyompenda Mama yako. Mheshimiane, mpeane haki, lakini pia msameheane Kwa makosa madogomadogo ya bila dhamiri. Makosa ya dhamiri hayasamehewi binti/kijana wangu.

16. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Duniani imeweka mifumo ambayo binadamu anatakiwa kuifuata ili tuishi kwa kuheshimiana..

Hata kutumia gari, ndege, pikipiki ni utumwa. Unatakiwa utumie punda na Farasi safari za Dar - Mwanza
Sio kila utaratibu ni wa kufuata,just imagine dini hizi sio zetu toka awali ni ustaarabu wa wazungu na waarabu but inatokea binti unampenda anakuambia mpaka mfunge ndoa ya kanisa.

Mama,Baba na babu zetu hawakufunga hizo ndoa za kanisa but ndio zao zilikuwa nzuri tu-siku hizi sasa.
 
Kuna binti namfahamu juzi kati amepata mchumba,kijana ni Muslim na binti kwao ni wakristo. Kijana yupi tayari kwenda kutoa mahali binti anasema yeye hawezi kubadili dini kuwa Muslim anasema labda kijana ndio abadilishe na kijana huyo radhi abadili ili amuoe binti lakini wazazi wake wamemkataza.

Sasa imagine dini ambazo sio zenu ni za waarabu na wazungu huko,zinaleta mgogoro mpaka watu wanaopendana wanashindwa kuoana.Ukirudi miaka 40-50 iliyopita hawa watu wangeishi pamoja maana jamii ilichukulia issue za dini kama njama za wazungu na waarabu kututawala
 
Duniani imeweka mifumo ambayo binadamu anatakiwa kuifuata ili tuishi kwa kuheshimiana..

Hata kutumia gari, ndege, pikipiki ni utumwa. Unatakiwa utumie punda na Farasi safari za Dar - Mwanza

Gari ni artificial
Ndoa sio artificial mzee
Ni kama Kula tuu

Wapo wanyama na ndege wenye kutumia mfumo wa ndoa naturally kama Simba, chui,n.k.
Ndege kama Njiwa kunguru n.k.
Binadamu naye mfumo wake ni wandoa.

Tofauti na wale wanyama wasio na mfumo wa ndoa natural kama Panya, Mbwa, Paka, Kuku n.k.

Unapofananisha mambo uhakikishe yanalengana kimfumo
 
KUAMINI NDOA NI MPAKA IFUNGWE KANISANI AU MSIKITINI NI DALILI YA UTUMWA NA UELEWA MDOGO KWA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Acha Dotto Magari adharau Wasomi. Ingawaje naamini hawadharau kwa mambo mazuri bali kwa baadhi ya ishu walizonazo. Hasa kifikra.

2. Fikiria binti aliyehitimu degree akiwa na ufaulu wa juu. Anaamini ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au Msikitini.

3. Au kijana wa kiume anaamini Ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au msikitini.

4. Ukiona mwanaume au mwanamke wanaishi pamoja kwa makubaliano ya kuwa mke na mume hiyo tayari ni ndoa.

5. Hakuna haja ya kwenda Kanisani
6. Hakuna haja ya kwenda Msikitini.

7. Mchungaji au Sheikhe hawachangii wala kuongeza chochote kwenye ndoa yenu. Chochote kile.

8. Oooh kubariki ndoa, sijui kuombea ndoa. Hakuna kitu kama hicho.

9. Ukipata kijana/binti, ukampenda, mkakubaliana. Mkaona mnaweza kufanya maisha pamoja.

10. Nenda kwa wazazi wake na wazazi wa mwenza wako kwa lengo la kuwashirikisha, kuwapata taarifa na kuwatambulisha.

11. Kama kuna zawadi toa. Kama hakuna sio lazima kutoa.

12. Lazima ni kuishi na mkeo/mumeo Kwa upendo, heshima, na Amani. Na sio vinginevyo.

13. Binti Yangu, ukipata mwanaume wakukuoa. Ukampenda. Achana na mambo ya kufikiri Sijui ndoa kanisani, au misikitini huko. Watibeli hatupo hivyo.

14. Mlete kijana huyo kwa wazazi wako. Mtambulishe tumfahamu. Aje akiwa huru sio mpaka ajipange. Ajipange nini? Ujingaujinga tuu.

15. Sisi Watibeli tunachohitaji ni Mpendane kama ulivyoniona mimi Babaako nilivyompenda Mama yako. Mheshimiane, mpeane haki, lakini pia msameheane Kwa makosa madogomadogo ya bila dhamiri. Makosa ya dhamiri hayasamehewi binti/kijana wangu.

16. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Makosa ya dhamiri ni kama yapi mkuu ili nimtimue huyu wangu
 
Wanaendekeza stress na huku wakimuhusisha Mungu wasomi wa hizi elimu za kuunga unga hawana ubongo kabisa
 
Duniani imeweka mifumo ambayo binadamu anatakiwa kuifuata ili tuishi kwa kuheshimiana..

Hata kutumia gari, ndege, pikipiki ni utumwa. Unatakiwa utumie punda na Farasi safari za Dar - Mwanza
Unataka kusemaje mkuu?
 
Back
Top Bottom