Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Ukweli ni kwamba mkiambiwa ukweli mnaona watu wanawachukia, ukweli mchungu

Ukimuacha mwanamke uliyemzalisha unataka akaolewe na nan? D

Ujinga uliyopitiliza na uzwazwa… Oa huyo mwanamke hatuwezi kuoa masingo maza kwa ujinga wenu na upumbavu.. ukimzalisha umuoe
Hayakuhusu ukweli ni upi na uongo ni upi wewe ndo hausomeki mpaka unabishia watu smart kama akina Mtibeli
 
KUAMINI NDOA NI MPAKA IFUNGWE KANISANI AU MSIKITINI NI DALILI YA UTUMWA NA UELEWA MDOGO KWA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Acha Dotto Magari adharau Wasomi. Ingawaje naamini hawadharau kwa mambo mazuri bali kwa baadhi ya ishu walizonazo. Hasa kifikra.

2. Fikiria binti aliyehitimu degree akiwa na ufaulu wa juu. Anaamini ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au Msikitini.

3. Au kijana wa kiume anaamini Ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au msikitini.

4. Ukiona mwanaume au mwanamke wanaishi pamoja kwa makubaliano ya kuwa mke na mume hiyo tayari ni ndoa.

5. Hakuna haja ya kwenda Kanisani
6. Hakuna haja ya kwenda Msikitini.

7. Mchungaji au Sheikhe hawachangii wala kuongeza chochote kwenye ndoa yenu. Chochote kile.

8. Oooh kubariki ndoa, sijui kuombea ndoa. Hakuna kitu kama hicho.

9. Ukipata kijana/binti, ukampenda, mkakubaliana. Mkaona mnaweza kufanya maisha pamoja.

10. Nenda kwa wazazi wake na wazazi wa mwenza wako kwa lengo la kuwashirikisha, kuwapata taarifa na kuwatambulisha.

11. Kama kuna zawadi toa. Kama hakuna sio lazima kutoa.

12. Lazima ni kuishi na mkeo/mumeo Kwa upendo, heshima, na Amani. Na sio vinginevyo.

13. Binti Yangu, ukipata mwanaume wakukuoa. Ukampenda. Achana na mambo ya kufikiri Sijui ndoa kanisani, au misikitini huko. Watibeli hatupo hivyo.

14. Mlete kijana huyo kwa wazazi wako. Mtambulishe tumfahamu. Aje akiwa huru sio mpaka ajipange. Ajipange nini? Ujingaujinga tuu.

15. Sisi Watibeli tunachohitaji ni Mpendane kama ulivyoniona mimi Babaako nilivyompenda Mama yako. Mheshimiane, mpeane haki, lakini pia msameheane Kwa makosa madogomadogo ya bila dhamiri. Makosa ya dhamiri hayasamehewi binti/kijana wangu.

16. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Ni imani tu kama tunavyoombea marehemu aende Mbinguni as if Mungu anasubiri sala zetu.
 
Kuna binti namfahamu juzi kati amepata mchumba,kijana ni Muslim na binti kwao ni wakristo. Kijana yupi tayari kwenda kutoa mahali binti anasema yeye hawezi kubadili dini kuwa Muslim anasema labda kijana ndio abadilishe na kijana huyo radhi abadili ili amuoe binti lakini wazazi wake wamemkataza.

Sasa imagine dini ambazo sio zenu ni za waarabu na wazungu huko,zinaleta mgogoro mpaka watu wanaopendana wanashindwa kuoana.Ukirudi miaka 40-50 iliyopita hawa watu wangeishi pamoja maana jamii ilichukulia issue za dini kama njama za wazungu na waarabu kututawala
Hiyo ni mikataba ya kilaghai mkuu, hakukuwa na upendo hapo
 
Ni imani tu kama tunavyoombea marehemu aende Mbinguni as if Mungu anasubiri sala zetu.

Ni kweli Kabisa.

Kuwa na hiyo Imani sio tatizo ila Imani hiyo kukugeuza mtumwa mambo yako yasikuendee hapo ndipo mimi naona tatizo.

Kwamba ushindwe kumzika Mpendwa wako kisa mchungaji kakataa kumuombea.
Si ndugi yeyote aendeshe ibada ya mazishi
 
KUAMINI NDOA NI MPAKA IFUNGWE KANISANI AU MSIKITINI NI DALILI YA UTUMWA NA UELEWA MDOGO KWA WATU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

1. Acha Dotto Magari adharau Wasomi. Ingawaje naamini hawadharau kwa mambo mazuri bali kwa baadhi ya ishu walizonazo. Hasa kifikra.

2. Fikiria binti aliyehitimu degree akiwa na ufaulu wa juu. Anaamini ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au Msikitini.

3. Au kijana wa kiume anaamini Ndoa ni mpaka ifungwe Kanisani au msikitini.

4. Ukiona mwanaume au mwanamke wanaishi pamoja kwa makubaliano ya kuwa mke na mume hiyo tayari ni ndoa.

5. Hakuna haja ya kwenda Kanisani
6. Hakuna haja ya kwenda Msikitini.

7. Mchungaji au Sheikhe hawachangii wala kuongeza chochote kwenye ndoa yenu. Chochote kile.

8. Oooh kubariki ndoa, sijui kuombea ndoa. Hakuna kitu kama hicho.

9. Ukipata kijana/binti, ukampenda, mkakubaliana. Mkaona mnaweza kufanya maisha pamoja.

10. Nenda kwa wazazi wake na wazazi wa mwenza wako kwa lengo la kuwashirikisha, kuwapata taarifa na kuwatambulisha.

11. Kama kuna zawadi toa. Kama hakuna sio lazima kutoa.

12. Lazima ni kuishi na mkeo/mumeo Kwa upendo, heshima, na Amani. Na sio vinginevyo.

13. Binti Yangu, ukipata mwanaume wakukuoa. Ukampenda. Achana na mambo ya kufikiri Sijui ndoa kanisani, au misikitini huko. Watibeli hatupo hivyo.

14. Mlete kijana huyo kwa wazazi wako. Mtambulishe tumfahamu. Aje akiwa huru sio mpaka ajipange. Ajipange nini? Ujingaujinga tuu.

15. Sisi Watibeli tunachohitaji ni Mpendane kama ulivyoniona mimi Babaako nilivyompenda Mama yako. Mheshimiane, mpeane haki, lakini pia msameheane Kwa makosa madogomadogo ya bila dhamiri. Makosa ya dhamiri hayasamehewi binti/kijana wangu.

16. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Upo sahihi 💯% mkuu. Nakubaliana nawe 100 kwa 100. Kufunga ndoa kanisani au msikitini, ni ushamba na kuendekeza ukoloni.
 
Upo sahihi 💯% mkuu. Nakubaliana nawe 100 kwa 100. Kufunga ndoa kanisani au msikitini, ni ushamba na kuendekeza ukoloni.
Tafsiri halisi ya ndoa ni pale wawili wanapokutana kimwili full stop ndo maana kanisa takatifu linatambua ndoa za kimila kama ndoa halali
 
Hayakuhusu ukweli ni upi na uongo ni upi wewe ndo hausomeki mpaka unabishia watu smart kama akina Mtibeli
Huyo smart kwako tu Mkuu

Ila hamna chochote anachojenga humu ni vilee tu watu wanapenda story

Utazidi kuwa jinga ukiendekeza ujinga mjinga wew
 
Nje Kidogo ya Mada : Hata kuamini kuwa kuna moto unawaka milele na watu watateswa milele ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo wa kifikra
 
Huyu jamaa kwa Ufahamu wangu mdogo niliopewa na Mnyaaz, anataka kuanzisha kitu chake sasa sijui tukiite dini, au jina tu au legacy sijui. Nikiite dini.

Sasa nishamfumania akisema Yesu ni mtu kama wewe na mimi tu, wa kawaiiida, akam group kundi moja na Muhammad na wengine.

Na nimemfumania akisema Biblia ni kijitabu tu cha watu eti ukijua kuandika andika vitu utawapata watu wa kukupandisha hadhi kukuita mtume, nabii, mungu etc.

Kwahiyo namuona ndo yuko kwenye harakati za kufanya kitu kama hicho.

Me nilishasema hapa na narudia:

Post in thread 'Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)' Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)

Ukitaka kutengeneza kitabu kikuu kuliko Biblia:

1)  Kwanza ufe, na tuhakikishe umekufa kama walivyohalikisha YESU amekufa kwa kumchoma kwenye mapafu na maji kutoka.

2) Kisha Ufufuke baada ya kuzikwa huko chini baada ya siku tatu wakati ushaoza. Tuweke na walinzi kabisa maadui zako ambao hawakukubali kama waliowekwa kulinda kaburi la YESU. Tuje tufukue tukute mwili haupo. Tukuone live ikiwezekana na uthibitisho wa majeraha yaliyokuua yawepo.

3) Halafu Kuwe na unabii kukuhusu ulioandikwa kabla hujazaliwa wa matukio yasiyopungua 300 kukuhusu, kuanzia kutungwa kwa mimba yako, kama ilivyo kwa YESU.

4) Na Ufanye miujiza kama YESU : wenye magonjwa ya ajabu yasiyotibika wapone, vipofu waone, viwete watembee, wafu wafufuliwe.

5) Wafuasi wako wa kwanza wakubali kuteswa na kuuawa ili kutoa ushuhuda kukuhusu, wakati hakuna faidia yoyote wanayopata hapa duniani sio utajri sio umaarufu sio wanawake, zaidi ni kudharauliwa na kuteswa, kama wanafunzi wa YESU.

6) Wafuasi wako angalau watano waandike yote haya uliyofanya, kila mtu kivyake. Kisha wawarithishe wanafunzi wao masimulizi kukuhusu. Na wanafunzi wao wawarithishe wenzao. Tuwape miaka 300.

Kisha wataalam wa forensics kina J. Warner Wallace watuambie hawa jamaa kwenye hiki kitabu cha huyu Mtibeli wamejitungia story au ni historia ya kweli inapitishwa kama ile iliyopitishwa na wanafunzi wa YESU.

Hapa miezi miwili tu chukua makala za huyu ajiitaye mtibeli utakuta ashajikanganya. Nakumbuka zamani aliwahi kusema mtu mzuri hajisifii uzuri anayejisifia sio mzuri. Baadae nikamfumania anasema yeye mzuri 😂. Nikasema hiii bagosha binadamu eniweis....

7) Mwisho kabisa ingepedeza kama ungepita rekodi hii:

kitabu chako kiwe na
vitabu angalau 60,
vilivyoandikwa na watu angalau 40
kwa miaka isiyopungua 1,500
wote wakikuongelea wewe tu kwa upatano na uelewano kama mtu mmoja,
kwa namna mbalimbali: masimulizi halisi ya historia, sheria, unabii, nyimbo, methali, mafumbo n.k
kama vile Biblia inavyomuongelea YESU.


Sasa kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache maana hadi miaka 1500 twafwaz, Ungeanza tu na hizo step mbili za mwanzo tumalize kazi chap, mimi nitamkana Yesu LIVE nikusujudie
:gachiCOOL:
Yaani!!
Mwishowe anaandika vitu ambayo havi make sense!
 
Back
Top Bottom