Huyu jamaa kwa Ufahamu wangu mdogo niliopewa na Mnyaaz, anataka kuanzisha
kitu chake sasa sijui tukiite dini, au jina tu au legacy sijui. Nikiite
dini.
Sasa
nishamfumania akisema Yesu ni mtu kama wewe na mimi tu, wa
kawaiiida, akam group kundi moja na Muhammad na wengine.
Na
nimemfumania akisema Biblia ni
kijitabu tu cha watu eti ukijua kuandika andika vitu utawapata watu wa kukupandisha hadhi kukuita mtume, nabii, mungu etc.
Kwahiyo namuona ndo yuko kwenye
harakati za kufanya kitu kama hicho.
Me nilishasema hapa na narudia:
Post in thread 'Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)'
Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)
Ukitaka kutengeneza kitabu kikuu kuliko Biblia:
1) Kwanza
ufe, na tuhakikishe umekufa kama walivyohalikisha YESU amekufa kwa kumchoma kwenye mapafu na maji kutoka.
2) Kisha
Ufufuke baada ya kuzikwa huko chini baada ya siku tatu wakati ushaoza. Tuweke na walinzi kabisa
maadui zako ambao hawakukubali kama waliowekwa kulinda kaburi la
YESU. Tuje tufukue tukute mwili haupo. Tukuone live ikiwezekana na uthibitisho wa majeraha yaliyokuua yawepo.
3) Halafu Kuwe na
unabii kukuhusu ulioandikwa kabla hujazaliwa wa matukio yasiyopungua
300 kukuhusu, kuanzia kutungwa kwa mimba yako, kama ilivyo kwa
YESU.
4) Na Ufanye
miujiza kama
YESU : wenye magonjwa ya ajabu yasiyotibika wapone, vipofu waone, viwete watembee, wafu wafufuliwe.
5)
Wafuasi wako wa kwanza wakubali
kuteswa na
kuuawa ili kutoa ushuhuda kukuhusu, wakati
hakuna faidia yoyote wanayopata hapa duniani sio utajri sio umaarufu sio wanawake, zaidi ni kudharauliwa na kuteswa, kama wanafunzi wa
YESU.
6) Wafuasi wako angalau watano
waandike yote haya uliyofanya, kila mtu kivyake. Kisha wawarithishe wanafunzi wao masimulizi kukuhusu. Na wanafunzi wao wawarithishe wenzao. Tuwape miaka 300.
Kisha
wataalam wa forensics kina J. Warner Wallace watuambie hawa jamaa kwenye hiki kitabu cha huyu Mtibeli wamejitungia story au ni historia ya kweli inapitishwa kama ile iliyopitishwa na wanafunzi wa YESU.
Hapa miezi miwili tu chukua makala za huyu ajiitaye mtibeli utakuta ashajikanganya. Nakumbuka zamani aliwahi kusema mtu mzuri hajisifii uzuri anayejisifia sio mzuri. Baadae nikamfumania anasema yeye mzuri 😂. Nikasema hiii bagosha binadamu eniweis....
7) Mwisho kabisa ingepedeza kama ungepita
rekodi hii:
kitabu chako kiwe na
vitabu angalau 60,
vilivyoandikwa na
watu angalau 40
kwa
miaka isiyopungua 1,500
wote wakikuongelea
wewe tu kwa upatano na uelewano kama mtu mmoja,
kwa namna mbalimbali: masimulizi halisi ya historia, sheria, unabii, nyimbo, methali, mafumbo n.k
kama vile
Biblia inavyomuongelea
YESU.
Sasa kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache maana hadi miaka 1500 twafwaz, Ungeanza tu na hizo
step mbili za mwanzo tumalize kazi chap, mimi
nitamkana Yesu LIVE nikusujudie