Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Duniani imeweka mifumo ambayo binadamu anatakiwa kuifuata ili tuishi kwa kuheshimiana..

Hata kutumia gari, ndege, pikipiki ni utumwa. Unatakiwa utumie punda na Farasi safari za Dar - Mwanza
Huyu Mtibeli ni mbishi tu. Ataandika kitu kisicho na mashiko, akipambe na maneno mengi, kisha aje abishane tu ndo furaha yake.

Anataka kujifanya hajui nguvu ya mapokeo ya kijamii.
 
Kuna binti namfahamu juzi kati amepata mchumba,kijana ni Muslim na binti kwao ni wakristo. Kijana yupi tayari kwenda kutoa mahali binti anasema yeye hawezi kubadili dini kuwa Muslim anasema labda kijana ndio abadilishe na kijana huyo radhi abadili ili amuoe binti lakini wazazi wake wamemkataza.

Sasa imagine dini ambazo sio zenu ni za waarabu na wazungu huko,zinaleta mgogoro mpaka watu wanaopendana wanashindwa kuoana.Ukirudi miaka 40-50 iliyopita hawa watu wangeishi pamoja maana jamii ilichukulia issue za dini kama njama za wazungu na waarabu kututawala
Kwa nini wasingefunga ndoa ya serikali kila mtu abaki na dini yake?
 
Kuna binti namfahamu juzi kati amepata mchumba,kijana ni Muslim na binti kwao ni wakristo. Kijana yupi tayari kwenda kutoa mahali binti anasema yeye hawezi kubadili dini kuwa Muslim anasema labda kijana ndio abadilishe na kijana huyo radhi abadili ili amuoe binti lakini wazazi wake wamemkataza.

Sasa imagine dini ambazo sio zenu ni za waarabu na wazungu huko,zinaleta mgogoro mpaka watu wanaopendana wanashindwa kuoana.Ukirudi miaka 40-50 iliyopita hawa watu wangeishi pamoja maana jamii ilichukulia issue za dini kama njama za wazungu na waarabu kututawala


Mimi miaka kadhaa iliyopita, mchumba wangu aliniuliza mimi dini gani. Nikamwambia achana na mambo ya dini.

Dini haisaidii chochote kwenye mahusiano yetu.
Baadaye Sana karibu mwaka akagundua ninasali sabato.
Akaniambia abadilishe kutoka Roma awe Msabato. Nikamwambia haina mana yoyote

Haitaongeza wala kupunguza chochote. Kama ningehitaji binti Msabato ningeoa huko usabatoni.

Mimi ninaangalia Tabia na imani kuliko dini. Factors zingine zikiwa palepale.

Baada ya miaka 5 kwa mara Kwanza tunaenda kanisani.
Siku mwambia abadili dini. Alibadili mwenyewe baadaye. Na nilimuambia unabadili Siku nimekuacha utaacha dini mpaka lini. Akasema hajabadili kwaajili Yangu.

Mara ya Kwanza tunaenda kwa wazazi wangu. Nikawa nimemvalisha suruali.
Akaniambia hawezi kuvaa suruali akienda ukweni tena mara ya kwanza

Nikamwambia vaa tuu. Sio tatizo.
Akavaa, hao tukalala Dodoma Siku mbili,
Hao tukafika Arusha, tukakaa pale Siku mbili.

Sasa safari ya kwenda home, Moshi kwa Wazazi wangu ikafika.
Siku hiyo usiku akaniambia Mimi kwa kweli sijisikii comfortable kuvaa suruali mbele ya Wakwe zangu.

Nikamwambia avae anavyosikia comfortable
Siku tulipoenda akawa amevaa gauni zuri.

Wazazi walifurahi Sana.
Tukiwa wote nikawa nahadithia hiyo situation. Wazazi wakawa wanacheka kweli.

Nikamwambia kesho asubuhi tusijemkuta yupo juu ya paa anasafisha paa na kutoa tando za buibui ili aonekane Wife material au isemwe Robert amepata Mke.

Nilimwambia Robert hapendi Wema au tabia njema za ku-fake.
Aishi kama tunavyoishi au anavyoishi kwao

Basi tulikaa pale wiki moja na nusu. Tukifurahi sana.

Baadaye tukaenda Kwao. Mambo yalienda hivyo.

Niliwaambia Wakwe zangu mambo ya ku-fake fake kwa kweli hayatanifurahisha na niliongea waziwazi.

Ni Bora Nile ugali mlenda kwa uwezo halisi kuliko mnikaribishe kwa kujibana, kukopa ili mnipikie manyama, sijui mavyakula gani.
Sisi Watibeli hatufurahishwi na ukaribisho fake wa mavyakula na vinywaji.

Mimi nikija kwako, endelea na ratiba yako ya kawaida ya kula. Kama ni ugali nitakula ugali. Hayo mambo ya maandalizi kwangu ni utapeli.

Ukweli, uwazi, humweka mtu huru. Huleta furaha ya kweli.

Hayo yote vijana wanatakiwa wafundishwe.
 
Sio kila utaratibu ni wa kufuata,just imagine dini hizi sio zetu toka awali ni ustaarabu wa wazungu na waarabu but inatokea binti unampenda anakuambia mpaka mfunge ndoa ya kanisa.

Mama,Baba na babu zetu hawakufunga hizo ndoa za kanisa but ndio zao zilikuwa nzuri tu-siku hizi sasa.
Basi ziache hizo dini sasa uone moto wake...

Hakuna mtu amezaliwa akijua hizi "taratibu". Ukizaliwa wewe ni kama karatasi nyeupe, mapokeo na tamaduni za jamii yako hujaza hiyo karatasi na kukufanya uwe wewe.

Ubishi hausaidii. Pengine utaweza kukataa taratibu moja lakini utafuata zingine nyingi. Chamsingi usiwashangae walioamua kutii taratibu.
 
Adam na Hawa walifunga ndoa kanisa gani? Na watoto wao walifunga ndoa parokia ipi?
Una point japo nao ni fiction story tu.
Hukuna tatizo ndoa kufungwa ila ujima wa Waafrika wengi ni huko kufikiri ndoa inafungwa kanisani au msikitini tu kumbe wenzetu sasa hivi ndoa wanafungia popote iwe nyumbani, hotelini n.k
 
Huyu Mtibeli ni mbishi tu. Ataandika kitu kisicho na mashiko, akipambe na maneno mengi, kisha aje abishane tu ndo furaha yake.

Anataka kujifanya hajui nguvu ya mapokeo ya kijamii.

Hakuna nguvu yoyote

Kwa kukujulisha tuu.
Zaidi ya Robo tatu ya Watanzania ndoa zao sio za kanisani wala msikitini.

Kwamba kwenye watu kumi unaowajua waliooa/kuolewa(wanaoishi kindoa) watu Saba hawajafungaa ndoa kanisani wala misikitini
 
Kanisani au Msikitini ni kwaajili ya uthibitisho rasmi unaotambulika, ni kama bidhaa inavyotakiwa kuthibitishwa kwanza na TBS

kwaiyo inaweza kuwa nzuri na haijathibitishwa

😂😂😂

Unafurahisha Sana.

Ndoa inathibitishwa na Mke na mume kuishi vizuri, kupendana, kuheshimiana, kuthaminiana.

Serikali, kanisa, msikiti haithibitishi ndoa.

Uwepo wa ndoa ni makubaliano ya watu wawili. Na wahusika wengine wanaoshirikishwa na wazazi au ndugu wakaribu kama walezi. Ila mhusika mkuu ni Wanandoa wenyewe
 
Sawa sawa na useme kutumia simu ni ushamba, na kuhimiza tuache matumizi ya computer mara AI.. na social media

Ustaarabu unakua , mambo yanaendelea

Zamani ndio ilikuwa hivyo, mkipendana hakuna cha msikiti wala kanisa, wazazi wana wapa baraka muende mkaanze maisha mema

Sasa hivi mambo yameendelea sana , hakuna ubaya wowote kwenda kanisani wala msikitini kubariki ndoa ni njia au maendeleo mazuri tu na binafsi yako hata wewe ulifanya hivyo au utafanya hivyo, umeleta uzi tu kuchangamsha baraza

Msikitini/kanisa ni mbadala wa Serikali katika maswala ya ndoa, serikali itajua kuwa ndoa yako imepita kutokana na wewe kupita msikitini au kanisani hakuna serikali za mtaa zitapeleka ujumbe kuwa Fulani na fulani wameoana

Nahitaji kuandika sana ila hii inatosha
 
Makosa ya dhamiri ni kama yapi mkuu ili nimtimue huyu wangu

😄😄

Hapana usiwaze kumtimua mtu

Pia usimuadhibu mtu kwa kosa ambalo hukumwonya au hukumwambia hapo kabla.
Usije sema kwani yeye hajui. Atasema alikuwa hajui au hakufikiri ni uzito kiasi gani

Makosa ya dhamiri ni kama Ku-cheat, kuua au jaribio la mauaji, uchawi.
Haya unafukuzwa bila kikao.

Makosa ya dhamiri yanayorudiwa mara kwa mara kimakusudi.
Unamkata Jambo Fulani. Hata kama Jambo hilo ni dogo analirudia mara kwa mara (sio mtiifu) unampa adhabu ndogondogo mama kumrudisha kwao.
Ukiona habadiliki unapiga chini
 
Kanisani au Msikitini ni kwaajili ya uthibitisho rasmi unaotambulika, ni kama bidhaa inavyotakiwa kuthibitishwa kwanza na TBS

kwaiyo inaweza kuwa nzuri na haijathibitishwa
Ujerumani na Austria makanisa hayafungishi ndoa kabla hamjafungishwa na serikali ya mtaa na kupeleka cheti cha ndoa kanisani. Ndoa inarasimishwa na serikali ya mtaa halafu kanisani mnaenda tu kuongezea sherehe kama mnataka.
 
Sawa sawa na useme kutumia simu ni ushamba, na kuhimiza tuache matumizi ya computer mara AI.. na social media

Ustaarabu unakua , mambo yanaendelea

Zamani ndio ilikuwa hivyo, mkipendana hakuna cha msikiti wala kanisa, wazazi wana wapa baraka muende mkaanze maisha mema

Sasa hivi mambo yameendelea sana , hakuna ubaya wowote kwenda kanisani wala msikitini kubariki ndoa ni njia au maendeleo mazuri tu na binafsi yako hata wewe ulifanya hivyo au utafanya hivyo, umeleta uzi tu kuchangamsha baraza

Msikitini/kanisa ni mbadala wa Serikali katika maswala ya ndoa, serikali itajua kuwa ndoa yako imepita kutokana na wewe kupita msikitini au kanisani hakuna serikali za mtaa zitapeleka ujumbe kuwa Fulani na fulani wameoana

Najitaji kuandika sana ila hii inatosha

Simu ni man made
Ndoa sio man made ni Jambo naturally

Dini ni man made
Imani ni naturally

Elimu ni man made
Akili ni naturally

Ukiwa unazungumzia mambo jitahidi uyaangalie katika upana wake.

Kingine, sijasema kwenda kanisani au Msikitini kuna ubaya.
Mimi nazungumzia sio lazima. Yaani mtu asiwe mtumwa, au asiache kuwa ndoani kisa mambo ya kanisani na misikitini ambapo ni miradi au mifumo ya watu kama Mimi na wewe.
 
Sawa sawa na useme kutumia simu ni ushamba, na kuhimiza tuache matumizi ya computer mara AI.. na social media

Ustaarabu unakua , mambo yanaendelea

Zamani ndio ilikuwa hivyo, mkipendana hakuna cha msikiti wala kanisa, wazazi wana wapa baraka muende mkaanze maisha mema

Sasa hivi mambo yameendelea sana , hakuna ubaya wowote kwenda kanisani wala msikitini kubariki ndoa ni njia au maendeleo mazuri tu na binafsi yako hata wewe ulifanya hivyo au utafanya hivyo, umeleta uzi tu kuchangamsha baraza

Msikitini/kanisa ni mbadala wa Serikali katika maswala ya ndoa, serikali itajua kuwa ndoa yako imepita kutokana na wewe kupita msikitini au kanisani hakuna serikali za mtaa zitapeleka ujumbe kuwa Fulani na fulani wameoana

Najitaji kuandika sana ila hii inatosha
Hiyo ya wazazi kutoa baraka ilikuwa ndio ustaarabu zaidi kuliko sasa ambapo watu wanahangaika na makanisa na misikiti pamoja na michango ya kukabana koo.
 
Hiyo ya wazazi kutoa baraka ilikuwa ndio ustaarabu zaidi kuliko sasa ambapo watu wanahangaika na makanisa na misikiti pamoja na michango ya kukabana koo.
Bado wazazi wanatoa baraka kama kawaida

ila kuna mamlaka zinatakiwa zipate taarifa.. teacher
 
😄😄

Hapana usiwaze kumtimua mtu

Pia usimuadhibu mtu kwa kosa ambalo hukumwonya au hukumwambia hapo kabla.
Usije sema kwani yeye hajui. Atasema alikuwa hajui au hakufikiri ni uzito kiasi gani

Makosa ya dhamiri ni kama Ku-cheat, kuua au jaribio la mauaji, uchawi.
Haya unafukuzwa bila kikao.

Makosa ya dhamiri yanayorudiwa mara kwa mara kimakusudi.
Unamkata Jambo Fulani. Hata kama Jambo hilo ni dogo analirudia mara kwa mara (sio mtiifu) unampa adhabu ndogondogo mama kumrudisha kwao.
Ukiona habadiliki unapiga chini
Nimekupata mkuu
 
Back
Top Bottom