Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Kuamini ndoa ni Mpaka ifungwe kanisani au Msikitini ni dalili ya utumwa na uelewa mdogo kwa watu

Kwa nini wasingefunga ndoa ya serikali kila mtu abaki na dini yake?
watu wengi hamjui dhana nzima ya ndoa. Kuthibishwa kanisani au msikitini au na serikali ndio kutafanya ndoa idumu?
 
Simu ni man made
Ndoa sio man made ni Jambo naturally

Dini ni man made
Imani ni naturally

Elimu ni man made
Akili ni naturally

Ukiwa unazungumzia mambo jitahidi uyaangalie katika upana wake.

Kingine, sijasema kwenda kanisani au Msikitini kuna ubaya.
Mimi nazungumzia sio lazima. Yaani mtu asiwe mtumwa, au asiache kuwa ndoani kisa mambo ya kanisani na misikitini ambapo ni miradi au mifumo ya watu kama Mimi na wewe.
Mtu akiwa anasoma nyuzi zako anaweza akasema iki kijamaa kina uelewa sana kumbe sivyo

Tunaombea uendelee kuwepo kuchangamsha JF.. unapendezesha sana

Maelezo mengi hapo umeyatoa lakini binafs sijaamua kukuelewa

Hata mimi pia sijasema kwenda kanisani na msikitini kama kuna ubaya hauwezi ukafanya mambo kama ya mwaka 1921 wakati huu ni mwaka 2026
 
Hizo ni imani za watu, hapa unashambulia imani za watu.
Sio kwamba watu/mtu anakua hajui hilo, ni imani yake. Mtu kazaliwa, kakua katika dini flani, ni haki yake kumaliza maisha yake yaliyobaki kwa dini/imani husika.
 
1) Nyie nmaosema dini dini mnafikiri mna akili sana but truly truly mko kama mmekatwa vichwa!

Wewe kama unajiona ni Sokwe uliyechangamka basi tafuta sokwe mwenzio muambatane msokwenke zenu.

Na waache waliotafuta KWELI ya haya maisha nao waambatane, whether hiyo kweli waliisikia kwa mara ya kwanza kwa mzungu, mchina, Alien...KWELI ni KWELI jana leo na kesho haibadiliki, isemwe na muafrika, muhindi haibadiliki, ikubalike na mmoja ikataliwe na mamilioni haibadiliki.

KWELI ni KWELI.

Kwahiyo waacheni walioipata KWELI na kuamua kuiishi waiishi, na mnaoishi kufuata tamaduni za mababu zenu, hisia zenu, mawazo yenu, matamanio yenu, trend za jamii.. vinavyobadilika kila kukicha na nyie ishini humo.

Lakini UKWELI ni kuwa huu ulimwengu una mwenyewe, ana mpango wake, na anakuja 🔥🔥🔥🔥🔥🔥


2) Btw, yes Ndoa kwa Mkristo ni Agano, na Agano sio maneno bla bla ya kuigiza mbele za watu, Agano ni vitendo.

So wewe kwenda kubwabwaja kuwa utampenda na kuwa muaminifu halafu hauishi hayo maneno, kisha useme na wewe una agano / ndoa takatifu kisa askofu aliwachorea msalaba, hayo tunayaita maigizo.

By the way kanuni ya Kimungu ni kila kitu kiwe na angalau mashahidi wawili.

So wachumba Wakristo wanaotaka kuweka agano la ndoa lazima washuhudiwe na angalau watu wawili.

“Kila tatizo litatatuliwa kwa ushahidi wa watu wawili au watatu,” yasema Maandiko."
2Wakorintho.13.1.BHN


"Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa."
Kumbukumbu.19.15.BHN


"Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe."
Mathayo.18.16.BHN


3) Plus mwenye akili aliona hatari na kujificha. Mwerevu anajifunza na makosa ya wenzake sio hadi yeye apite humo humo alipoona mwenzake kaanguka na yeye aanguke. So hatutegemei mwanamke mwenye akili leo hii atakubali kuishi bila ndoa inayotambulika kisheria.
 
Mtu akiwa anasoma nyuzi zako anaweza akasema iki kijamaa kina uelewa sana kumbe sivyo

Tunaombea uendelee kuwepo kuchangamsha JF.. unapendezesha sana

Maelezo mengi hapo umeyatoa lakini binafs sijaamua kukuelewa

Hata mimi pia sijasema kwenda kanisani na msikitini kama kuna ubaya hauwezi ukafanya mambo kama ya mwaka 1921 wakati huu ni mwaka 2026

Sasa mimi na mtazamo wako nani anamawazo ya mwaka 1921 huko?

Unajikanganya Mzee
 
Kanisani, msikitini ni ushahidi.
 
We nae unaolekea wewe...
Haya
Huyu jamaa kwa Ufahamu wangu mdogo niliopewa na Mnyaaz, anataka kuanzisha kitu chake sasa sijui tukiite dini, au jina tu au legacy sijui. Nikiite dini.

Sasa nishamfumania akisema Yesu ni mtu kama wewe na mimi tu, wa kawaiiida, akam group kundi moja na Muhammad na wengine.

Na nimemfumania akisema Biblia ni kijitabu tu cha watu eti ukijua kuandika andika vitu utawapata watu wa kukupandisha hadhi kukuita mtume, nabii, mungu etc.

Kwahiyo namuona ndo yuko kwenye harakati za kufanya kitu kama hicho.

Me nilishasema hapa na narudia:

Post in thread 'Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)' Nipo mbioni kufungua dini yangu (imani mpya ya kuabudu)

Ukitaka kutengeneza kitabu kikuu kuliko Biblia:

1)  Kwanza ufe, na tuhakikishe umekufa kama walivyohalikisha YESU amekufa kwa kumchoma kwenye mapafu na maji kutoka.

2) Kisha Ufufuke baada ya kuzikwa huko chini baada ya siku tatu wakati ushaoza. Tuweke na walinzi kabisa maadui zako ambao hawakukubali kama waliowekwa kulinda kaburi la YESU. Tuje tufukue tukute mwili haupo. Tukuone live ikiwezekana na uthibitisho wa majeraha yaliyokuua yawepo.

3) Halafu Kuwe na unabii kukuhusu ulioandikwa kabla hujazaliwa wa matukio yasiyopungua 300 kukuhusu, kuanzia kutungwa kwa mimba yako, kama ilivyo kwa YESU.

4) Na Ufanye miujiza kama YESU : wenye magonjwa ya ajabu yasiyotibika wapone, vipofu waone, viwete watembee, wafu wafufuliwe.

5) Wafuasi wako wa kwanza wakubali kuteswa na kuuawa ili kutoa ushuhuda kukuhusu, wakati hakuna faidia yoyote wanayopata hapa duniani sio utajri sio umaarufu sio wanawake, zaidi ni kudharauliwa na kuteswa, kama wanafunzi wa YESU.

6) Wafuasi wako angalau watano waandike yote haya uliyofanya, kila mtu kivyake. Kisha wawarithishe wanafunzi wao masimulizi kukuhusu. Na wanafunzi wao wawarithishe wenzao. Tuwape miaka 300.

Kisha wataalam wa forensics kina J. Warner Wallace watuambie hawa jamaa kwenye hiki kitabu cha huyu Mtibeli wamejitungia story au ni historia ya kweli inapitishwa kama ile iliyopitishwa na wanafunzi wa YESU.

Hapa miezi miwili tu chukua makala za huyu ajiitaye mtibeli utakuta ashajikanganya. Nakumbuka zamani aliwahi kusema mtu mzuri hajisifii uzuri anayejisifia sio mzuri. Baadae nikamfumania anasema yeye mzuri 😂. Nikasema hiii bagosha binadamu eniweis....

7) Mwisho kabisa ingepedeza kama ungepita rekodi hii:

kitabu chako kiwe na
vitabu angalau 60,
vilivyoandikwa na watu angalau 40
kwa miaka isiyopungua 1,500
wote wakikuongelea wewe tu kwa upatano na uelewano kama mtu mmoja,
kwa namna mbalimbali: masimulizi halisi ya historia, sheria, unabii, nyimbo, methali, mafumbo n.k
kama vile Biblia inavyomuongelea YESU.


Sasa kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache maana hadi miaka 1500 twafwaz, Ungeanza tu na hizo step mbili za mwanzo tumalize kazi chap, mimi nitamkana Yesu LIVE nikusujudie
:gachiCOOL:
 

Attachments

  • IMG_9309.png
    IMG_9309.png
    131.8 KB · Views: 13
Duniani imeweka mifumo ambayo binadamu anatakiwa kuifuata ili tuishi kwa kuheshimiana..
Hatakiwi kalazimishwa na kushawishiwa tu ili biashara ipate wateja
Hata kutumia gari, ndege, pikipiki ni utumwa. Unatakiwa utumie punda na Farasi safari za Dar - Mwanza
Vyombo vya moto ni aina mpya ya usafili ambao faida ake iko wazi... ni biashara inayotoa manufaa kwa pande zote mbili(mtumiaji /mtengenezaji)
 
Endelea kutushahuri basi ili dunia ikusikilize unavyosema iache kuwafata wenye akili zao

Kushauriwa na mimi ni hiyari yako Mkuu. Hakuna aliyekuita ushauriwe na Mimi.
Dunia inawatu wengi, na Kila mtu na makundi yanadunia yao

Ndio maana kuna dunia ya Sisi watibeli na watu wengine. Kuna dunia yako na Jamii na watu wenye mtazamo na akili kama zako
 
Back
Top Bottom