Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Somo tajwa hapo juu lahusika.

Ukiona mtu amedondoka chooni au bafuni ujue lazima tu amerogwa au kapigwa chuma ulete. Na mara nyingi hutokea kwenye vyoo au bafu zilizofunika ( vya ndani), maana ndo sehemu pendwa ya majini.Majini hayapendi vyoo na bafu za wazi juu. Na yanapenda sana mahala pasafi.

Ukidondoka lazima tu utakuwa umetupiwa jini fulani na mtaalam ! Ukizimia ukaamka ujue limekukosa kosa tu lakini haliondoki hiyo sehemu mpaka likamilishe lengo lake.

Jipange ndugu.
Nasikia kuna Dua inapigwa kabla ya kuingia chooni.
 
Watu wanadondoka kwa sababu. Unakuta mtu ametoka usingizini anaenda msalani.ukiwa umelala mwili una relax. Ukiamka ghafla na kutembea inakua shida. Ndo maana wataalau wanashauri ukiwa umelala na unataka kuamka inabidi uamke halafu ukae kitandani miguu ikiwa chini kwa muda ili mwili uwe ktk hali ya kawaida halafu ndo usimame uanze kutembea. Tofauti na hivyo ni shida.
 
pona pona yako unapata stroke/kiharusi, hii watu weng sana imewatoke. Sababu ya hii inaelezeka hata kisayansi, imani nyingne naskia ipo ila mimi sina fact. Na hii ya kufa mi sijui
 
sasa ndio inaitwa chuma ulete!!!utashitakiwa na wanajamii kwa kuandika vitu tofauti.
 
Kwa iq fupi kama hizi mtukufu endelea kukaza vyuma mpaka wajitambue!!
Naomba niishie hapa.
 
Wanaojisaidia vichakani wakidondoka wanaruhusiwa kusema wamedondoka chooni?
 
kwa kawaida watu wenye magonjwa ya moyo na wanatumia dawa fulani hushauriwa. kutosimama kwa muda mrefu na wanaume wanatakiwa kukojoa wakiwa wamekaa. Mbali na hivyo huwa katika hatari ya kuanguka kwa kizunguzungu. Ndiyo maana wengi wanaoanguka chooni huwa wanaume.
Hizo takwimu umezitoa wapi
 
Kuna wengine huwa wanadondoka pindi wanapojimwagia maji ya baridi ilhali mwili ni wa joto
Matokeo yake huwa ni mabaya
Hayo mengine yapo na wengine kupigwa kofi kabisa
Yaani jiandae kwa mengi
 
Nnesha dondoka chooni Mara mbili na sikua chochote,Mara ya kwanza niliogopa sana maana nlisikia ukiabguka choon kuna hatihati ya kupooza,sikua hivyo!;
 
Back
Top Bottom