Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Nilipata kusema humu kwamba kwa namna Samia asivyo na nia ya dhati kwa aliyokuwa akikubaliana na Mbowe litakuwa ni suala la wakati tu wawili hao kutofautiana tena.
Baadhi yetu kwa siku za hivi karibuni tumekiona CHADEMA kama kimefifishwa kwa maneno matamu ya Samia na CCM yake lakini ukweli haupo hivyo tudhanivyo bali Chadema walijipa tu mda wa kuona yaahidiwayo na Samia na CCM yake yakitimu jambo ambalo hadi leo blah-blah ni nyingi pasipo matendo.
Tuitarajie CHADEMA inayoenda kumsumbua Samia isivyokuwa ikitarajiwa!
Fimbo ya CHADEMA kumchapia Samia imerahisishwa na yafuatayo:
Ukosefu wa umeme wa uhakika, ukosefu wa maji safi na salama hasa Dar es Salaam, miradi mingi ya umeme vijijini kukwama, rushwa na ufisadi kurejea kwa kasi, huduma za afya kuendelea kuwa duni, mafisadi kurejeshwa kwenye mstari na GHARAMA ZA MAISHA KUPANDA HASA MFUMKO WA BEI WA MAHITAJI MUHIMU.
2023 na kuendelea itakuwa ni uwanja mchungu wa mapambano kwa Samia.