Ushauri wa maana kwa bimkubwa awaachie tu kiti akapumzike hii mikikimikiki yote ya nini??? Ameshakaa miaka 4 ameshaweka historia basi. A good dancer should know the time to the stage.
Kama ningekuwa mimi ndo bimkubwa nawachonganisha huku nikiacha alama kudadeki.
Kwa mfano....
Mimi sasa ndo bimkubwa:..Katiba ya Mzee Warioba ipo wapi,..? nataka ile original.
Wao sasa:..Hii hapa mama!.
Mimi:.okk, hii sindo waliyoipitisha wananchi wakataka iwe hivi???
Wao: ehhh
Mimi: Kesho toa taarifa nataka kuongea na Taifa.
Wao: Kwani kuna nini mama!!
Mimi: Nimesema toa taarifa...
Kesho sasa mwanawane natokea kama Shwaznigaa kudadeki ndandandaa ndaaaa.
Picha linaanza nimeshika katiba ya warioba mkononi. Natangaza: ...Kwa ajili ya kuleta mshikamano na kuponya Taifa lisipasuke namfungulia Lissu, pili; kwakuwa muda ni mfupi uliobaki kwenda katika uchaguzi naipitisha katiba ya warioba iliyopitishwa na wananchi ili tuitumie katika uchaguzi huo, tatu natangaza kutogombea uchaguzi huu napisha nafasi Chama kiteue mtu mwingine.
Nafunga press nasepa. Najua wao Watatoa mlio saaaana, lakini kwa wananchi bonge la shangwe.
Hii inaitwa mwaga ugali nimwage mboga.