Kudai Israeli ni Taifa la Mungu huku Wayahudi wakimkaata Yesu, ni ushahidi hizi dini zimejaa uongo mwingi

Kudai Israeli ni Taifa la Mungu huku Wayahudi wakimkaata Yesu, ni ushahidi hizi dini zimejaa uongo mwingi

. Mimi hayo mambo ya dini nimeyapotezea muda mrefu sana.
Hawa Ndo wametumbukia kwenye shimo reeefu.

Yohana 14:9
“Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba;

Yohana 5:37 SRUV
Naye Baba aliyenituma amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wowote, wala sura yake hamkuiona.
 
Si mwanadamu amesema ,ni Mungu amesema. Wewe uliye udongo tu unamuuliza mfinyanzi? Usiniambie Mungu, kama wanakosea atawaadhibu yeye mwenyewe siyo Wewe.
Hizi dini zimewalemaza vibaya[emoji28]
 
Ukristo ulianzishwa miaka 15 Baada ya Yesu

Wakati wazungu wanaanzisha dini ya ukristo na kuwahubiria watu kuwa Yesu ni Mungu

Wayahudi waliocheza kombolela na Yesu katika mitaa ya Galilaya walikuwa bado wapi

Wayahudi waliokuwa wanapiga mishe na Yesu za kuchonga vitanda na makabati walikuwa bado wapo

Wayahudi waliokuwa wanaishi jirani na Yesu walikuwa bado wapo

Hivyo basi hiyo dini ya uongo iliyoanzishwa na Wazungu wakawachia Wazungu wenyewe waendelee kuwadanganya

Na Yesu alikuwa myahudi wa kabila sio dini
Halafu we mwehu baadae utakuja na vifungu vyako vya aya za kipigaji kutoka kwa wavaa kobazi!!
Ndo nyienyie wazee wa mapokeo mnameza matangopori ya waarab bila kumumunya!!
 
Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.

Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unatahiili kuombewa.

Hata hivyo, cha kushangaza ni sisi sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu huku Wayahudi wakiwa hawamkubali Yesu na wengi wa hao Wayahudi wameukaa kristo. Ajabu sana!

Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .

Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?

Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.

Salary Slip:

Kwa nini usiende kwenye source? Mkuu Salaery Slip. ni aibu kama wewe Mkristo unashindwa kupata majibu yako toka kwenye Biblia, hii sio kwako tu, ni kwa muumini wa dini yoyote ile, nikiwa Mwislamu lazima niitee dini yangu toka kwenye source yake, yaani Quran..

Watu wengi dini wamerithi tu, kwa vile wazazi walikuwa Wakristo basi ndio umekua Mkristo, au kwa sababu Wazazi wangu ni Waiislamu na mimi ni Muislamu.....kwa njia hii watu wengi ni very shallow mno katika Imani zao.

Mkuu Salary Slip, just take your time go to the source, Bible......start with the New Tastement.....itajibu kirahisi majibu yako!
 
Ukatoriki ulifikaje Rome-Italy na kuwa dhehebu la kwenye ukristo.
Anglican wamekuaje waingereza na ni christians.
Lutheran pia nao ni vipi.
Mwamposa, Gwajima, Mzee wa upako nk wanatofauti gani na hao wengine kuanzia Vatican mpaka pale church of London.

Biblia imeanzia pale mashariki ya kati Israeli, na biblia hiyohiyo inasema Israeli ndio Taifa teule.. na sio Tanzania wala Kenya..

Yaani Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi atuumbe wooote na mataifa yetu halafu aibariki Israeli na waIsraeli.
Uyo Mungu wenu atakua kichaa kulibariki taifa la hovyo lililomsaliti, lisilomtambua Kama israeli
 
Dini hizi ni utapeli mtupu!

Zimelifanya bara la Africa kuwa bara la hovyo kuliko yote na watu wake hovyo zaidi.
Tatizo ni wapokeaji wenyewe au aina ya dini au namna dini husika ilivyofikishwa kwa watu.

Historia iko wazi kwamba mahali popote ambapo Ukristu halisi ulipenya, watu walipata maendeleo makubwa na kwa kasi sana.

Wanasayansi, wanasiasa, wasomi, wanasanaa na viongozi mashuhuri asilimia kubwa msingi wa mafanikio yao ni Ukristu.

Ulaya na Marekani ni mifano miwili.
 
Ni kweli usipohoji ni kosa, lakini unahoji huku tayari umeshafikia hatma ya kuwa ni uzushi?? Hapo haujahoji bali umethibitisha

Hivyo haiwi hoja bali ni uthibitisho na ndio maana nikasema kwa mkristo wa kweli alieisoma Biblia ataelewa kuwa Wayahudi walimkataa Yesu kipindi hiko, na ndio maana alisulubiwa

Sawa ili nijiridhishe kwenye nini hasa

Maana hata historia inaonesha wazi Yesu aliishi duniani
Wewe si inaonekana ni evangelical. Wewe haufahamu mahali ulokole ulipoanzia?

Historia inatoonyesha wazi unazungumzia Historia ipi? Hiyo unayosoma shuleni au?

Mimi nashangaa sana unamtaja Yesu, ambaye ni wa agano jipya. Ambaye hataki uonevu wala mauwaji ya mwanadamu yoyote achilia mbali watoto.

Lakini unakuja tena unatetea huo uovu kwa reference maybe ya agano la kale.

Hata ukitizama hoja ya mleta mada, ungetambua contradictions za ajabu kama alivyoleta hoja yake.

Kuingizwa chaka kupo, lakini kusikupatie hasara kama ilivyotokea kwa bara letu la Africa. Hata mleta mada ametoa mfano wa Kibwetere nk.

Shida sana sisi waafrika.
 
wazungu wanaendelea kuja AFRICA na mikataba yao ya KIPUMBAVU coz wanapitia mlemle kwenye akili za mababu zao kwamba bado tumelala!!!
Mikataba ya DP World, Loliondo... ni ya Wazungu?
 
Hata ufisadi unaofanywa na serikali ya CCM ( kwa ushahidi wa ripoti za CAG za kila mwaka) nao umefanywa na wazungu?
Ufisadi si ndo unaotokana na ujinga wa miafrika? Kwani wewe unadhani ni Tanzania tu? Kwanza juzi rais wa Nigeria amepigiwa kelele na wananchi kwa kujiagizia meli ya kifahari all maarufu “yatch” na magari ya kifahari kwa viongozi wote pamoja na mke wake.

The list goes on…
 
kasome kwanza bible usiwe kama andazi.

bible imeandika wazi,Yesu alikataliwa na hao wayahudi,ndio sababu hata ya kuuawa kwake.
Just a simple logic , Yesu amekufa msalabani akafufuka pangoni akapaa kisha atarudi tena Duniani na atakufa tena, this means Yesu atakufa mara mbili sababu iko wazi njia ya kuondoka duniani ni kufa!! Kweli hili ni changa la macho laivu!

Swali 1 : ni binadamu gani tunaemjua amekufa tukamzika futi sita ardhini eti mara akafufuka akapaa na akarudi Duniani na akafa Tena!! Nani tunaemjua amewahi kufa mara mbili? Stori ni kuwa maumivu ya kutoka roho ni sawa na kumchuna ngozi binadamu alie hai!!

Swali 2: Yesu ni Mungu, yaani kama ni kweli Ina maana binadamu aliowaumba (Jews) wakamuua? Mungu tangu lini akawa fundi seremala , Mungu anakula mikate? Kweli kabisa mtu Na akili zako unaamini? Mungu anaenda msalani kweli? Tuache utani turudi kwenye dini zetu za kutambika! Na pia ina maana Mungu Yesu alipokufa msalabani Dunia ilibaki bila Mungu?!! Hii nayo imekaaje?

Swali 3: biblia inasema amelaaniwa aangikwae juu ya mti (kusulubiwa) ina maana Yesu kusulubiwa nae ni mlaaniwa? Yaani Mtume wa Mungu alaaniwe? Kweli kabisa inaingiaje akilini!!

Biblia inaacha maswali mengi bila majibu wajanja kina Mzize wamechomoka!!

Naona hapa kuna mengi ya kujifunza!

Ukweli ni kuwa si Jews Wala wazungu ambao ni wakristo, uzunguni 99% ni wapagani hawamjui Mungu ila wanatuma pesa Africa kulea makanisa! Haya ni maajabu sana ya Dunia! Hata Dem wangu mzungu alikuwa akishangaa wabongo kujaa makanisani!!

Kamusi inatafsiri synagogue kama 'msikiti' wa wayahudi meaning Yesu hakuwa mkristo! Babylon ni Iraq, Korintho ni Ugiriki, Sinai Misri, Babeli Iraq, Nazareth, Jerusalem na Bethlehem ni Palestine, yaani Ina maana Yesu alitembea kwa miguu na wanafunzi wake umbali mrefu akihubiri katika nchi karibu kumi!!na kipindi hicho Cha Yesu Dunia ilijaa ubabe, vita na utumwa Ina maana hawakutekwa? Hili ni changa la macho pia! sijui ukristo ulianzishwa na nani na ni nani alieandika biblia, kwa lengo Gani?

With my view kwa ninavyojua history ya himaya (empires) za dunia ya kale nimeona Yesu aliishi Palestine tu huko kwingine ni Mbali sana na Kuna sehemu lazima uvuke bahari na zilikuwa himaya zingine Yesu asingeweza kukatiza bila kuuwawa au kufanywa mtumwa , hizo stori za sehemu nyingine za Mbali mno ni changa la macho tu!

Vitabu vya historia kama The History of Ancient World vinaandika Jesus was a Palestinian aliepambana kukataa udhalimu wa Wayahudi hasa katika mji wa Jerusalem!

Kwa wasiojua historia , msalaba ni miti miwili inayokinzana na zamani ilikuwa inatumika ulaya hasa nchi ya warumi na wayahudi kusulubisha na kuua mateka wa vita, watumwa na wahalifu , haijulikani ilianza lini na kwa nani msalaba ambao ni mti wa kuulia wahalifu kumaanisha ukristo! Mfano Gaius Julius Caesar Jemedari wa jeshi la warumi aliwasulubu kwenye njia ya kuingia Rome watumwa 6000 walioasi chini ya mtumwa kiongozi Spartacus , yaani misalaba elfu sita iliwekwa na kuwaua kina Spartacus!! Hapo habari ya ukristo haikuwepo ila misalaba ilikuwepo kabla ya Yesu kuzaliwa.

Siku hizi bongo watoto wetu wanaharibiwa na makanisa maana picha za yule jamaa aliyeekti muvi maarufu ya Yesu akiitwa Jonathan Roumie zimemaanisha ndio Yesu mwenyewe kabisa na juzikati alikuja bongo kutembelea vivutio watu wakaalikwa kwenda kumuona Yesu wa Nazareth!!

Wayahudi ndio walijenga Colosseum wakati wa Roman empire, zile stadiums ambazo watumwa gladiators waliuwana kufurahisha warumi! Yaani Taifa teule la Mungu ndo lijenge viwanja vya kuulia watu kama burudani? Kweli kabisa?

Wayahudi milioni 6 waliuwawa na Adolf Hitler huko ujerumani kwenye vyumba vya gesi wakati wa vita ya pili ya dunia.Yaani Mungu awaache Taifa lake wauwawe na mhuni Hitler hivi hivi tu asiwalinde? Kweli?

Wayahudi wengi kama makabila yao ya Banu Qurayza, Banu Nadir na Banu Qaynuqa walijiunga na waasi wa Macca against Mtume Muhammad SAW na kuuwawa na kutokomezwa kabisa hadi leo huko Madina walikoishi enzi za Mtume SAW.

Wayahudi wanaua watoto hospitals za Gaza right now!!

Hapo kwa wayahudi hakuna Mungu na haijulikani nani alianzisha hiyo habari ya kuwa ni Taifa la Mungu , walisoma wapi?

Pole sana waumini, someni my comment without bias mtapata kitu!
 
Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.

Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unatahiili kuombewa.

Hata hivyo, cha kushangaza ni sisi sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu huku Wayahudi wakiwa hawamkubali Yesu na wengi wa hao Wayahudi wameukaa kristo. Ajabu sana!

Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .

Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?

Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.
Kuna vitu vya msingi katika imani ya Kikristo unavikosa. Jibidishe, ili kujijengea ufahamu katika imani yako.

Maswali machache na mafupi ya kawaida:

1) Kwa kadiri ya maandiko, Waisrael waliwahi kuadhibiwa na Mungu kwa kwenda kinyume na maagizo yake, mara ngapi?

2) Mara ngapi baada ya Waisrael kumkosea Mungu, na kisha kuadhibiwa kwa kupigwa na maadui zao, na hatimaye kutiwa utumwani, aliwatumia manabii, na kisha waisrael baada ya kukiri uovu wao na kumrudia Mungu, aliwaokoa kwa mkono wenye nguvu na ushindi mkubwa dhidi ya maadui zao?

3) Kwa kadiri ya maandiko, kutokana na uovu na makosa yao, je, kuna wakati Mungu aliwahi kuwaambia Waisrael kuwa kwa sababu ya kosa hili, kuanzia leo ninyi siyo Taifa teule?

4) Kwa kadiri ya maandiko, hata sisi tusio Waisrael, mara ngapi tumeanguka katika dhambi? Je, kuanguka kwetu katika dhambi, kumetufanya tusiwe wana wa Mungu?

5) Ukisoma biblia vizuri, maneno mengi ya manabii na Masiha Yesu, amezungumza sana juu ya Wayahudi kutompokea Masiha, na hivyo Mungu kuwaadhibu kutokana na kosa hilo. Anazungumzia juu ya mfalme kuwatuma watumishi (manabii), lakini wayahudi kuwakataa; kisha kuamua kuwatumia mtoto wake (Yesu) akitarajia watamheshimu na kumsikiliza, lakini wakaamua kumwua. Na anawauliza, je mfalme atawatenda nini watu wa namna ile? Nao wanajibu kuwa atawaangamiza. Kiimani, hata yale ya kuangamizwa na Hitler au Hamas, yaweza pia kuwa adhabu ya Mungu kwaajili ya kumkataa masiha. Kwa kadiri ya unabii, kuna siku watamkiri Kristo, na utakuwa mwisho wa mateso na maangamizi yao.

Ni sawa na mfalme, awe na wanawe wakorofi. Wakiwa wakorofi anaweza kuwakasirikia. Akiwa amewakasirikia, ninyi wengine mtaonekana ni wazuri kuliko wanawe watukutu. Lakini ninyi wengine, mkafanya jitihada ya kuwabadilisha watoto wale, hata wakarudia katika hekima, mfalme atawashukuru sana hawa waliowasaidia watoto wake hadi wakarudi katika kujitambua. Baada ya watoto wale kurudi katika hekima, ni dhahiri nafasi yao bado itakuwa ya juu kuliko ninyi mliowasaidia hata wakawa watu wema, na si ajabu wale waliowasaidia watoto hawa kurudia katika hekima wakapata thawabu kubwa kwa kazi hiyo njema, kuliko waliowatendea uovu wakati wa kipindi chao cha uovu.
 
Ufisadi si ndo unaotokana na ujinga wa miafrika? Kwani wewe unadhani ni Tanzania tu? Kwanza juzi rais wa Nigeria amepigiwa kelele na wananchi kwa kujiagizia meli ya kifahari all maarufu “yatch” na magari ya kifahari kwa viongozi wote pamoja na mke wake.

The list goes on…
Point yangu ni kuwa matatizo ya Africa yanaletwa na sisi Waafrika wenyewe. Wazungu walitufanyizia na wameshaondoka ila watawala wengi wa kiafrika wamegeuka kuwa wakoloni weusi.
 
Back
Top Bottom