Kuna vitu vya msingi katika imani ya Kikristo unavikosa. Jibidishe, ili kujijengea ufahamu katika imani yako.
Maswali machache na mafupi ya kawaida:
1) Kwa kadiri ya maandiko, Waisrael waliwahi kuadhibiwa na Mungu kwa kwenda kinyume na maagizo yake, mara ngapi?
2) Mara ngapi baada ya Waisrael kumkosea Mungu, na kisha kuadhibiwa kwa kupigwa na maadui zao, na hatimaye kutiwa utumwani, aliwatumia manabii, na kisha waisrael baada ya kukiri uovu wao na kumrudia Mungu, aliwaokoa kwa mkono wenye nguvu na ushindi mkubwa dhidi ya maadui zao?
3) Kwa kadiri ya maandiko, kutokana na uovu na makosa yao, je, kuna wakati Mungu aliwahi kuwaambia Waisrael kuwa kwa sababu ya kosa hili, kuanzia leo ninyi siyo Taifa teule?
4) Kwa kadiri ya maandiko, hata sisi tusio Waisrael, mara ngapi tumeanguka katika dhambi? Je, kuanguka kwetu katika dhambi, kumetufanya tusiwe wana wa Mungu?
5) Ukisoma biblia vizuri, maneno mengi ya manabii na Masiha Yesu, amezungumza sana juu ya Wayahudi kutompokea Masiha, na hivyo Mungu kuwaadhibu kutokana na kosa hilo. Anazungumzia juu ya mfalme kuwatuma watumishi (manabii), lakini wayahudi kuwakataa; kisha kuamua kuwatumia mtoto wake (Yesu) akitarajia watamheshimu na kumsikiliza, lakini wakaamua kumwua. Na anawauliza, je mfalme atawatenda nini watu wa namna ile? Nao wanajibu kuwa atawaangamiza. Kiimani, hata yale ya kuangamizwa na Hitler au Hamas, yaweza pia kuwa adhabu ya Mungu kwaajili ya kumkataa masiha. Kwa kadiri ya unabii, kuna siku watamkiri Kristo, na utakuwa mwisho wa mateso na maangamizi yao.
Ni sawa na mfalme, awe na wanawe wakorofi. Wakiwa wakorofi anaweza kuwakasirikia. Akiwa amewakasirikia, ninyi wengine mtaonekana ni wazuri kuliko wanawe watukutu. Lakini ninyi wengine, mkafanya jitihada ya kuwabadilisha watoto wale, hata wakarudia katika hekima, mfalme atawashukuru sana hawa waliowasaidia watoto wake hadi wakarudi katika kujitambua. Baada ya watoto wale kurudi katika hekima, ni dhahiri nafasi yao bado itakuwa ya juu kuliko ninyi mliowasaidia hata wakawa watu wema, na si ajabu wale waliowasaidia watoto hawa kurudia katika hekima wakapata thawabu kubwa kwa kazi hiyo njema, kuliko waliowatendea uovu wakati wa kipindi chao cha uovu.