Mgogoro wa Palestina si mgogoro wa kidini, ni mgogoro wa nchi moja kuikalia na kuikandamiza nyengine.Dai kwamba Israeli ingali taifa teule la Mungu ni sawa kabisa na lile la Ukatoliki kwamba lenyewe ni Kanisa la Mungu lililokabidhiwa ufunguo wa Mtume Petro wa mamlaka duniani & mbinguni (Mat. 16:18, 19).
Huu ni ughashashi wa kidini, tena uliokubuhu!
Hata hivyo Mwisraeli mmoja mmoja akimkubali Bwana Yesu anaokolewa.
Warumi 11
[13] Lakini nasema na ninyi, mlio watu wa Mataifa. Basi, kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa Mataifa, naitukuza huduma iliyo yangu,
[14] nipate kuwatia wivu walio damu moja na mimi [Wayahudi] na kuwaokoa baadhi yao.
[15] Maana ikiwa kutupwa kwao kumeleta upatanisho kwa ulimwengu, je! Kukubaliwa kwao kutakuwa nini kama si uhai baada ya kufa?
[16] Tena malimbuko yakiwa matakatifu, kadhalika na donge lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo kadhalika.
[17] Lakini iwapo matawi mengine yamekatwa, na wewe mzeituni mwitu ulipandikizwa kati yao, ukawa mshirika wa shina la mzeituni na unono wake,
[18] usijisifu juu ya matawi yale; au ikiwa wajisifu, si wewe ulichukuaye shina, bali ni shina likuchukualo wewe.
[19] Basi utasema, Matawi yale yalikatwa kusudi ili nipandikizwe mimi.
[20] Vema. Yalikatwa kwa kutokuamini kwao, na wewe wasimama kwa imani yako. Usijivune, bali uogope.
[21] Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili [Wayahudi], wala hatakuachia wewe.
[30] Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepata rehema kwa kuasi kwao;
[31] kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema.
[32] Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
Baadhi ya waafrika hawajielewi, Wazungu wamejawa undumilakuwili na wako kimaslahi. ANC walipokuwa wanapambana kwa siasa na silaha kwa sababu ya kukaliwa nchi yao na kukandamizwa, wazungu waliwaita magaidi pia. Leo Urusi anapopiga mabomu na kuua wasio na hatia, wanaikingia kifua ukraine bali Palestina wanapopigwa na kuuliwa watoto na wasio na hatia wanasema "hii ni vita"
Hivi meli za kivita, ndege, vifaru unapambana na Hamas ambao hawana jeshi na ni kikundi tu!