Kabla sijaenda mbali, kwanza nikiri mimi ni Mkristo ila Ukristo wangu sio sababu ya kutohoji hata kama mtasema imani yangu ni ndogo.
Tukirudi kwenye mada, huku kwetu ukimpinga Kristo, hutaeleweka na utachakuliwa kuwa ni mwenye dhambi na unatahiili kuombewa.
Hata hivyo, cha kushangaza ni sisi sisi tunaodai Israel ni Taifa telule la Mungu huku Wayahudi wakiwa hawamkubali Yesu na wengi wa hao Wayahudi wameukaa kristo. Ajabu sana!
Kwa kifupi, jambo hili linaweza kuwa ni ushahidi tosha kuwa katika hizi dini, kuna mambo ya kutunga katika hivi tunavyovitta vitabu vitakatifu na huenda ni maandiko/aya zote ni uongo au baadhi ya maandiko/aya ndio za uongo .
Pia, nawaza,Tulia watanzania wengi hawamkubali, lakini huko nje ya nchi wamemkubali na kumpa cheo kikubwa tu. Je, ndio yale yale ya Wayahudi kumkataa Yesu na sisi huku kumkubali kama Mwana wa Mungu?
Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.
Mkuu ukristo uislam na dini nyingine uijuayo, ni ngonjera ya kulainisha watu ili watawaliwe vizuri.
Imani ya kweli ni inayozingatia misingi ifuataayo:
1. Kuipenda, kuitunza na kuilinda familia yako vizuri.
2. Kuwaheshimu, kuwapenda na kuwaenzi wazazi wako pamoja na wakubwa wenzao.
3. Kutenda wema kwa binadamu wenzako bila kujali jinsia, rika, umri, rangi, tamaduni, imani, mazingira au kipato!
4. Kuzingatia, kuenzi, kusimamia na kulinda misingi, taratibu, miongozo, mila, desturi, kanuni, sheria na tamaduni za jamii yako.
Waisrael sio taifa la Mungu, kwa sababu tulitegemea tuone special treatment ya kutoka kwa Mungu tofauti na jamii zingine.
1. Je wanavuta hewa tofauti na wengine?
2. Je hawaishi kwa chakula kama wengine.
3. Je hawazaliwi, kukua na kuzeeka kama wengi?
4. Je hawafi kama wengine?
5. Je hawajishughulishi kuishi kama wengine.
6. Je hawajitawali kama wengine?
7. Je wanakutana na huyo Mungu wao ana kwa ana, bila kutumia maandishi ya historia?
8. Je huyo Mungu wao anawaondelea changamoto, shida, matatizo yao mubashara tofauti na wengine?
9. Je walivyo kuwa wanauawa kipindi cha Hitler huyo Mungu wao hakuona, ashughulike na Hitler.
10. Je bila msaada wa Marekani na ulaya wanaweza kuzichapa na majirani kwa nguvu ya Mungu wao wakashinda?
11. Huyo Mungu kwa nini asiwanyakue na kuwa peleka kwenye ardhi isiyo na ukame, mawe, vita na majirani Visiwani?
12. Huyo Mungu wao kwanini asiwabadilishe majirani zao wapalestina au kuwa ondoa kabisa?
Mkuu nikijibiwa maswali hayo, bila ngonjera na maneno mengi nitaamini kweli hawa jamaa ni wateule au watu wa Mungu!