Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Hukumu huwa inakuja kwa njia nyingi mno.

  • Wengine walipigwa gharika.​
  • Wengine walipigwa na moto.​
  • Wengine walipigwa na magonjwa ya milipuko.​
  • Wengine walipigwa kwa vita na maangamizi mengine.​

Sasa hivyo haya mambo yatakuwepo, japo naamini hiki kizazi chetu kinaweza kukumbwa na matatizo makubwa mno kwasababu THIS IS A SECOND TIME WE HAVE SUCCESSFULLY BUILT A MULTI-CONTINENTAL CIVILIZATION under a web of Globalization and Capitalism.
Katika sayansi Inasemekana dunia imewahi kuwa na 5 mass level extinctions events kama ile ya asteroid iliyoua dinosaurs miaka millioni 66 iliyopita (cretaceous-paleogene extinction event).
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Sasa unatushaurije sie wapenda ndoa?
 
Hivi nyoka wenye sumu, nzi wa majumbani, mende na mbu wanaoambukiza Malaria nao walipona kwenye gharika?
Hapo sijui mkuu, labda nitafute chanzo nijue kama viumbe vyote havikupona au vilipona
 
Hapa duniani shetani atashinda, ushindi wake unapimwa na wangapi ameweza kuwapotosha, lakini Mbinguni Mungu anamsubiri na huko shetani hana mamlaka yoyote na ataadhibiwa pamoja na wafuasi wake
Katika zama hizi na zama za kale je ni kipindi kipi ambacho shetani aliabudiwa sana na kuwa na wafuasi wengi sana na upinzani mchache?
 
Kipindi hiki shetani ana wafuasi wengi, ukitaka kujua hilo angalia population ya wakati huu na wakati uliopita
 
kusema kweli mimi kama shetani mwenyewe nimeshangaa sana!, binadamu mmekuwa mkinisakama kwa vingi sana,maswala yenu yakiwashinda mmekuwa mkinirushia mimi zinga la nyuki!.
kama ndoa zimewashinda mimi inanihusu nini..?
sio mimi ninaefungisha hizo ndoa hayo ni mambo yenu!,Hivyo basi ninakemea vikali sitaki na sihitaji mnihusishe na mambo yenu haswa ya ndoa!. Pia nitoe rai kwa yeyote atakaenisingizia basi natangaza nitamalizananae ki ubaya ubwela... 👿
 
Umesahau kwamba uliapa utahakikisha unawapoteza wanadamu?
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.

Hayo yaliandikwa katika hicho kitabu au yalitabiriwa katika maandiko kwenye nyakati za mwisho?? 😥
 
Hayo yote yapo katika hicho kitabu, familia ni chapter mojawapo tu, yapo mambo mengine mengi
 
Nilimaanisha hicho kitabu kiliandika sawa. Reference ya Vitabu vya dini zinasemaje?
 
Vitabu vya dini vimetabiri dalili za nyakati za mwisho na mambo ambayo yatatokea nyakati hizo.

Nadhani kitabu cha Ufunuo ndyo kinaeleza hayo mambo
 
Kukanusha na kudanganya ndyo tabia yako Kuu
nakupa onyo!. kama huna fikra pana achana na kunisingizia kwenye mambo yenu!, nyinyi mmedanganywa shetani sihusiki na dhambi zenu!, Je hamuoni kwenye vitabu vyenu mmeandikiwa mtabeba misalaba yenu..? kama mimi nawatendesha mbona sio mzigo wangu!
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Hakuna jipya chini ya jua. Ni jambo jipya kwa unayeishi sasa, ila hofu hiyo ilikuwapo na itakuwapo hata baadae, maisha yanaendelea.
 
Back
Top Bottom