Kudorora kwa muhimili wa familia na wimbi la kukataa ndoa ni ishara ya ushindi kwa shetani

Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Kimyaaa hovyoo
 
ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Andiko nzuri,
usisahau kwenye kuoa, hufungi ndoa na watakatifu.
Kufunga ndoa na mashetani ni kumtukuza bwana shetani pia.
kila mtu akimbie mbio zake,
 
Huo ni utani tu wa mitandaoni, wabongo bado ni watu wanaothamini sana ndoa. Ukitaka kuthibitisha hilo angalia kadi za michango ya harusi unazopokea
Nakubaliana na wewe watu bado wanaoa
 
Andiko nzuri,
usisahau kwenye kuoa, hufungi ndoa na watakatifu.
Kufunga ndoa na mashetani ni kumtukuza bwana shetani pia.
kila mtu akimbie mbio zake,
Kila mtu ajitahidi kujua mbinu za shetani ili kuziepuka
 
Hakuna jipya chini ya jua. Ni jambo jipya kwa unayeishi sasa, ila hofu hiyo ilikuwapo na itakuwapo hata baadae, maisha yanaendelea.
Hofu ilikuwepo lakini kwa sasa imezidi
 
KlKATAA NDOA ishi kwa furaha na amani bila kumkwaza mtu kwasababu makwazo pia ni dhambi, kuuana kisa mmefumaniana ni dhambi, kumtesa mwenzio kwenye ndoa ni dhambi, kuwa mnyonyaji kwenye ndoa ni dhambi
Suluhu ya hayo yote hapo ni KUKATAA NDOA kila mtu awe huru kufanya mambo yake.
 
Ukikataa ndoa ni ishara kwamba wewe ni madhaifu na unaogopa kukutana na changamoto, ndoa ni jambo jema lakini pia kuna mitihani ndani yake
 
Amani ya moyo wangu na utulivu wa akili yangu ni kipaumbele changu namba 1 kwasababu ndivyo huniwezesha kufanya mengine kwa usahihi ikiwemo kumtukuza Mungu.
 
Unamtukuza Mungu kwa kuzini kila siku?
 
Habari za wakati huu wadau na wana familia wote.....

Moja ya nguzo muhimu katika maisha ya mwanadamu ni familia, hata Mungu alipo muumba Adam aliona amekuwa mpweke na akamletea mwenza, pia mwisho akawaamuru waende wakaijaze dunia.

Hivyo basi, njama au lengo kuu la shetani ni kusambaratisha na kuvuruga nguzo ya familia, na njia mojawapo ni kuhakikisha hakuna ndoa wala malezi ya pamoja.

Ifuatayo ni mifano au mambo ambayo yanaashiria ushindi huu ambao shetani anaupata.....

Mfano 1. Kumeibuka wimbi kubwa la vijana kudai na kuhamasisha wengine kupinga na kukataa swala la ndoa, hii ni ishara ya juhudi na ushindi wa shetani katika kuharibu Muhimili wa familia.

Mfano 2. Malezi ya pamoja yamepungua, single mothers wameongezeka na watoto wengi wanapata malezi ya upande mmoja.

Mfano 3. Watoto kutumia muda mwingi mashuleni, asubuhi mpaka jioni mtoto anashinda nje ya nyumbani, malezi ya wazazi atayapata sangapi au mpaka weekend?

Mfano 4. Wimbi la mapenzi ya jinsia moja, kama watu wakishiriki aina hii ya mahusiano basi tayari hapatakuwa na familia tena kwani hakuna uwezekano wa kuzaa watoto.

Mfano 5. Wanawake kutoka nyumbani, Muhimili wa familia unategemea sana uwepo wa mwanamke, kama anatoka kutwa nzima na kuwaacha watoto, hapo tayari familia inakosa uimara wa malezi ya upande wa mama.

Mfano 6. Ongezeko la talaka au ndoa kuvunjika, tunashuhudia namba kubwa ya ndoa ambazo zinavunjika baada ya muda mfupi tu kufungwa, hii ni ishara kwamba Muhimili wa familia upo hatarini kupotea au kusambaratika kabisa.

Haya yote yamo katika kitabu ambacho kiliandikwa mnamo mwaka 1990 kabla mifano tajwa hapo juu kuenea kwa kasi kama ilivyo sasa.

View attachment 3063649

ANGALIZO : Kwa wale wote ambao wanapinga na kukataa kuwa na familia, mnapaswa kujua kwamba mnamsaidia shetani kutimiza lengo lake.
Acha kuwatia watu hofu za kijinga,kwani lazima watu waowe na kuoana? Nyie wahafidhina ndio manafanya vijana wasikuhizi waishi kama popo yani wanastress balaa,waache waishi maiaha yao wewe oa ila usipangie watu namna yakuishi.
 
Wahafidhina ni watu gani Mkuu?
 
Kweli sio sahihi kulazimisha, lakini ni vyema kuwakumbusha kwani tunaishi katika jamii ambayo inategemeana, kama wengi wakikataa ndoa inamaana tutakuwa na jamii ambayo haina maadili na uzinifu utakuwa kwa kasi na itaonekana ni jambo la kawaida
KIpindi watu walikua wanaonana kulikua hakuna uzinifu?hakuna jipya chini ya jua.
 
Wanafanya kazi isiyo na mshahara, wanamsaidia shetani na mwisho wanapata hasara
And they're very serious na kwamba huwaambii kitu.

Mbaya sana ni kwamba viongozi wa kidini wanaunga mkono hali halisi, behind wanaogopa kukimbiwa na waumini kwenye nyumba za ibada.

Wanaogopa kukemea dhambi, wameamua kutembea na mdundo wa dunia, they know ukikomaa na maandiko unabaki mwenyewe kwenye jengo 😅, hatari.
 
Pia shetani hana kazi na watu ambao tayari amewapoteza, ana deal na hao viongozi wa dini kwani wao ndyo wabishi na wana uelewa na imani kubwa, hao ndyo anawawinda kwa nguvu zote
 
Kama ni choice na mtu anachagua kwenda huko ni vipi awe ameshindwa wakati amefuata uchaguzi wake ?
Huo uchaguzi wake ndyo kushindwa kwenyewe, kama wewe huamini katika Mungu huwezi kuelewa hilo ndugu
 
Ndoa ni mpango wa Mungu kwa mwanadamu. aliianzishaYeye mwenyewe pale bustani ya Edeni.
mume ni mfano wa Kristo
mke ni mfano wa kanisa

kanisa ni bi arusi, na Kristo ni Bwana arusi. Biblia imeayaongea haya mambo kwa namna ya ajabu sana.

Waefeso 5 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³¹ Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
³² Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.
 
Back
Top Bottom