Kuelekea 2025: Hawa wafuatao bora niharibu kura yangu kuliko kuwachagua

Kuelekea 2025: Hawa wafuatao bora niharibu kura yangu kuliko kuwachagua

kaligopelelo

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2013
Posts
2,832
Reaction score
4,070
Maoni yangu binafsi kuelekea uchaguzi mkuu 2025. Hapa Nina orodha ya Watanzania wenzetu,wanasiasa ambao Kwa namna moja au nyingine huenda miongoni mwao watakuwepo wenye tamaa ya kutaka kuwania kiti cha urais uchaguzi mkuu utakapofika.

Hii ni sehemu yangu ya kujiwekea kumbukumbu Ili nisije nikasahau wanayotufanyia Watanzania kipindi hiki. Kwani iko wazi kipindi cha kampeni wanasiasa wanakuwa na lugha nzuri mno na ahadi zisizotekelezeka.

Orodha hii itanisaidia mimi na mtanzania yeyote atakayeona kuwa orodha hii Inamsaada kwake pia. Lakini pia naomba orodha iongezeke kadri itakavyoongezeka.

Pia orodha ipate muda wa kutosha wa kukaa hewani mpaka siku ya uchaguzi 2025 panapo majaliwa Kwa mwenye kufika siku hiyo akiwa hai na mzima wa Afya.

1. Tundu lissu - Mkimbizi, muongo muongo, hajui anachokihitaji, mtu mwenye ahadi za kurejea nchini Kila uchao na hazitimii. Huyu yupo tayari kuiingiza nchi kwenye utumwa na ukoloni kwa kujipendekeza kwa Wazungu.

2. Prof Ibrahimu Lipumba --- mbinafsi, anatumika kuuhujumu upinzani.

3. Mwigulu nchemba - Huyu jamaa janja janja akipewa nchi atawahamishia Watanzania wanaompinga Burundi, anaiharibu nchi Kwa kuwafisidi wananchi wanyonge wanaotafuta maisha kwa Tozo zake.

4. Edward lowassa - Huyu ni mwanasiasa Malaya Malaya.

5 Frederick Sumaye - Huyu ni mwanasiasa Malaya Malaya ananunulika kama alivyosema Hayati Julius Kambarage Nyerere akiwazungumzia wanasiasa wa namna hiyo.

6. Hashimu Rungwe - Ana upeo mdogo wa maono, mtazamo finyu na uwezo mdogo wa kufikiri.

7. Dr Bashiru Ally - ❌

8. Humphrey Polepole -❌ kihere here ,elimu haijamsaidia.

9. Prof. Sospeter Muhongo - Liprofesa liongo liongo linatumika vibaya na wanasiasa.

10. Palamagamba Kabudi - Lisomi uchwara mueneza propaganda,anatumika vibaya na wanasiasa elimu yake haijamsaidia.

11. Zitto Kabwe - Msomi uchwara mwenye njaa ya mafanikio binafsi kuliko ya umma. Yupo tayari kuuza utu wake linapokuja suala la masilahi binafsi.

12. January Makamba - Kiongozi mkubwa mwenye utoto mwingi, mbinafsi anafeli kusimamia Wizara ya Nishati kwa kujiona mjuaji na kutaka kushindana na legacy ya mzee Magufuli katika kuiboresha wizara hiyo. Huyu roho mbaya hafai.


Wagombea wengine ongezeeni ninyi,hii inaweza ikawasaidia kujitathimini huenda wakabadili mitazamo waliyonayo.
 
Ccm wangejitambua tusingekua tunateseka hivi watu hawawezi kua mbadala wa maisha yetu kwanini tusitengeneze mifumo imara kupitia katiba? Yaan tukubaliane kiongozi akila rushwa au ufisadi kunyongwa siku ya kazi jumatatu asubuhi mbele ya bunge pale dodoma huku tukio likiwa live tbc..lakin Hawa wa urefu wa kamba hawa hàmna viongozi hapo
 
Hivi inamana hujui kilichompata Tundu Lissu? Je mpaka leo kuna mshukiwa amekamatwa au kushtakiwa? Sasa unataka mtu arudi akufurahishe wewe ikiwa bado usalama wake haupo sawa
Tanzania iko salama achana fikra za kipindi Cha mpito tulichopitia.
 
Pambana mwenyewe Hakuna mtawala yeyeto wa kiafrica anaweza letea watu maendeleo. Naona Kenya safari hii wamejifunza kutouana kwa faida ya walamba asali wameona ni ujinga kuuana kwa sababu ya uchaguzi. Wananchi ndio wapatao shida na sio watawala. Mimi yeyeto tu hata asipowekwa mtu nchi hizi za kiafrica zinajiongoza zenyewe hata bila uchaguzi,
 
Kakamkubwa, pamoja na kuwa na haki ya kuchagua na kuchaguliwa haka kapanyarodi hakana heshima wala adabu, katakuwa kama mwendazake.
 
Back
Top Bottom