Kuelekea Uchaguzi, Mbinu zipi hutumika kuiba kura?

Msimsingizie,

Yeye hakuwahi kutuhumiwa kuiba kura,

Mfumo ulliiba uchaguzi,

Kuhusu kuiba kura, aliyenadi msemo wa BAO la mkono, anatakiwa achangie hapa.
Magufuri aliiba uchaguzi kwa kauli zake,matendo yake,matukio ya 2019 na 2020 siyo mfumo bali mwendakuzimu Magufuri.
 
Niliyoyashuhudia na kuyaona 2020 sitakuja kusahau kamwe.
 
Fact.
 
Hata Kenya, Gambia, Zambia, Malawi, Ghana na Senegal ambako vyama tawala viliondolewa watawala walikuwa na kauli hizi hizi chin ya mifumo hiyo hiyo. Hakuna njia nyingine bora zaid ya kufanya mabadiliko ya nchi zaidi ya uchaguzi.
huko si sw na tz , ccmu ameishika hii nchi na kutudumaza kiakili tofauti na huko kwingine mtu anakula mlo mmoja hlf anamshabikia mwizi wa 41B
 
2020 hawakupora kura zilizopigwa na wapiga kura waliweka za kwao tu za wapiga kura wakazitupa majalalani.

Wewe hukuona wasimamizi walienda na mabegi yamejaa ballots?
 
2020 hawakupora kura zilizopigwa na wapiga kura waliweka za kwao tu za wapiga kura wakazitupa majalalani.

Wewe hukuona wasimamizi walienda na mabegi yamejaa ballots?
Ndiyo maana mimi nimesema katika mfumo ambao watu wanaiba uchaguzi mzima, mfumo wote wa uchaguzi wanauiba, ukijikita kuzuia wizi wa kura tu, unajikita kwenye sehemu ndogo tu ya tatizo, bado kuna sehemu kubwa watakupiga tu.
 
Uchaguzi wa 2020 wizi ulianzia kwenye kanuni za uchaguzi Tume ilizitengeneza zile kanuni kwa lengo la kuharibu uchaguzi na siyo kusimamia uchaguzi.

Tume ilikuwa inawachukulia wagombea wa upinzani kama wahalifu na haikuwa na ilikuwa inawezesha wafanyiwe kila aina ya uhalifu na wapinzani wao pamoja na wasimamizi wa uchaguzi.

Hizi Kanuni ziliandaliwa mahususi kwajili ya kufanikisha uhuni wa 2020 na tume yenyewe.View attachment 1595919061-SUPP GN NO 402 TEXT 5 JUNE 2020 - THE National Elections Regulations 15 May 2020.pdf
 
Ndiyo maana mimi nimesema katika mfumo ambao watu wanaiba uchaguzi mzima, mfumo wote wa uchaguzi wanauiba, ukijikita kuzuia wizi wa kura tu, unajikita kwenye sehemu ndogo tu ya tatizo, bado kuna sehemu kubwa watakupiga tu.
Hakika wizi wa kura pekee ni eneo dogo sana la madhaifu ya mifumo ya uchaguzi nchini na pengine huwa ni rahisi kudeal nalo kuliko mchakato wa uchaguzi wenyewe.

2020 kuna wagombea wa udiwani walienguliwa wakakata rufaa tume ya uchaguzi halafu barua za kurejeshwa kwao wakapewa siku tatu kabla ya uchaguzi.

Kuna wagombea wa ubunge walienguliwa wakakata rufaa kwenye tume halafu wakarejeshwa wiki kadhaa kabla ya uchaguzi mambo kama hayo yanaonesha wazi uchaguzi unakuwa hauna maana.
 
Naam,

Ndiyo maana nasisitiza kuangalia tatizo kimfumo, sio kuishia kwenye udhibiti wa wizi wa kura tu.

Kwa sababu kuna wagombea wameondolewa kwenye ugombea kwa sababu za kipuuzi sana ambazo zimo katika sheria na kanuni za uchaguzi. Kwa mikakati ya kisiasa.

Huwezi kudhibiti hiyo issue kwa kudhibiti wizi wa kura.
 
Vyakula vya Marekani ni bora zaidi kuliko unavyokula,unamkataa mzungu wewe kama nani wakati chanjo na madawa karibu yote unayotumia anatengeneza yeye?stop being stupid
 
CCM kwa wizi wa kura ni out of this world kabisa, jamaa hata aibu hawana, mimi huwa wananimaliza pale wanapotoka wakaanza kusherekea baada ya kujitangaza washindi kwa kuiba kura
Kutoka kushangilia ni Mbinu ya kimedani,

Ni kujaribu kuwaaminisha watu kuwa wao wameshinda kihalali na kuwadhoofisha walioibiwa ushindi wakate tamaa kuinuka kudai HAKI.
 
Kwa sasa hawana mbinu nyingine zaidi ya kupindua matokeo kwa nguvu ya NEC na vyombo vya Ulinzi Usalama.
 
Yote hiyo ilikuwa ni mipango ya Magufuri ili ionekane kuwa ccm inakubalika na Watanzania pamoja na yeye kazi zake kuwa ndiyo msingi wa vyama vya upinzani kushindwa kwenye box la kura.
 
Ukweli ndiyo kinachofanya Magufuri achukiwe ni uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019,Maneno yake ya shombo kwamba mkiweka upinzani sileti maendeleo na uchaguzi mkuu 2020
Yote hiyo ilikuwa ni mipango ya Magufuri ili ionekane kuwa ccm inakubalika na Watanzania pamoja na yeye kazi zake kuwa ndiyo msingi wa vyama vya upinzani kushindwa kwenye box la kura.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…