Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

mwingine alikuja inbox maswali mengi nikawa namjibu kama ilivyopaswa.
kaomba na picha za kutosha nikamtumia ile bidhaa ilikuwa juu ya meza. mwisho wa siku ananiuliza "hiyo meza vipi huuzi?"πŸ™ŒπŸ™ŒπŸ˜‚

Yaani tutoke kwenye kujadili bidhaa husika tuanze kujadili meza tena.
 
Biashara ya nguo naona itanipasua kichwa aisee. Ukiweka za aina hii watu wazima wanasema hizo ni za vijana. Ukileta za vijana watu wazima wanakuambia sivai Modo[emoji28]
Ngoja nihamie kwenye simu tu au niuze vyote kwa pamoja. Advice??

Biashara ya nguo ni ngumuu hata physically

Yaani watu wana machaguo unaweza ukachanganyikiwa atleast wanaume kidogo

Ila za kike[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Mkuu wanafikiri sisi wanunuzi hatujielewi.
Ukiuliza ugomvi unakuja ,japo sio wote kuna watu wako vyema sana kwa taarifa.
 
Mbona hata physical ni hivyo hivyo tu, siye wauza genge anakuja bidada anaminyaminya nyanya halafu ananunua biringanya.
Sisi wauza urembo unakuta mdada anataka wanja anachagua mmoja anautest halafu anarudisha anachukua mpya ambao haujaguswa ndio ananunua ule aliotest anakuachia .Hii tabia wanafanya hata kwa bidhaa nyingine pia .
 
Nje ya mada mkuu. Scenario ya mtoa inahusu kuweka maelezo kamili.
 
Kuna mbwa mmoja anauza vipodozi kawe kuna siku mamilow kanituma nimfuatie. Yule mshenzi nimepanda gari hadi kawe kanisani. Ofisi yake iko karibu na lile eneo. Kunielekeza akawa anaona usumbufu akaanza ukali nikamchenjia maana alizidi.

Kuelekeza hajui halafu akawa analazimisha niingie nyumba ambayo sijui kama ndio yenyewe namwambia toka nje ya geti anakaza nikamwambia kama hilo hawezi mi niondoke zangu tusibishane sana. Akamtuma mtoto akasimama nje ya geti na kuniita.

Sikutaka hata kuonana nae wala kuingia ndani niliamuru nipewe bidhaa husika niondoke haraka iwezekanavyo. Basi mineno ikawa inamtoka huyo mama huko ndani, Oh hii ofisi yangu ina utaratibu sio mtu unakuja kunipangia, watu wote wanaingia ndani wanaelekezwa sijui blah blah. Nikamjibu wenye ofisi wako Bagamoyo Road sio uswahilini kawe tena kwenye makazi ya watu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ akasonya nikachukua zaga nikasepa.

Tangu siku hio nimemwambia bibie biashara ya kuniagiza nikuchukulie vitu vyako vya order kama hawakuletei sintofanya upuuzi huo.
 
Nilichogundua biashara ya online. Watu hawasomi yale maelezo unayoandika. Kama umeweka link ya whatsaapp ye anaingia tu na kuanza kukuuliza habari ambazo uliandika kwenye tangazo. Unatakiwa kulijua hilo japo linakera. Unaweza kuweka Lists yote ya bidhaa ulizonazo lakini mtu akauliza kingine kabisa, pengine amekitafuta sana hivyo anajaribu tu kwa matumaini. Hilo nalo ulijue na usamehe.

Pia tambua kuweka maelezo mengi siyo kwamba ndiyo utaepuka wingi wa maswali. Ni bora ukaweka machache yanayoenda kwenye points, ambayo mtu hataona uvivu kusoma.

mwisho, hiyo ni biashara, haulose kitu ukimhudumia bila makasiriko. Zaidi zaidi anaweza kukuletea wateja zaidi
 
 
itakuwa kweli hawasomi ni mtu anatazama tu picha then huyo direct anakuja inbox
 
Sasa unanunua Rolex kwa tsh. 170,000 unategemea Nini mkuu?
 
Kwa hiyo mkuu tuhitimishe kwamba hata mleta mada ni mgaigai na kirusi hamuachi mtu salama?
 
Customer reviews hua hauangalii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…