Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Ukiwa mfanyabiashara kitu cha kwanza kabla ya vyote unatakiwa ujue mteja ni MFALME na MFALME anaweza akauliza au akataka kujua chochote kutoka kwako

Ungekua umesoma Customer care na Entrepreneur nadhani hio situation isingekupa shida maana ungejua una-deal na wateja wa aina ipi
 
Anaulizia maswali ya wateja ya kupuuzi, hivi mfano umeweka bei sawa bado kila anaye coment anataka umtajie bei na aljsha ona coment zingine umetaja bei, unafanyaje? Sikiliza wanunuaji huwa hawa coment pale ananyanyua simu anakupigia,

Huwa wanunuaji hawa coment hata siku 1, wale wanao.sumbua kwa coment sio wanunuaji wale
 
Wauzaji pia sio waaminifu.. ndo maana wateja tunakua na maswali mengi ili kujiridhisha na huduma mkuu..
Imagine kuna mzgo nmeagiza kutoka dar tangu J3 ya wiki iliyopita, ila cha ajabu mpaka leo muuzaji hajautuma.

Uaminifu wenu ni ZERO
Na hili ndio kubwa, wabongo na waafrika kwa ujumla uaminifu ni zero kabisaa, nishapoteza laki 4 kununua simu mtandaoni ambayo sikuipata
 
Ni mbuzi kabisa, wamejaa huko instagram
Yaani wanakera, ukiangalia biashara yenyewe anayoringia sasaa, 🤣🤣🤣
 
Ngoja tuendelee kumpopoa mawe mkuu, maana wachuuzi wa namna hii wanazingua
Yaani anafanya biashara halafu anataka awe anatoa amri badala ya kujibu maswali ya wateja wake, watu wengine ni useless kabisa
 
Mwingine anaweka tangazo, Bei haweki.
Anaaandika TU "serious buyer, check my pm"

Unabaki kujiuliza,
huyu mtu anaakili kweli?

Hivi Ni wangapi wataingia pm kwake?
Hajui kua wengine hushawishika kununua Kwasababu Bei iko chini?
Mafala Hao mkuu, wapo kibao instagram
 
yaani kweli nimexprience sana hii wanunuaji hawanaga mbambamba nyingi.

mfano leo nimeweka bidhaa dada wa Tanga kainua tu simi kanipigia, then tumejadili delivery inakuaje. Mwisho nimemplekea bidhaa ndugu yake pesa nimepewa.
lakini nikionyesha hapa inbox kuna watu wana maswali kibao ambayo tayari kwenye tangazo majibu yapo mwisho wa siku hakuna wanunuaji.
watanzania nimewavulia kofia🙌😂😂😂
 
Ngoja tuendelee kumpopoa mawe mkuu, maana wachuuzi wa namna hii wanazingua
Yaani anafanya biashara halafu anataka awe anatoa amri badala ya kujibu maswali ya wateja wake, watu wengine ni useless kabisa
Hakuna anayekataa maswali mkuu maswali uanayajibu vzr tu.

ila how mtu unakuja kuuliza swali ambalo kwenye item description lishajibiwa tena kwa mpangilio unaosomeka vyema.

Unakuja unauliza maswali ya kiwaki tena. Serious?? Yaani kwa mtu serious unasoma maelezo tu pale kwenye tangazo.
me nategemea kama kuna miss information ndizo hizo mtu aje inbox anihoji. Sio unamsumbua mtu kwa maswali ambayo tayari maelezo yake yametolewa.
 
Kuna watoa huduma Wana nyodo balaa sio tu online business kila idara MBADILIKE
Mimi nimejiwekea kanuni, nikija dukani kwako usiponisikiliza siwezi kununua kwako, haiwezekani nitafute hela kwa Shida halafu kuitumia Tena iwe kwa Shida, mbona ukiingia Bar wale wahudumu wanakuuliza unachohitaji, Hawa wachuuzi wengine nyodo tu zimewajaa ilihali nao ni masikini
 
Mkuu ww jibu tu maswali, hiyo si ndio kazi yako inayokupatia ugali
Hakuna hela nyepesi, Kila kazi Ina ugumu wake
Ushajiuliza ugumu wanaoupata walimu, ungekua wewe si Ungeacha kazi kabisa
 
Mkuu wabongo kwenye online sio kabisa, na bado saaa kwenye Delivery hapo ndio balaaa, anakumbia mfano niletee kuku walio.chinjwa watatu dakika za mwisho ndio unampelekea anakumbia nimepata shida hapa nitachukua mmoja tu au wawili. Acha kabisa
Eeeboo...., kuna watu wanatia hasira sasa hao kuku wengine wameshanyonyolewa anatarajia upeleke wapi?
 

Kuna wengine wanafungua akaunti za biashara zao na wanajiweka status ya "private"...

Sasa unajiuliza huyu mpuuzi ana utofauti gani na mwendawazimu ambaye kajenga duka ndani ya fensi, na ili uweze kununua kitu lazima kwanza ugonge geti...
 
Mimi nimeacha kabisa kununua nguo, viatu na handbags online. Ptuuu Wabongo ni waongo rangi imewekwa filter, size za uongo, hata hand bag kwanini mtu asiweke hata rula kama kipimo. Unaagiza handbag kubwa kinakuja kidunchu cha kuchezea watoto.

[emoji23][emoji23]hii iliwahi nikuta mimi na rafiki tulijuta from there sitamani kuagiza vitu mtandaoni, mama yake rafiki yangu alituambia hizo handbag or vichupi.
 
Mie huwa nafanya direct selling ama door to door kuna ambao nafunga nao biashara mapema ila kuna ambaye lazma upoteze zaidi ya dakika 20!

Na still anaweza chomoa ila treatment yangu huwa sawa kwa siku nahudumia more than 25 Outlets. Ukiwa charismatic unauza zaidi japo sio kila mtu atanunua maana kuna ambao hela hawana.
 
Yah mkuu ndio maan biashara za Bar znafanikiw sana kuliko hata awa wengine,biashara pekee haitoshi bila kuwekeza ukarimu kwa wateja
 
Tena nakuona wew una kijitabia ,wateja watakukataa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…