PreGE2025 Kufika Agosti 1, 2025 CHADEMA itakuwa imefutwa kwenye daftari la Msajili wa vyama vya siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mama Samia tarehe imepita, msajili wa vyama vya siasa hajafuata maelezo yako, mtumbue.
 
Kwahiyo msajili kada wa CCM akiifuta CHADEMA ndio ulingo wa kisiasa utakaa sawa na joto la kisiasa litashuka hatimaye wingi wa watangnyika waliolikataa genge lilojipachika madarakani kwa mitutu ya bunduki litajipatia kibali cha kukubalika??
 
Kinafutwa lini?...au mchakato unaendelea?
 
Vipi hiyo tarehe haijafika!!??
Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu.
 
ANC iliundwa 1912 , lakini haikuwahi kuwa na jengo , wala mahali maalum pa kukutania hapo SA , walikua wanafanya harakati zao kwa siri kuwakwepa makaburu huku kilichowaunganisha ni "ITIKADI" ofisi wamekuja kuwa nazo miaka ya 1990+

Leo hii chama ni platform tu ambayo huunganisha watu wenye itikadi sawa.

Leo hii huko wajinga wamekaaa wakaona waifute CHADEMA wakiamini ndio itakua suluhu na nchi kupoa ila ninawapa pole in advance kufuta itikadi ni suala gumu sana.

Ukitaka kujua hilo huhitaji shahada ya chuo kikuu maana CHADEMA tangu June mwaka jana tarehe 10 walifungiwa kufanya mikutano ya kisiasa wala kutumia mali za chama kama majengo, magari n.k ila joto la itikadi bado liko pale pale .

Huwezi kuhadaa watu miaka 65 ya uhuru kwa ahadi za kuwapa maji, lami na majengo ya hospitali huku unateka , unaua, unalawiti , unaficha pesa account za nje, unatoa ajira kwa misingi ya kujuana .

Itikadi imeshawafikia wananchi kwa wingi na ukijumlisha na kuzidi kupungua kwa rika la watu 1950 , 1960 na 1970 ambalo kwa muda mrefu liliishi kwa hadaa na kuaminishwa bila CCM hakuna kitakachoendelea Tanzania basi ni suala la muda CCM kabla ya CCM kuelekea kwenye anguko lake .

Mimi naona mmechelewa sana kujua futeni CHADEMA halafu muone kama patapoa au ndio mtazalisha itikadi mpya zaidi.
 
Kwa hiyo mkifutwa itakuwa chama cha kigaidi? Maana ukiwa na itikadi wakati hutambuliki na Msajili na wewe unasema chama kipo huo ni ugaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…