Kufuatia upungufu wa dola, BoT yatoa maelekezo ya kudhibiti Viwango Vya Miamala

Dkt. Abdallah Tego abainisha hatua gani za maamuzi magumu ya kisiasa ndiyo yatarekebisha hali hii ya Tanzania kukumbwa na upungufu wa dola

Your browser is not able to display this video.

Kufuatia kuadimika kwa Dola ya Marekani tumemtafuta mtaalamu wa masuala ya kifedha Dkt. Abdallah Y. Tego kutuchambulia masuala yenyewe ni haya yafuatayo:

Fiscal revenue measures
Clearance of external arrears
Governance reform
Banking sector restructuring plan
Curbing Government expenditure

Bio:
Dr. Abdallah Yahya Tego is a holder of BA (Ed) (Hons) from University of Uganda, MA in Islamic Studies from Muslim College London and PhD in Economics (Islamic Microfinance) from Omdurman Islamic University Khartoum Sudan.

Sheikh Tego has more than 15 years working experience in the Islamic Finance profession, he has served various Shariah Advisory Boards for several banks including KCBT Sahl Banking Shariah Advisory Board as a member.


Currently he is a lecturer at Muslim University of Morogoro.
Sheikh Tego has more than 15 years working experience in the Islamic Finance profession, he has served different Shari’ah Boards for the banks including AMANA Bank, NBC and now serving KCBT Sahl
Banking Shari’ah Advisory Board as a member.
 
Naomba namna kupata GB za bure.Kwa tigo au airtel na voda.
 
Nondo za maana umeshusha kwa uelewa wangu wa ABC za uchumi.

Lakini hizi rate kuna kipindi cha awamu ya tano zilikuwa zinashushwa gradually? Nini kilipelekea kusimamisha ushushaji wa riba kwa mikopo?

Kudos mkuu.
 
Mh. Dr. Saada Mkuya Salum waziri wa fedha Zanzibar agusia sababu ya upungufu wa dola

siku za karibuni pesa ya Marekani (Dola) imeendelea kuadimika kwenye maeneo mbalimbali duniani hali inayosababisha changamoto kwa matumizi yanayohitajia pesa hiyo ikiwemo ununuaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Bio:
Dr. Sanda Mkuya Salum holds a Masters of Business Administration from Heriot-Watt University in Edinburgh, Scotland, and a PhD in Business Administration from the Open University of Tanzania (OUT).
 
Nondo za maana umeshusha kwa uelewa wangu wa ABC za uchumi.

Lakini hizi rate kuna kipindi cha awamu ya tano zilikuwa zinashushwa gradually? Nini kilipelekea kusimamisha ushushaji wa riba kwa mikopo?

Kudos mkuu.
My post ilikuwa inaongelea hatua za US central bank katika kupambana na inflation huko kwao na kuonyesha hakuna uhusiano wa karibu na Tanzania kuleta madhara.

Swali lako ni tofauti kidogo na hiyo hoja ya juu; kwa nilivyoelewa unauliza nini kinachangia kupanda au kushuka kwa interest rates za commercial banks, Tanzania.

Hilo swali ni refu kidogo kulielezea ntajaribu kulifupisha hope utapata picha. Kawaida kuna mambo makuu matatu yanayochangia banks kwenye kuamua interest rate ya kukopeshea.

Mainly inajumuisha rate ya wao waliyokopea kwenye hiyo hela wanayokupa, jumlisha rate ya inflation na mwisho rate ya faida. Hiyo ni kwa kifupi kuna rate pia inaweza ongezwa depending na default risk factors za mkopaji.

Matokeo yake ukijumlisha zote hizo unakuta interest rate zipo kwenye double digits Tanzania; sometimes higher than necessary with pressure banks wanaweza shusha. Personal sifuatilii sana riba za banks Tanzania so siwezi testify tofauti ya administration yoyote.
 
Magufuri alifunga hizi Bureau de change za mtaani zisizo na leseni au uhalali wa kufanya mabadilishano ya fedha, mkamuona ana roho mbaya, haya leo mnaona balaa lake.
 
Samahani naomba nikusahihishe mkuu, unatakiwa useme, "Our economy is headed for a cliff.
 
Kuna watu wanadhani urais ni ufalme badala ya kujua kuwa nafasi hiyo ni ya utumishi kwa nchi. Ikulu ni mahali patakatifu!

Mtanikumbuka.
 
Aliyemtangulia mkapa wakati wake ndio Structure Adjustment Programs zilifanyika na officially tukaingia katika mfumo wa kiuchumi wa kibepari ingawa ukiuliza hawa wapuuzi wanasema sisi ni taifa la kijamaa, ujamaa my foot.

Kutokea pale pesa nyingi sana ziliingia na kuingizwa kwenye mashirika ya bima, bandari, kilimo, mabenki etc. Kwakifupi ilikuwa neema sana pesa ilikuwa ni nyingi sana na huyu magufuri tuliyekutana nae 2015 - 2020 tungempata wakati ule basi hili taifa lingesonga mbele sana ila kwa bahati mbaya mzee Ruksa walimuonea kama wanavyomuonea huyu mama kwa kuzipiga zile pesa especially shirika la bima.

Walipiga sana na kuyafilisi mashirika ya uma huku wakiacha madeni lukuki. Mafisadi hawakuanza leo. Huyu mama na aliyefuata baada ya mkapa wote ni changamoto katika kudeal na waharibifu wa uchumi maana unatakiwa kuwa mtata kweli kweli.
 
Miezi michache tu baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu kusema kwa ujasiri kwamba nchi iko katika hali nzuri kiuchumi, sasa inaanza kuonekana kama alizungumza mapema sana na anaweza kulazimika kumeza maneno yake.

Suluhu, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Siku ya Wanawake Duniani mapema Machi mwaka huu, alisema Tanzania imeimarika kiuchumi kuliko Nchi nyingine zote za Afrika Mashariki.

 
Kwa sasa ni chini ya 4.9
 
Ufisadi unasababisha majizi kusaka dola ili yakafiche kwenye akaunti za nje ili yanapopeleka wake zao kujifungulia marekani basi yawe na dola za kutosha kwenye akaunti zao.
 
Watu wanafikiria tu kuagiza ma viieite ya viongozi na kuanzisha miradi ya kimchongo ya kilimo sijui na umeme jua.....hovyo kabisa.
 
Haya huwa yanatokea endapo kiongozi akishindwa, akianza vizuri huwa mnapiga vigelegele.

Kama Magufuli alifanya hivyo kwa kurekebisha yaliyoharibiwa na waliopita basi hatukupaswa kumpa sifa pale ambapo mambo yalienda vizuri, tungewapa waliopita.

Hata sasa mambo yakienda vizuri ni ya sasa, yakihribika ni waliopita. Mnafanya watu kama mazuzu.
 
Banking sector restructuring plan
Curbing Government expenditure

MIKOPO MINGI YA KIBIASHARA DUNIANI IMEKUWA YA GHARAMA KUBWA, SASA TUNAGEUKIA MIKOPO YA NDANI​

mikopo mingi ya kibiashara Duniani imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa

29 May, 2023

Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, akifungua mkutano wa Wataalamu 30 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, unaofanyika jijini Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El- Maamry Mwamba, amesema kuwa nchi za Kusini mwa Afrika zinaangalia namna ya kuendeleza soko la ndani la mitaji kwa kutumia Hati fungani ili kuziwezesha kupata mikopo ya ndani wakati ambao mikopo mingi ya kibiashara Duniani imekuwa ikipatikana kwa gharama kubwa.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha kwa niaba yake na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Japhet Justine, wakati wa Mkutano wa Wataalamu wa masuala ya uchumi na fedha wanaosimamia madeni ya nchi zao kutoka nchi 16 za kusini mwa Afrika.

Bw. Japhet Justine amesema kuwa nchi za kusini mwa Afrika zinaangalia namna ya kutumia Soko au Hati fungani za ndani ambazo ni za muda mfupi, wa kati na mrefu zinatoa nafuu kubwa kwa nchi za Afrika, kwa kuwa mikopo ya aina hiyo ni nafuu na haihitaji matumizi ya dola wala uwekezaji wa nje na haina shinikizo wakati huu ambao soko la Dunia halifanyi vizuri.

“Duniani mikopo ya kibiashara inapatikana kwa gharama kubwa, hivyo mikopo ya ndani itakuwa sehemu ya hatua muhimu ya kuzisaidia nchi za Afrika kufanikisha ufadhili wa bajeti kwa ajili ya maendeleo yao”, alisema Bw. Justine.

Bw. Justine alieleza kuwa kuliendeleza Soko la ndani la Hati Fungani kunatoa fursa kwa nchi za Afrika kufanya vizuri zaidi, ambapo Tanzania kwa sasa inapata mikopo ya zaidi ya trilioni saba kutoka soko la ndani ambayo husaidia kufanikisha bajeti Kuu ya Serikali.

Aliongeza kuwa zipo nchi ambazo zinafanya vizuri katika bajeti zao kwa kutumia fursa ya soko hilo ikiwemo Namibia ambayo zaidi ya asilimia 80 ya Bajeti yake inatokana na mikopo ya ndani kupitia hati fungani zake.

Alisema Mkutano huo utajadili na kuchambua aina ya hati fungani za ndani zinazotolewa huwa na manufaa katika kukuza uchumi wakati ambao mikopo inapopungua kutoka kwa wakopeshaji wa kimataifa na pia wakati huu ambao Soko la hati fungani la Ulaya limepungua kwa kiasi kikubwa.

Aidha amewataka wajumbe wa Mkutano huo kuhakikisha wanakuwa na majadiliano yenye tija na kubadilishana uzoefu ili kuzisaidia Serikali za nchi zao katika kufikia maendeleo endelevu.

Bw. Justine amezipongeza nchi zote zilizoleta wawakilishi wao na pia amewataka wajumbe wa mkutano kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.

Mkutano huo umezishirikisha nchi za kusini mwa Afrika ikiwemo wenyeji Tanzania, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Afrika Kusini, Uganda, Kenya, Sudani Kusini na Ethiopia.
Mwisho
Source : NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA ZAGEUKIA MIKOPO YA NDANI | MoF - Ministry of Finance and Planning
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…