Watanzania tumekaririshwa sana mambo yaliotokea 2015, ila hii ya safari hii tutaona mapya mengi zaidi, maana katika kitu CCM wamefeli basi haya maamuzi yao ya kumtoa Membe uwanachama.
Kwanza, asilimia 90% ya wana CCM hawamkubali mwenye kiti wao, ila wanaishi kinafiki tu. Badala ya kutibu tatizo waliokua nalo wameenda kuongeza tatizo.
Kwa kilichitokea kwa Membe ni "SMS" kwa yoyote yule atakaetaka kuchukua form ya kugombea urais na kushindana na Magu. Kifupi, CCM imekua chama cha mtu mmoja tu (Kampuni Ya Mtu Binafsi), hakuna mwenye sauti ya kuongea anachoona na anachoamini.
Ikumbukwe mwanzo kabisa CCM walikua wanashangilia upinzani na raia walivyokuwa wanasulubiwa na watawala, wakaambiwa wakishaisha kushughulikia wapinzani na raia kusulubu kutahamia ndani ya chama. Sasa yamewafika.
CCM wamejiingiza kwenye wakati mgumu sana toka chama kianzishwe. Na mwisho wao umefika kisiasa.