Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

Uchaguzi 2020 Kufungiwa Lissu kwa siku 7 ni ‘advantage’ kubwa sana kwake

Mhubiri chuki amefungwa breki aende akashtaki kwa Robert [emoji16][emoji16][emoji16]
Kusema watu wameuwawa ni kuhubiri chuki?
Kusema watu wanaporwa KOROSHO zao hko kusini ni kuhubir chuki.
Kusema watumishi wa umma hawajaongezewa mishahara kwa miaka 5 kinyume cha sheria ni kuhubiri chuki?
Kusema watu wamenyimwa uhuru wa kuongea ni kuhubir chuki?
Kasome wewe hujui maana ya chuki. Umesahau kwamba kuna mpuuzi mmoja anaongea kilugha chake akiwa jukwaani.zile ndo chuki sasa
 
Sijui nielimishe
Sasa kama hujui Kwa nini umeuliza utopolo wako hapa???? Jinga kabisa wewe!!

Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali na kuishauri serikali

Kazi ya mbunge ni kutunga sheria

Kazi ya mbunge ni kuwasilisha hoja za wananchi wako kwa serikali!!
 
Kuleta MAENDELEO kwenye jimbo sio kazi ya mbunge?
Sasa kama hujui Kwa nini umeuliza utopolo wako hapa???? Jinga kabisa wewe!!

Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali na kuishauri serikali

Kazi ya mbunge ni kutunga sheria

Kazi ya mbunge ni kuwasilisha hoja za wananchi wako kwa serikali!!
 
Kabla hajakuja kuomba kura za urais atuambie kwanza alifanya MAENDELEO gani alipokuwa mbunge.
Unajua zinatengwa shs ngapi kwa mwaka wa fedha??? Kwa kila jimbo???

Utajenga mradi wa maji kwa Mil 60??? Utajenga barabara kwa Mil 60??? Utajenga shule kwa Mil 60???
 
Tunamuongelea mwanasheria apa yeye kama anaweza kuvimba basi aendelee kuvimba tuone
Mnataka aendelee na kampeni ili mseme amefanya kosa mumuondoe kweny uchaguzi?,/hata kama kafyata mkia poa siku 7 si nyingi subiri spana zingine
 
FANYA KAZI KWA BIDII SIO MAGUFULI WALA LISU ATAKAYE KULETEA MAENDELEO.
hakuna sehemu yenye Vita wanapoishi kwa kula raha
Kiongozi wa nchi humletea mwananchi maendeleo, bali hujui. Huwezi kuwa na uchumi binafsi ulioshamiri kama uchumi wa taifa uko legelege. Sera za uchumi hutungwa na kusimamiwa na dola na kiongozi ni rais. Utaendelezaje uchumi binafsi kama sera zinazotungwa ni za kusimamia maslahi ya wachache na wengine ni kukamuliwa kodi hata ukiuza mchicha? Utajengaje uchumi wako wakati wengi waliokuzunguka wamekata tamaa? Kifupi kasome nadharia ya uchumi.
 
Pamoja na kuwa atakuwa hayuko majukwaani lkn mazingira ya jinsi NEC ilivyomzuia yanatosha kumpigia kampeni, sasa wananchi na jumuia za kimataifa zimejua kweli Tume haiko huru na inapendelea, vyombo vya habari vya ndani na nje vinaripoti habari yake.

Muda huu apumzishe ubongo na akili na mikiki mikiki ya barabarani, afanye tathimini ya kampeni aliyoifanya, muda huu anaweza kuutumia kwa press conferences, kupitia daftari la mpiga kura, kuandaa mawakala, jinsi ya kuzuia wizi, kuandaa polling center, kutafuta pesa za kampeni, kufuatilia rufaa za wagombea, n.k.

Wapinzani walizuiwa kufanya siasa kwa miaka mitano lakini baada ya kuruhusiwa tumeona walivyobadili upepo kwa muda mfupi, nini siku 7. Magufuli amejaza mabango kila kona ya nchi lkn faida yake haina tofauti na yule ambaye hana picha hata moja. Kwa hiyo kama wananchi hawakutaki hata ufanye kampeni peke yako hawatakuchagua.

Lissu afahamu tunatafuta Rais atakaye simamia misingi ya sheria kwa wanaoonewa na wasioonewa, hata kama ameonewa tayari wananchi wameshaona, ajishushe kwa moja ili apate mbili.

Mwisho, Mungu naye ana makusudi yake, hatuwezi kujua ndani ya hizi siku 7 kungetokea nini kibaya walichopanga juu yake.
Hii ngoma ni ngumu kwa Lissu, kuna vizingiti vingi sana vyama vya upinzan wamewekewa, hapa nipo Kigogo mwenyeviti wa mitaa wanapita kuchukua vitambulisho vya kupigia kura na namba za simu, Uswahilin uelewa mdogo hata kuhoji ni vinaenda kufanyiwa nn hamna!
 
Naunga mkono hoja iliyotolewa, TAL kwa kipindi hiki cha mapumziko ajikite zaidi kuandaa clips mbalimali kwenye mitandao ya kijamii akizifafanua sera za chama chake na kujiombea kura kwake yeye , wabunge wake na madiwanu

Ajikite zaid kwenye mambo yanayo wasibu wananchi wakawaida, wakulima na wafanya kazi , wakulimwa kudhulumiwa kwa tozo mbali mbali na kukosa uhuru wa kuuza mazao yao kwa bei wanayotaka

Wafanya kazi wa sekta binafsi na serikalini kudhulumiwa na mafao yao baada ya kupitishwa sheria ya kikokotoo, kutoongezwa mshahara kwa miaka mitano

Wanafunzi kukaa chini , wanavijiji hawana maji , shule hazina matundu ya vyo ambayo ni salama kwa watoto wetu

Ukosefu wa ajira kunakotokana na unynysaji wa wawekezaji

Makato ya asilimia 15 kwa mikopo ya elimu ya juu

Na mambo mengi yanayo fanana na hayo

Kwa sasa asiizungumzie kabisa Jiwe na mambo yake wala kile chama cha mboga mboja

Aje na mikakati kama yeye LISU na chama chake , mambo ya jiwe hatuyataki manake tayari mpaka vjijini wanafamu hilo
 
Pamoja na kuwa atakuwa hayuko majukwaani lkn mazingira ya jinsi NEC ilivyomzuia yanatosha kumpigia kampeni, sasa wananchi na jumuia za kimataifa zimejua kweli Tume haiko huru na inapendelea, vyombo vya habari vya ndani na nje vinaripoti habari yake.

Muda huu apumzishe ubongo na akili na mikiki mikiki ya barabarani, afanye tathimini ya kampeni aliyoifanya, muda huu anaweza kuutumia kwa press conferences, kupitia daftari la mpiga kura, kuandaa mawakala, jinsi ya kuzuia wizi, kuandaa polling center, kutafuta pesa za kampeni, kufuatilia rufaa za wagombea, n.k.

Wapinzani walizuiwa kufanya siasa kwa miaka mitano lakini baada ya kuruhusiwa tumeona walivyobadili upepo kwa muda mfupi, nini siku 7. Magufuli amejaza mabango kila kona ya nchi lkn faida yake haina tofauti na yule ambaye hana picha hata moja. Kwa hiyo kama wananchi hawakutaki hata ufanye kampeni peke yako hawatakuchagua.

Lissu afahamu tunatafuta Rais atakaye simamia misingi ya sheria kwa wanaoonewa na wasioonewa, hata kama ameonewa tayari wananchi wameshaona, ajishushe kwa moja ili apate mbili.

Mwisho, Mungu naye ana makusudi yake, hatuwezi kujua ndani ya hizi siku 7 kungetokea nini kibaya walichopanga juu yake.
Good, CC :Lissu
 
Hii ngoma ni ngumu kwa Lissu, kuna vizingiti vingi sana vyama vya upinzan wamewekewa, hapa nipo Kigogo mwenyeviti wa mitaa wanapita kuchukua vitambulisho vya kupigia kura na namba za simu, Uswahilin uelewa mdogo hata kuhoji ni vinaenda kufanyiwa nn hamna!
Acha wafanye ila kuna siku hata nyani hushindwa kupanda miti.
 
Back
Top Bottom