Kuhusu dhuluma dhidi ya Tundu Lissu ni wakati muafaka sasa uchunguzi huru ufanyike

sem2708

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,414
Reaction score
4,534
Dear JF members , ni wakati sasa mh Rais aamuru uchunguzi huru ufanyike dhidi ya waliotaka kumuua Tundu Lissu. Kwa kufanya hivyo serikali hii itajitanabaisha kuwa ni ya kutenda haki ... nawasilisha
 
Dear JF members , ni wakati sasa mh Rais aamuru uchunguzi huru ufanyike dhidi ya waliptaka kumuua Tundu Lissu. Kwa kufanya hivyo serikali hii itajitanabaisha kuwa ni ya kutenda haki ... nawasilisha
Nakubaliana nawe, lakini najua hawawezi kufanya hivyo. Hawa wote wanalinda maslahi yao hata kama kiongozi wao kaondoka.

Ndiyo, Tundu Lissu au mtu/watu wanaomwakilisha wawasilishe ombi hilo kiutaratibu ili pawepo na kumbukumbu.
Serikali wakikataa kwa kulinda watu wake au heshima yake hapo itajulikana wamekata.

Kwa hiyo Tundu Lissu atumie njia zake, kama bado hajaanza, kufanya uchunguzi wa kuwatambua bila ya shaka yoyote wahusika waliopanga na waliotumwa kutekeleza uhalifu huo.

Siamini kwamba hili jambo halimsumbui akilini Tundu Lissu, kutojua, au kutokuwa na uhakika na ushahidi kamili wa nani wahusika waliotaka kutoa roho yake.
 
Well said mkuu , ikibidi chama chake kimsaidie
 
Hii ingekuwa agenda namba moja ya CHADEMA watakapoonana na Mh. Rais. Ni fursa pia kwa serikali kujisafisha.
 
Dhalimu ndio muhusika, hivyo usitegemee uchunguzi kufanyika. Japo sio vibaya kudai uchunguziguzi ufanyike, na wakigoma ndio ushahidi wa wahusika unazidi kukamilika.
Exactly, na hapo dunia nzima itajua wote Lao moja
 
Lissu ninani azalishwe yeye huko alipo anasafisha matako ya wazungu na mwenzie Lema na Corona hii chanjo hii wanachekacheka tu na kusema "mi ni mtu mkubwa Huko Africa nione hivi hivi "
Pumbavu
 
Haki na uhuru vitaiweka serikali huru.
Sahau hilo wanalindana hawa Mungu pekee ndio hukumu ya haki kamlipia Lisu.
Waliotaka atangulie wametangulia wao pili waliobaki hai hukumu ya Mungu awatoikwepa kama albadili imeanza juu huku chini kwenye ile chain itasafisha tu.Wengine Wana aibu na hatia ya milele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…