Nchi ina mfumo wa vyama vingi tangu 1992 kwanini maccm waendelee kufanya uhuni wao kwa miaka 30 sasa kukumbatia katiba ya mfumo wa chama kimoja? Kwanini Butiku na Warioba ambao ni maccm damu damu wanaunga hoja ya kuwa na Katiba mpya. Kwanini Bashiru kabla ya kuwa Katibu Mkuu wa maccm aliona umuhimu mkubwa wa kuwa na Katiba mpya?
Je katiba mpya ni takwa la wanasiasa au la wananchi......??
 
Ni maoni yako. Kuna ambao wanapata maisha bora kupitia katiba hii hii. Kuna watendaji wanaongeza pato la taifa kupitia katiba hii hii.

Rwanda hana katiba nzuri lakini nchi yao inapaa kiuchumi.
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Sema kimeumana..hahahahhahaha..nmefurah sana..mama anaupiga ule ule wa mzee baba sema kwa saut ya kinyonge sana.saf mama samia

Mnaohis hamwez ish bila siasa imekula kwenu
 
Unafikiri katiba mpya itasababisha mshinde uchaguzi? kwa nini usiamini katika kujenga vyema chama chenu? Je unafahamu kwamba Vyama vingi vya upinzani hapa nchini ni vya hovyo hovyo tena bado hawajitambua? Je malengo yenu ya katiba mpya yanalenga nini zaidi ya kutaka kushinda uchaguzi? Nitajie katiba mpya ya nchi yoyote ilivyosaidia graduate wote wa nchi hiyo kupata ajira,
Mwisho naungana na wewe ukitaka katiba mpya ingawa malengo yako hayajaangalia masilahi ya walio wengi.
 

Mkuu, nini kimebadilika?

Alisema Samia = JPM watu wakamshangilia na wengine huku wakanuna.

Nini alifanya? Leo hii kina Nigrastratatract wanapanga kuunda chama kipya.

Anachosema acha aseme. Tujikite kwenye anafanya nini. Hilo la kwanza. Ila la msingi zaidi ni kuwa tumtake kuheshimu katiba kwa kuendelea na shughuli zetu kwa mujibu wa katiba. Huo ndiyo msingi wa hoja kwenye uzi huu:


Kwa nini kelele za chura tusinywe maji?
 
Ni maoni yako. Kuna ambao wanapata maisha bora kupitia katiba hii hii. Kuna watendaji wanaongeza pato la taifa kupitia katiba hii hii.

Rwanda hana katiba nzuri lakini nchi yao inapaa kiuchumi.
Hii katiba ipo toka mwaka 1977 ingekuwa nzuri basi CCM wasingeiweka kwenye ilani ya uchaguzi mwaka 2015 ibadilishwe. Ofcourse tunajua kuwa Serikali ya Magufuli na Samia akiwa makamu wake ilifanya uhuni na kukataa kutekeleza suala hilo!

Haiwezekani mtu aliyeomba kazi ya kuwa makamu mwenyekiti wa bunge la kubadili katiba aone eti katiba mpya siyo kipaumbele chake. Kwa hii flipflop ambayo rais anaifanya anaonyesha kuwa naye kanogewa na katiba hii ya kidikteta
 
Wapi nilipoandika kwamba Katiba mpya itasababisha Chadema ishinde uchaguzi? Unajua chochote kuhusu uchaguzi huru na wa haki ambao vyama na Watanzania wanashiriki bila ya hofu ya kupigwa mabomu ya machozi, risasi na kuibiwa kura zao?

Mbona maccm Butiku na Warioba nao wanaipigia debe Katiba mpya? Mbona Mkapa kabla ya kufariki alitaka uchaguzi wa 2020 usimamiwe na Tume huru!?

Huwezi kusema eti hatuhitaji katiba mpya Kwa sababu vyama vingi nchini havijitambui na vya hovyo hovyo.

Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi ni haki yetu Watanzania bila kujali uwepo wake utabadili vipi matokeo ya uchaguzi nchini.

 
Samia ni mccm tu, Katiba Mpya na Tume huru ni kitanzi kwa CCM.
 
Mimi nilisema Mkuu Maza sina imani naye sasa maneno yangu yametimia Mkuu.

Wakuu BAK na bwana Missile of the Nation sioni penye lolote jipya. Kumbukeni huyu mama alishatamka:

Samia = JPM

Kuna iliyo more serious leo kuliko hiyo? Kwani hata aliyosema hivyo alifanya nini?

Jamani tuwe watulivu hakuna lolote jipya.

Kufahamu haki haitakuja kwa kupewa ni suala la msingi sana. Tulipofika hata angekuwa jiwe angesalimu amri.

Vita hivi ni vita vya watu wanaotegemea kusikia habari mbaya zaidi kuliko kila mbaya tunazopata.

Ni kwa njia hiyo tu ambayo kwayo tutashinda.
 
Reactions: BAK
Ni vema Rais Samia akaruhusu mchakato wa katiba mpya kufanyika kuliko akasubiri alazimishwe.

Rais hajui kuwa hawezi kupata wawekezaji makini bila kuwa na sheria nzuri ja zinazoheshimika na kila mtu. Huwezi kupata sheria nzuri kama huja katiba nzuri.
 
Kwanini mnataka kuchukua nafasi kama wasemaji wa wananchi? chadema ndo waongeaji wakuu wa katiba?
 
Hiyo ni sawa na kumwuliza mtu kama anataka usingizi mzuri au godoro zuri.
 
Ccm ni ileile, hata kama Rais ni mama lazima muisome namba kina faru John & Co.
 
Ni ngumu sana nchi hii kupata katiba nzuri kwasababu agenda yenyewe imetekwa na wanasiasa, tena uchwara.

Wananchi wamewekwa pembeni.
Hao wanasiasa wanapigania katiba mpya kwa maslahi ya nani.....??
 
Je unadhani wananchi wana uelewa wa umuhimu wa katiba na faida za moja kwa moja zitokanazo na mabadiliko ya katiba mpya.......na kipi ni kipimo cha wananchi cha uelewa wao juu ya katiba mpya......??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…