Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Nyie mnaodai katiba mpya ni WAPUMBAVU. Inawezekana vp kwa bunge lile 99% ni CCM lijadili na kupitisha mnayotaka nyie?? Hivi hamuoni kuwa ni upumbavu? Kwann msihangaike na tume huru ya uchaguzi ili mkijaa bungeni muweze pata uungwaji mkono.
HUWA NASHANGAA SANA MTU KAMA MBOWE KUWA MWENYEKITI WA CHAMA. YAAN MPUMBAVU ANAWAONGOZA WEREVU.
 
Rais kutuzuia wananchi kutaka namna ya kuongozwaje hiyo ni dharau kubwa ya rais na chama cha mapinduzi kwa wananchi.
Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali!

Ccm wanaona katiba mpya kama nyaraka ya uchaguzi, hivyo hawako tayari maana wanajua kukiwa na mazingira rafiki ya ushindani, itakula kwao. Hii kelele ya katiba mpya haitakiwi kusimama, ccm na mwenyekiti wao wanajua hii agenda ni ngumu kwao, hivyo wanajaribu kutupoteza maboya ili tutoke kwenye reli. Hakuna kuachia ni hapa hapa.
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Eeeeehhh...naona ufipa sasa akil zinawakaaa sawaaa..mbumbumbu wa mwishoo..yaan ccm inawachezesha ngoma usiku na mchanaa
 
Nyie mnaodai katiba mpya ni WAPUMBAVU. Inawezekana vp kwa bunge lile 99% ni CCM lijadili na kupitisha mnayotaka nyie?? Hivi hamuoni kuwa ni upumbavu? Kwann msihangaike na tume huru ya uchaguzi ili mkijaa bungeni muweze pata uungwaji mkono.
HUWA NASHANGAA SANA MTU KAMA MBOWE KUWA MWENYEKITI WA CHAMA. YAAN MPUMBAVU ANAWAONGOZA WEREVU.

Aliyekuambia lazima katiba mpya iandikwe kwenye hilo bunge la majizi ya kura ni nani?
 
Katiba haina Chama lakini iliyopo inakumbatia Chama kilichopo madarakani.Lakini lazima wanasiasa wote wajue hakuna Chama au Utawala wowote utakaodumu milele.Ikitokea kuna dalili ya Chama au Utawala kama huo Mungu mwenye huingilia kati, amini usiamini CCM inakwenda kuondoka madarakani na haitakuwa rahisi lakini inakwenda kutokea hatuna miaka 20.
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie Katiba Mpya, tungependa kumueleza Rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au Serikali yake kujenga Uchumi, Labda Rais atueleze, je Katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu? Hapa kimsingi Rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya Katiba wanayoitaka.

2. Mchakato wa Katiba Mpya si hisani ya Rais bali ni hitajio la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayo-govern Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya, Sisi wananchi tunamtaka Rais atekeleze Sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.

3. Hofu ya Rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya Rais ya kukataa kuipa Katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa Makamu wa Rais, Rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta Katiba Mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata Katiba Mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki Katiba Mpya, lakini kama alivyowahi kusema Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya Katiba Mpya haitakufa mpaka ipatikane.

4. Kujenga Uchumi bila kuwa na Katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa Rais Mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya Serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila Katiba nzuri huwezi kuulinda Uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la Katiba Mpya ni muhimu sana

5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na Katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa Rais, na kiukweli ni Katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni Katiba Mpya na si maneno matamu tu ya Rais Samia
Hivi hakuna uwezekano wa kisheria kudai mchakato uendelee? Mfano kufungua kesi mahakama kuu kwa maana tayari ilishatungwa sheria...
 
Aliyekuambia lazima katiba mpya iandikwe kwenye hilo bunge la majizi ya kura ni nani?
Ww mwehu, sasa ujue kuwa sheria inasema wabunge wote wanakuwa wajumbe wa katiba je unadhani watapitisha matakwa yenu? Anzeni na TUME YA UCHAGUZI.
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Mkuu, hapa sio swala la kuuliza sababu mchakato ulishakuwepo na haukukamilika.
 
Nani anataka kupiga kura yake ya kuchagua Rais, Mbunge au diwani kisha kura hiyo ikaibiwa kwa mtutu wa bunduki? Chama kiko madarakani kwa miaka 60 sasa kimefanya lipi katika kuboresha uchumi wa nchi katika hiyo miaka 60?

Ajira hakuna graduates wanasaga lami, elimu yetu ni ya hovyo sana, matibabu pia ni hovyo sana, usafiri pia ni hovyo sana. Mishahara ya wenye ajira ni ya chini mno miaka sita sasa bila nyongeza. Hebu tia akili kichwani japo KIDUCHU badala ya KUKURUPUKA.
Magufuli alisitisha kwa kigezo cha uchumi. Leo mama akasema uchumi umeshuka. sasa kuna uhakika gani uchumi utapanda ndipo katiba mpya ipatikane.
 
Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
Too simple, una maana katiba si muhimu. Kama katiba iliyopo inampa nafasi rais aliyepo madarakani nafasi ya kucheza na maisha ya watu iachwe tu ili mfradi watu wanakula?
Pamoja na hayo mimi naamini mama atalishughulikia hili. Anajipa muda ili ajue inaendaje, hataki kukurupuka.
 
Kwa nini wanasiasa,hamuwaulizi wananchi,nyinyi mwataka Katiba mpya,wakati wananchi,twataka mkono uwende kinywani.Nyinyi wanasiasa mwatetea upande wenu,hamtaki kuwasikiza wananchi wanataka nini.
Mbona Wananchi walishaulizwa na wakatoa maoni yao. Cha kujiuliza sasa ni kwa nini hao walio madarakani hawataki kufuata maoni ya Wananchi...!!?
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Sasa nani kakudanganya Kuwa Katiba inazuia uchumi kukua au inazuia mlo wa Mtanzania...!?
 
Ww mwehu, sasa ujue kuwa sheria inasema wabunge wote wanakuwa wajumbe wa katiba je unadhani watapitisha matakwa yenu? Anzeni na TUME YA UCHAGUZI.

Narudia tena, sio lazima hiyo katiba ikajadiliwe kwenye hilo bunge la majizi ya kura.
 
Mimi sio mfatiliaji sana wa siasa ila kwa mtazamo wa nchi inavoenda kama kuruhusu chanjo ya covid,kusainiwa kiholela mikataba ya uwekezaji,kuendelea kuminywa kwenye kodi,kuanza kujitokeza matukio ya uhalifu baada ya polisi kupumzika kwa muda mrefu kidogo na mpaka hii leo ndani ya siku 100 tu mama kashaanza kukiri urais ni kazi ngumu hata kusema tumuache kidogo,Hii inaonesha Hali ishaanza kuwa tete kwa upande wake ingawa inabidi aoneshe ukakamavu,wazee tukumbuke Mwanaume alianza kuumbwa kabla ya mwanamke hivo itafika tu muda tutamkumbuka Rais magufuli na alishasema tutamkumbuka tena kwa mazuri si mabaya...Ni kumuomba tu Mungu maana me nnavojua hata iweje maisha hayajawai kuwa rahisi kwa watu Wa kipato cha chini tusipoangalia tunaweza kurudi tulipotoka kibaya pia rais magufuli amekufa na maono yake kichwani ni vigumu kuelewa alikuwa anataka kutufikisha wap ingawa dalili zilishaanza kuonekana.

PRAY FOR TZ PRAY FOR MAMA SAMIA.
 
Bado mama ni bora kuliko shetani jiwe. Tutaendelea kumshauri kila inapowezekana
Nakubaliana na Pythagoras. Mama hajasema katiba mpya haitakuwepo. Angalau huyu tunaweza kufanya biashara naye. Tumpe muda ajiweke sawa. Lands sasa hivi tuombe "minimum constitutional reforms" ikiwemo ya kuunda tume huru ya uchaguzi. Mengine tusubiri 2025 -2030.
 
Mumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Kwani sisi tunaojadili hapa ni Raia wa Mbinguni? Akili zingine bwana!
 
Nakubaliana na Pythagoras. Mama hajasema katiba mpya haitakuwepo. Angalau huyu tunaweza kufanya biashara naye. Tumpe muda ajiweke sawa. Lands sasa hivi tuombe "minimum constitutional reforms" ikiwemo ya kuunda tume huru ya uchaguzi. Mengine tusubiri 2025 -2030.
Mama kasema Katiba mlya badae kidogo kuna mambo mengi sana ya Kufix. Ndani ya Chama chake pekee kuna Kenge wengi mno. Lazima hawa awadhibiti kwanza. Mama nimemwelewa sana ameongea lugha ya fasihu mno. Hata hivyo Mama atafanya mangapi ndani ya miezi mitatu? Bado ana miaka minne mbele.

Tazama tulivyo na amani ndani ya miezi mitatu?? Je itakywaje miaka mnne iliyobaki?

Bado Mama yuko vizuri mno.
 
Back
Top Bottom