Kuhusu Katiba Mpya: Hoja ya Rais Samia haina mashiko
Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
Basi nyie wachumia tumbo msiojua mbele wala kesho kaeni kimya.
 
Hicho kibovu ndio maana yeye Ni rais na kwa vile ashaonja utamu sidhani Ni rahisi kihivyo ajitose kwenye fungu la kukosa.
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Hivi kasema uchumi utatengemaa lini?

Na kipimo cha uchumi kuwa mzuri ndipo katiba ifanyike kipimo cha uchumi huo ni kipi; hadi hapo kila mwananchi atakapokuwa na Noah Yake?

Naona mama hajui namna ya kudanganya ili watu waweze kuamini ayasemayo.
 
Rais kutuzuia wananchi kutaka namna ya kuongozwaje hiyo ni dharau kubwa ya rais na chama cha mapinduzi kwa wananchi.
Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali!
Atawaambia vumilieni; mbona miaka yote mlivumilia na hiyo katiba mbovu hadi alipokuja kuivuruga hata hiyo mbovu mtangulizi wake?

Atawatuliza kwamba yeye atafuata hiyo mbovu bila kuivunja hadi hapo uchumi utakapokuwa katika hali nzuri..., hana haja ya kueleza uchumi wa namna hiyo ni wa aina gani!
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie Katiba Mpya, tungependa kumueleza Rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au Serikali yake kujenga Uchumi, Labda Rais atueleze, je Katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu? Hapa kimsingi Rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya Katiba wanayoitaka.

2. Mchakato wa Katiba Mpya si hisani ya Rais bali ni hitajio la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayo-govern Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya, Sisi wananchi tunamtaka Rais atekeleze Sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.

3. Hofu ya Rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya Rais ya kukataa kuipa Katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa Makamu wa Rais, Rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta Katiba Mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata Katiba Mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki Katiba Mpya, lakini kama alivyowahi kusema Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya Katiba Mpya haitakufa mpaka ipatikane.

4. Kujenga Uchumi bila kuwa na Katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa Rais Mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya Serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila Katiba nzuri huwezi kuulinda Uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la Katiba Mpya ni muhimu sana

5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na Katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa Rais, na kiukweli ni Katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni Katiba Mpya na si maneno matamu tu ya Rais Samia
KWA kweli kitendo Cha mama alichokiongea kuhusu vyama vya siasa sijapenda,kwamba anaendelea na katazo lile ambalo ni kinyume Cha katiba, kwamba mtu afanye mikutano katika eneo lake, mh SSH umenikwaza Sana KWA kauli yako, sio sawa
 
Mama anawafurahisha wapinzani kweli kweli ngoja ifike 2024 ndo ataona rangi zao
 
Ajabu ni kwamba kila rais anayeingia hutaka tuamini kwamba nchi ilikuwa inaliwa na hivyo inahitaji kujengwa upya.Ukiwasikiliza utafikiri hawakuwa sehemu ya serikali zilizotangulia.Anadai ajenge uchumi Kwanza,je,huo uchumi ataukamilisha baada ya muda gani? Kwa mujibu wa katiba iliyopo amebakiza miaka minne tu ikiwa tungelikuwa na uchaguzi huru na wa haki.Ataanza kutwambia ,huu uchumi ninaoujenga nitamwachia nani?
 
Nilikuwa na bado nipo makini kusema lolote juu ya huyu mama, maana huwezi mtabiria mtoto akianza kuona!.

Wale wanazi wa kusifia na kusema tuliumizwa sana huko nyuma nawafuatilia kwa kuzoom nione wanachokoment.
 
Rais Samia anasema eti suala la kipaumbele kwake ni uchumi kwanza halafu mambo ya katiba mpya ni ya baadae huko mbeleni.

Ningependa kumkumbusha Rais Samia kuwa, hoja ya Katiba Mpya ni hoja nyeti, ni suala muhimu sana na haliwezi kuwa option ya pili katika mambo yanayopaswa kufanyika nchini kwa sasa. Na hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Katiba mpya haizuii kujenga uchumi
Rais anaposema eti tumpe muda ajenge uchumi kwanza ndo afikirie Katiba Mpya, tungependa kumueleza Rais kuwa kuwa na katiba mpya hakumzuii yeye au Serikali yake kujenga Uchumi, Labda Rais atueleze, je Katiba bora iliyo nzuri inazuiaje yeye kuvutia wawekezaji, inazuiaje kuboresha utalii, inazuiaje kujenga miundo mbinu? Hapa kimsingi Rais hana hoja yenye mashiko kabisa juu ya kukataa kuwapa wananchi aina ya Katiba wanayoitaka.

2. Mchakato wa Katiba Mpya si hisani ya Rais bali ni hitajio la kisheria
Ipo sheria ya mwaka 2012 inayo-govern Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya, Sisi wananchi tunamtaka Rais atekeleze Sheria hiyo, asifanye hili suala kama hisani yake binafsi, hili ni hitajio la wananchi wengi.

3. Hofu ya Rais ni ya kisiasa na si kimaslahi ya kitaifa
Kauli ya Rais ya kukataa kuipa Katiba kipaumbele ilianza kwenye awamu ya tano ambayo yeye alikuwa Makamu wa Rais, Rais wa wakati huo na yeye alisema hoja hizohizo za kujenga uchumi kwanza kabla ya kuleta Katiba Mpya, leo hii tuna miaka mitano bado tunapigwa kalenda hizohizo za ngoja tujenge uchumi. Huhitaji kuwa genius kuona kwamba hofu ya viongozi hawa ni hofu za kisiasa tu, za kuhofia hatma zao na vyama vyao kisiasa iwapo Taifa litapata Katiba Mpya, ni dhahiri wahafidhina ndani ya CCM hawataki Katiba Mpya, lakini kama alivyowahi kusema Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Hoja ya Katiba Mpya haitakufa mpaka ipatikane.

4. Kujenga Uchumi bila kuwa na Katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa Rais Mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya Serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila Katiba nzuri huwezi kuulinda Uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la Katiba Mpya ni muhimu sana

5. Watanzania hatuko tayari kurudi katika utawala wa kidikteta aina ya awamu ya tano
Ktk utawala wa awamu ya tano tuliona matendo ya kinyama na kiuonevu yaliyofanyika, sababu mojawapo ya matendo hayo ni kuwa na Katiba inayotoa mwanya mtawala kuvunja sheria bila consequences ikiwemo kushtakiwa, Katiba hii imetoa mamlaka makubwa kwa Rais, na kiukweli ni Katiba ya kidikteta, Hatuwezi kuruhusu scenario ya kupata aina ya uongozi wa awamu iliyopita, na guarantee bora ya kutofika huko ni Katiba Mpya na si maneno matamu tu ya Rais Samia
Hata wewe huwezi kuongoza nchi eti kila mwananchi atasema lake na mapendekezo yake na wewe ufuate tu,nchi haitatawalika maana mnadhani hilo ndilo linalowezekana,msidhani katiba ni kitu rahisi sana,kina madhara yake pia
 
Samia anacheza vizuri huu mziki, leo anapiga rungu inakua zogo, kesho anatupoza na lingine tunashangilia, kesho kutwa rungu tunaanza yalaaaaaa next anatupoza tena tunashangilia.

Hivo hivo Mama tutafika.
 
4. Kujenga Uchumi bila kuwa na Katiba ya kuulinda ni kazi bure
Hii katiba tuliyonayo inampa Rais Mpya power za kuvunjilia mbali mafanikio ya Serikali zilizopita, anaweza kusitisha mradi wa kimkakati, anaweza kuingia mikataba ya siri isiyo na faida, anaweza kutapanya rasilimali zetu na asishtakiwe. Kwa hiyo ni dhahiri hata ujenge uchumi mzuri kivipi, bila Katiba nzuri huwezi kuulinda Uchumi huo, ndiyo maana hitajio letu la Katiba Mpya ni muhimu sana
Hapa Uko Sahihi 100%, Mfano ni Uongozi wa Awamu ya Tano, nchi iliendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja. Alilokuwa wanalisema ndio ilikuwa sheria na kila mtu alikubaliona nao apende asipende...Katiba mpya ndio jibu la mambo ya namna ile...
 
Back
Top Bottom