Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Unajua wewe una ji contradict mwenyewe wala hata huelewi ulicho kiandika.

Mwanzoni ulianza kwa kusema, Mungu hapimwi katika vitu na mazingira ya kibinadamu.

Halafu tena unasema kila kitu kinacho exist na chenyewe ni Mungu...

Hapa tayari umeshampima huyo Mungu kwaku mfananisha na vitu na mazingira ya kibinadamu.

Kama Mungu ni kila kitu na kila kitu ni Mungu, Kwa hiyo huyo Mungu alijiumba ili awe kila kitu kisha ajitawale tena yeye mwenyewe?

Kama kila kitu ni Mungu including sisi binadamu, Utasemaje kwamba tuliumbwa?

Kama sisi binadamu tuliumbwa, Je sisi sio Mungu?

Kama sisi binadamu ni Mungu, Ni Mungu gani tena alituumba?
 
Nashindwa kuelezea katika lugha ya kawaida, navyosema Mungu hapimwi katika vitu namaanisha watu humpima Mungu Katika vitu vya nje yaani katika macho ya kawaida wakidhani ni extra Ili wapate matokeo,

Swali lako la mwisho kila unachoona Katika macho ya kawaida kilitoka katika vitu visivyoonekana ina maana kabla havijaexist kila kitu kilikuepo katika Ulimwengu wa Roho infinity havina mwanzo wala mwisho,
Creation ilitokea kudhihirisha vitu vya ndani vikatoka nje dhahili

Kiufupi najaribu kuelezea katika lugha ya Kibinadamu ndio maana nakosa namna ya kuelezea vitu spiritual maana katika lugha ya Kibinadamu ni vitu vigumu kuvielewa
Ni hivi kila kitu katika Ulimwengu wa Roho na Mwili vipo katika Infinity

Weird!
 

Hivi ndivyo nnavoelewa!kila kitu kinachoonekana kwa macho ujue kilianzia kwanza kwenye ulimwengu wa roho!ulimwengu huu una mambo mengi sana ambayo hayajawahi kuonekana na macho yetu kuliko haya tunayoyaona kwa macho!Nadiriki kusema inawezekana ukaishi Duniani miaka 200 na ufahamu wako kuhusu dunia na ulimwengu ukawa haujafika hata 1%.
 
Huo ulimwengu wa roho kama haujawahi kuonekana kwa macho, Aliyesema ulimwengu huo upo yeye aliuona wapi?
 
Kweli mkuu Ulimwengu wa Roho ni complex sana sema watu wengi hawajawahi kuuexperience ndio maana inakua ngumu kumuelezea mtu ni namna gani mambo yanaenda katika Ulimwengu,
Unajua hata wanasayansi wanajaribu kufanya jitihada kutaka kuufahamu Ulimwengu wa Huu wa kawaida kwa kutumia akili zao formula,na namna ya Elimu walizojitungia wenyewe hapa ndipo utaona kina Kiranga &co wanajaribu kutaka kutumia formula kuelezea Ulimwengu ajabu hawajui Ili uujue Ulimwengu huu hata kwa pointi 1 anzia kwenye Spiritual Realm kuuchunguza utakuja kushuhudia mambo ya ajabu na makubwa yatakayo kupa mshtuko wa moyo
Maana huko ndiko utapata namna gani Light na Dark science vinafanya kazi
Mambo ya Dimensions na mwingiliano wa viumbe katika Ulimwengu wa mwili na roho unavyoathiri maisha ya kawaida utakuja shtuka hapa Duniani kuna race kipao zimejichimbia kwa maelfu ya miaka na zina fanya mambo yao kimya kimya ila kwasababu wapo high advanced kwenye science na Technology wamejificha kwenye Dimensions ambapo kamwe hutaona kitu,
Their is secret behind all na ndio maana kuna secret Societies zinazooparate Haya maswala na wachache wanajua hii siri ya Ulimwengu wa Roho ndio wanatawala huu Ulimwengu wa macho ila wanazuga hawaelewi kitu kumbe ndio ma master Mind!
 
Wewe huo ulimwengu wa roho uli u experience wapi?

Kama ulimwengu wa roho hauonekani, wewe uliuona wapi?
 
Huo ulimwengu wa roho kama haujawahi kuonekana kwa macho, Aliyesema ulimwengu huo upo yeye aliuona wapi?
Hahaha Ulimwengu wa Roho haipimwi kwa macho na Mazingira mkuu,
Hauwezi ukaoneshwa ni huu au ule ukitaka kuu taste lazima Uingie huko maana ni Dimension nyingine,
Na kama unataka kuingia
Na unataka kuingia huko acha kuuwekea limit ubongo na moyo wako njoo nitafute kwa gharama yoyote nitakupa starting point nianze kukupa mambo ya Dimensions uingie huko kuona mambo nitafute nipo seriously!
 
Wewe huo ulimwengu wa roho uli u experience wapi?

Kama ulimwengu wa roho hauonekani, wewe uliuona wapi?
Nitafute nikupe siwezi kukuelezea tu hapa ukaelewa coz hata mimi nilikua kama wewe Mwaka jana tu nilibadiliasha gear angani,
Kiufupi nilishafikia kua Senior Atheist humu humu ila kutokana na kuchimba ukweli kuhusu accient civilization na high advanced tech ya kale nikaja kuingia 18 za Ulimwengu wa Roho (Spiritual Realm)
Nikaja pata mambo makuu yaliyonibadilisha mtazamo na sikuona aibu kurudi hapa JF na nikakiri kua nilikua sina maarifa na kama ulikua mfuatiliaji wa nyuzi zangu za maswala ya Accient civilization utajionea namna gani nimebadilika,
Now natambua Ulimwengu wa Roho unavyo endesha mambo makubwa na maendeleo na tafiti soon nitakuja dondosha uzi hapa namna gani Spiritual Realm inaendesha mambo yake na athari zake nitqkukaribisha katika hiyo thread!
 
Wewe huo ulimwengu uliupima na nini?

Kama ulimwengu huo hauonekani, wewe uliwezaje kuuona?

Huoni kwamba unaji contradict mwenyewe, Kama ulimwengu huo hauonekani wewe uliwezaje kuuona?

Kama uliweza kuuona huo ulimwengu, Basi huo ulimwengu unaonekana.
 
Huo ulimwengu wa roho ndo ushirikina au?
 
For greatest thinker ONLY 🏆
 
Huo ulimwengu wa roho ndo ushirikina au?
Ulimwengu wa Roho umegawanyika pande mbili
Mosi ni
Ulimwengu wa Nuru Unaongozwa na Master of High Realm Yashua Amashiach Mnazarene (Jesus Christ of Nazareth)
Kama LORD GOD huyu ni Nuru ni ana mng'ao mara Quatllion kuliko mng'ao wa jua letu na ndio source of everything in our Universe na out of our Universe,
Huyu anaitwa the Son of God na kila kitu kiliumbwa kwa ajili yake!

Pili ni Ulimwengu wa giza huu Unaongozwa na mkuu wa Giza Mwanzo alijulikana kama Queen of Heaven sasa ndie Ibilisi/Satan huyu aliyeteka uumbaji hatujui chanzo chake ila tangu Mwanzo wake ni mbaya na Mwongo hana kweli ndani yake ndie kabeba Maovu yote yanayoathiri Ulimwengu zote mbili na ana mwisho wake,
Na mwisho wake ni kukomeshwa na yule Mwana wa Mungu yaani Neno aliyefanyika mwili Yashua Amashiach Mnazarene!

Huo utakua mwisho wa uovu (end of evils)

Ndio maana kuna battle kali katika hizi Ulimwengu mbili nikipata muda nitaeleza ni namna gani haya mambo yanaendeshwa!
 
Hakuna contradiction hapa kitu kama hukioni wewe Sio kila mtu hakioni au hakipo
Hata ungerudi Mwaka 1420 na kamwambia Vasco Da Gama kwamba tunaweza kutoka Portugal to India kwa chombo kinachopaa angani kwa masaa tu tunafika atakuona Mwendawazimu na unajicontradict unavyompa formula zake,
Hata huu umeme unatumia ukirudi Mwaka 1677 ukamwambia George Washington kwamba unaexist atakuona punguani ila haimanishi kitu ambacho hukioni wewe hakipo ila inahitaji formula kukiona kinaexist hapo ndipo siri ya maarifa inaanzia
Fungua ubongo tukupe maarifa vitu tunavyoexiperince wenzio bila hivyo utakua gizani na utajionea na maarifa na hoja kumbe bado kindergarten kuhusu mifumo ya vitu vingi!
 
Well narrated! Tatizo Infropreneur inaonyesha wazi amejikita kwenye ubishi yaani pamoja na maelezo na mifano clear uliyoweka hapo juu still atakuja kubisha......
 
Well narrated! Tatizo Infropreneur inaonyesha wazi amejikita kwenye ubishi yaani pamoja na maelezo na mifano clear uliyoweka hapo juu still atakuja kubisha......
Hata mimi nilikua kama yeye miaka michache tu hapo nyuma ila kutokana na utomaso nikajikuta katikati ya sintofahamu nilipojiona nimeingia kumi na nane za Spiritual Realm nikaja jua kumbe kila kitu kina wenyewe!
 
Sasa usiseme kwamba huo ulimwengu hauonekani.

Kama wewe umeweza kuuona huo ulimwengu hata mtu mwingine anaweza kuuona hivyo hivyo.

Hivyo huo ulimwengu unaonekana.

Hakuna ulimwengu usio onekana.
 
Well narrated! Tatizo Infropreneur inaonyesha wazi amejikita kwenye ubishi yaani pamoja na maelezo na mifano clear uliyoweka hapo juu still atakuja kubisha......
Huyu Dumas the terrible alianza kusema kwamba huo ulimwengu wa roho hauonekani, Halafu tena anadai yeye anauona.

Hivi huoni kwamba ana ji contradict mwenyewe?

Kama ulimwengu huo hauonekani, yeye kawezaje kuuona?

Kama ameweza kuuona huo ulimwengu, atasemaje kwamba hauonekani?

Huoni Contradiction hapo?
 
Hata mimi nilikua kama yeye miaka michache tu hapo nyuma ila kutokana na utomaso nikajikuta katikati ya sintofahamu nilipojiona nimeingia kumi na nane za Spiritual Realm nikaja jua kumbe kila kitu kina wenyewe!
Hakuna spiritual realm mambo yote yapo kwenye ulimwengu huu huu unao onekana...
 
Wacha ninywe maji kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…