Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

kipawa kinachowezesha kufikiri, kuelewa, kuwasiliana, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo.
Ulijuaje kinaitwa akili?

Au umekuta jina tu kipawa hicho kikiitwa akili?

Aliyekiita kipawa hicho akili alijuaje anacho na kuthibitisha kinaitwa akili kweli?

Au alibuni jina tu " Akili" na kuamua kuita hivyo, kipawa hicho cha kufikiri, kuelewa,kujifunza na kuamua?
 
Nadhani imetosha kukupa maana ya neno akili. Kama bado hujaelewa basi ni juu yako.
 
Subri apigwe na ugonjwa tu kama wa kisukari, kansa au figo uone kama ataendelea na ngonjera zake hapo juu.

Wewe hauwezi hata jiongezea japo umri ufikishe miaka 200, halafu unaanza kuvimba dhidi ya aliyeviweka vyote hivi tunavyoviona na tusivyoviona.

Hizo imani zote lengo mama ni kumuabudu na kumtafuta Mungu mkuu muumba wa vyote ingawa zinatofautiana utaratibu, hivyo inawezekana wote wakawa sahihi.
 
Akili ni neno la kufikirika tu.

Si kitu ambacho kinaonekana au kipo kwenye ubongo wa mwanadamu.

Ufanyaji kazi wa ubongo ndio ulipachikwa jina "Akili"

Ukipasua kichwa cha binadamu huwezi kuta hiyo akili
Akili ni sawa na ubongo? Yani unafananisha Mind na Brain? Nadhani unapaswa kufanya tafiti ya kina kuhusu akili/Mind.
 
Unajuaje ulimwengu una mwanzo?
 
MUNGU wa kweli ni Mungu wa Mbinguni, wanamwita Yaweh, Jehovah, ambaye pia ndiye Mungu wa Abraham, Mungu wa Isaka na Mungu wa Israel. Aliyeumba Mbingu na Dunia na Viumbe wote wanaoonekana na wasio onekana, vilivyohai na visivyohai. Yeye ndiye Asili ya yote, Hana mwanzo na hatakaa awe na Mwisho.

Ukielewa chukua, hutaki endelea na majizingaombwe ya Dunia.
 
Nimekwambia hivi, ufanyaji kazi wa ubongo ndio ulipachikwa jina Akili.

Hiyo mind unaweza kuthibitisha ni nini?
Hakuna tofauti kati ya Mind, akili au intellect. No vitu ambavyo huwezi ona kwa macho.

Lakni Brain ni physical na Ina kazi tofauti kama ku sence.
 
Unajuaje ulimwengu una mwanzo?
Mzee Wa maswali.... Yaani wewe Kila topic jamaa yangu badala ya kujibu hoja unaanza kumuhoji mtoa hoja.... Aseee... Why can't u just quit or skip the topic... We are not here to question each other rather to add inputs on what posted.... Nevertheless you better know questioning has never being the measure of intelligence. Reasoning is.
Hebu grow up Sasa!
 
Habagui dini wala kabila, yeye ni Mungu wa wote na kwake tutarejea.
 
Hakuna tofauti kati ya Mind, akili au intellect. No vitu ambavyo huwezi ona kwa macho.
Ndio maana nilikwambia Akili ni jina tu la ufanyaji kazi wa ubongo.

Huwezi kutaka uthibitishiwe akili ipo au haipo kwa vile akili ni neno tu.
Lakni Brain ni physical na Ina kazi tofauti kama ku sence.
 
Ndio maana nilikwambia Akili ni jina tu la ufanyaji kazi wa ubongo.

Huwezi kutaka uthibitishiwe akili ipo au haipo kwa vile akili ni neno tu.
Hatakama ni neno tu, Bado akili ipo na kama hauamni kwamba ipo basi kwako ndy itakuwa haipo.
 
Kwenye kujibu hoja kuna namna nyingi.

Kuna Socratic Method, tunakwenda wote mdogo mdogo kwa kuulizana maswali mpaka tunaelewana.

Unajuaje ulimwengu ni lazima uwe na mwanzo?

Kama hujajibu swali hili, hoja zote kuhusu "mwanzo wa ulimwengu ni nini?" zinakuwa zina mapungufu makubwa.

Kama uso wa dunia hauna mwanzo au mwisho, ni mfano wa tufe la mviringo ambalo ukizunguka unaweza kurudi palepale ulipoanzia, swali la kuuliza "uso wa dunia umeanzia wapi?" ni swali lisilo na msingi katika ukweli. Ni swali linalotokana na ujinga tu wa kutokujua kwamba uso wa dunia hauna mwanzo.

Sasa, tunarudi kwenye hoja ya ulimwengu, unajuaje ulimwengu una mwanzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…