Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Bado hujajibu swali la msingi,..usiruke stage

Nilikuuliza kwa unavyoona viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla,.Je huoni design yoyote kwa kutazama hivyo vitu?

Hiyo 👆🏼 ndiyo point ya msingi, unless ukimbie swali maksudi...

NB:- Jibu kwanza swali kisha tutafika hapo unapopataka easy kabisa.
 
Bado hujajibu swali la msingi,..usiruke stage
Sawa.
Nilikuuliza kwa unavyoona viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla,.Je huoni design yoyote kwa kutazama hivyo vitu?
Ndio Sioni Design yeyote ile kwa kutazama hivi vitu, Kwa sababu vitu hivi vinaweza kuwepo vyenyewe tu na designs zake. pasipo kuhitaji Designer.

Yani vimeweza kuji design vyenyewe tu.
Hiyo 👆🏼 ndiyo point ya msingi, unless ukimbie swali maksudi...

NB:- Jibu kwanza swali kisha tutafika hapo unapopataka easy kabisa.
 
Sawa.

Ndio Sioni Design yeyote ile kwa kutazama hivi vitu, Kwa sababu vitu hivi vinaweza kuwepo vyenyewe tu na designs zake. pasipo kuhitaji Designer.

Yani vimeweza kuji design vyenyewe tu.
Okay,..kwa majibu haya uliyotoa.., watu wenye akili timamu wakisema una ubishi usioingia akilini.....utawakatalia?

Kwa majibu hayo uliyotoa inathibitisha wazi kwamba umejipanga kubisha tu hata uletewe ukweli ulio wazi.

NB:- Nasema hivyo kwasababu akili yenye afya njema haiwezi kukataa uwepo wa designs tofauti tofauti kwenye viumbe hai, Dunia na ulimwengu kwa ujumla.
 
Vitu vyenyewe ndio Designs zenyewe.

Usicho elewa ni nini?
 
Tujitahidi kuwa watulivu huku tukiwekeza sana kwenye tafiti mwisho tutaujua ukweli au tutapotea kabla ya kuujua ukweli kitu ambacho hakina madhara kuliko hivi sasa tunavyotaka kulazimisha uongo kuwa ukweli.

Kama huyo Mungu yupo, basi yeye ndiye anatakiwa kuhangaika na sisi na sio sisi kuhangaika nae.... Kwa upande wetu tupambane na maisha ambayo tumejikuta nayo kwakuwa ndio tanatuhusu
 
Well well well. Ninaomba utulivu wako kidogo.

1. Japo kua kila culture inaamini miungu yake lakini culture zote zina vitu vinavyofanana...A. Maisha baada ya kifo kwa mfano wa mizimu na mababu B. Uwepo wa ulimwengu mwingine usioonekana kwa macho C. Kuwepo kwa viumbe wengine wasioonekana kwa macho.
Hii inaonyesha kuwepo kwa vitu common kwa watu ambao hata hawako karibu kijeografia mfno. America kusini na Afrika mashariki.

2. Japo hapana evidence yoyote kuhusu kuwepo kwa miungu hiyo ila evidence inayotolewa na hizo culture ni evidence ambazo hata Wanascience hawana majibu. Mfano...Tunajua kuwa sayansi ya madawa asili yake ni waganga wa Jadi, pia Astrology asili yake ni waganga wa jadi...Culture zilikua zinajua vitu vingi kuhusu sayari na nyota kwa namba ambayo haielezeki kwa kuwa hawakuwa na teknolojia hiyo au satelite miaka hiyo.

3. Japo miungu ipo mingi kwa ajili ya uzazi wa mashamba, mvua, magonjwa, kuagua na elimu ya nyota..culture zote zinaamini kuwapo na Mungu mmoja aliyeumba vyote...wengine wanaamini ni jua, wengine nature etc.

Nina evidence nyingi ila nitakaribisha maswali ili nisichoke kuandika.

Inapokuja kwa mtu ambaye haamini kama Mungu yupo kwa sababu hakuna ushahidi.

1. Science pia haina uwezo wa kuprove kuwa Mungu hayupo.

2. Science ikisema hakuna ushahidi kuwa Mungu hayupo inashindwa kuelezea kwa ushahidi asili ya kila kitu moja wapo asili ya ufahamu...Kumbuka big bang na theory zingine zinaongelea matter kuform matter...Mwamba kutengeneza mwamba mwengine kisa kugongana inaeleweka kisayansi, Ila matter kutengeneza viumbe vyenye ufahamu na uamuzi na kijitambua ni kitu Science haiwezi kukijibu. How can matter make consiousnes?

3. Dunia na sayari zinaonekana zimekaa kwenye mfumo ambao haiwezekaniki kutokea kwa bahati tu.

Jua lingeongezeka joto hata kidogo au kupungua hata kdgo kusingekua na maisha, dunia ingekaa mbali au karibu kdogo na jua au na sayari zingine kusingekuwa na maisha, ng'ombe kula nyasi, nyasi kupita kwenye matumbo yanayosababisha gesi ambayo ikitoka inanufaisha nyasi ni kitu ambacho hakiwezi kitokea tu.

Huwezi kujiuliza kawanini kila ugonjwa na kila sumu inayopatikana kwenye nature kuna tiba yake hapo hapo? Hiyo yote ni kwasababu vitu viligongana hewani kutengeneza dunia na sayari?

Hujiulizi kwanini kuna misimu na majira ya joto, baridi, mvua na ukame? Kwamba kungekua na vitatu kati ya hvyo kusingekua na maisha duniani?

Hujiulizi kama maisha ya viumbe vyote asili yake ni single cell organism kutokea baharini mbona bacteria hawabadiliki na kuwa watu? Fine inachukua mamilioni ya miaka, mbona bacteria walikuwepo tokea hapo?

Hujiulizi mbona bacteria wanamaamuzi binafsi ya kujongea kutoka eneo moja kwenda jingine japo kua hawana ubongo?

Hujiulizi kwanini DNA zetu na nyani zinalingana kwa asilimia 98 lakini sisi tunaenda hadi mwezini?

Bado nina vitu vingi kuliko nilivyoandika ila napenda kuwauliza swali moja. Utumie sayansi unipe evidence na measurement ya Hasira, Akili, Mawazo au hata nguvu ya mvutano!!!

Hivi vitu havina evidence inayoshikika wala kuonekana, ila haimaanishi kuwa havipo.

Namna ya kujua uwepo wa Mungu ni kuangalia dunia na maisha kuwa vitu hivi havijatokea by chance na haiwezekaniki kila kitu kikawa precise kama vimedizainiwa perfect kwa ajili ya kusapoti maisha.

Naamini huamini kuwa ulikua nyani eti?
 

Infropreneur
 
Binadamu anapambana kumtafuta Mungu kwa sababu ya kuhitaji vitu visivyoonekana..

Kama binadamu unahitaji amani, furaha, upendo na utulivu...hivi vitu havipatini kwa kijihangaisha na kupambana, havionekani na havipimiki.

Ndio maana ukishapata pesa na umaarufu nakila unachokihitaji utagundua huna nguvu juu ya vitu ambavyo havionekani na ukishakuwa na kila kitu hofu ya kila mtu inakuja anapofikiria kifo na mwisho wake na sababu ya maisha na kupambana na kujituma...bila kuwa na jibu kwenye hayo huwez kuwa na amani..

Bila kumjua Mungu hamna aman ya ndani
 
Umeandika vitu vya msingi sana ila watu na imani zao hawezi kuelewa hii kitu. Ila mwisho umesema "dini zimetengenezwa na wachache wanaojua ukweli," ukweli ni kwamba hata wao hawajui chochote kuhusu Mungu, ni waliamua tu kutunga stori Kisha ili ziaminike kilazima wakasingizia ni maneno ya Mungu.
 
Well well well. Ninaomba utulivu wako kidogo.

1. Japo kua kila culture inaamini miungu yake lakini culture zote zina vitu vinavyofanana...
A. Maisha baada ya kifo kwa mfano wa mizimu na mababu
Kabla hujazaliwa maisha yako yalikuwa wapi?

Kama ulikuwa huna maisha kabla hujazaliwa, kwa nini unadhani utakuwa na maisha baada ya kifo?

Kwa nini usiwe na maisha kabla ya kuzaliwa ila uwe na maisha baada ya kifo?
B. Uwepo wa ulimwengu mwingine usioonekana kwa macho C. Kuwepo kwa viumbe wengine wasioonekana kwa macho.
Kama ulimwengu huo na viumbe hao havionekani kwa macho, Wewe uliviona wapi au nani aliyeona ulimwengu huo akajua upo?

1. Science pia haina uwezo wa kuprove kuwa Mungu hayupo.
Angalau kitu kinaweza kuthibitishika kipo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika na kuhisika.

Mungu huyo hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Haonekani, Hashikiki, Hasikiki wala haisiki.

Mungu huyo ni mawazo ya kufikirika tu, imaginations just an illusion. Hayupo katika uhalisia.
Kama Dunia na sayari haiwezekani vitokee kwa bahati tu, Hata huyo Mungu haiwezekani atokee kwa bahati tu.
Hujiulizi Mungu huyo kabla ya kuumba mbingu na Dunia alikuwa wapi?

Huko alikokuwa kulitoka wapi?
 
Amani, furaha na upendo hutamalaki tele pale kila mtu anapokuwa bize na mambo yake...
Haya maswala ya Mungu na miungu ndio yaliyotowesha amani, furaha na upendo
 
Umeuliza bila kusoma
 
Akili ni kama jua . Elimu ni kama mwezi . Akili ndio ilibuni elimu . Akili ni superior kuliko elimu .
Kama Akili ni superior kuliko elimu, Kwa nini ulienda shule kusoma?

Kwa nini akili ya mtoto inazaliwa haijui chochote mpaka ikue ipatiwe elimu?
 
Umeuliza bila kusoma
Nimesoma.

Ndio maana kupitia maelezo yako nimekuuliza hayo maswali ili utathmini kama kweli ulicho kiandika ni majibu yenye ukweli.

Au unafosi tu imani zako za huyo Mungu ziwe majibu?

Wewe mwenyewe umeshindwa na unashindwa kujiuliza huyo Mungu unayedai yupo, kabla ya kuumba mbingu na dunia alikuwa wapi?

Na huko alikokuwa kulitoka wapi?
 
Unadhani kama Mungu yupo atakua anahitaji kuprove chochote? Unafikiri atapata hasara yoyote au faida yoyote ukimheshimu au ukimjua? No.

Kama yupo na kama amefanya yote hawezi kuhitaji chochote kwetu, zaidi sana tunahitaji kutoka kwake
 
Mungu hapimwi katika vitu na Mazingira ya Kibinadamu,huwezi ona,kugusa au kusema namna fulani ndio kipimo cha kufanya yeye awepo au asiwepo hata hizi dini hizi majority of them hawaelewi concept ya Uungu
Yaani ni Mbumbumbu sababu wao wanajaribu kumtafuta Mungu out of them hawaelewi kua Uungu ni Asili yaani Nature
Ni hivi kila kitu kinachoexist katika Ulimwengu huu ikiwemo wao ndio MUNGU kama Asili maana huwezi tenganisha Uungu na vitu vyake yaani yeye ni chanzo cha vyote na haexist mahali popote ukamwona maana hata hapo popote ni yeye mwenyewe,
GOD is everything dat exist,
Yaani kila kitu ni Mungu na Mungu ndio kila kitu,

Dini na mafundisho yake toka kale yalipokea tofauti kuhusu Uungu wakidhani yeye ni extra kumbe ni Intra

Aliyekuja kufunua siri ya Uungu ni Master Yashua Amashiach Mnazarene (Jesus Christ)
Yeye ndie pekee aliyefunua siri ya Uungu kwamba yeye ni Mwana wa Mungu yaani Uungu usioonekana ndie yeye katika mwili (code 1)
Na anaenda mbali kia kila mtu Mungu yupo ndani yake ni wewe kukubaliana na anachokisema na ukatambua itakuafanya uamshe Roho Mtakatifu (Mungu ndani Yako)
Na kufanya kuwa sehemu yake (code 2)

Kwamba wewe ndie Mungu na kila kitu kinachokuzunguka kiliumbwa ukitawale sababu wewe ndie muumbaji wa vyote
(man is fresh and spirit)
Yaani kabla hujawa mwili ulikua Roho na katika Roho ulikua mmoja na Mungu (Katika Asili)

Hivyo katika Ulimwengu wa Roho Bwana
Yashua Amashiach
(Jesus Christ) ndie mzaliwa wa kwanza wa Mungu maana yeye ndie aliyekua wa kwanza kujua siri ya Uungu na kutufunulia Wanadamu hivyo yeye na ile Asili vilikua kwanza kushikana na huwezi vitenganisha kwa sababu ni kitu kimoja katika Mazingira tofauti,

Ukitambua hii siri ya Uungu na ukifanya kile Neno la Yesu limekuagiza ufuate na ukitambua inafungua milango ya wewe kuzaliwa mara ya pili
(kuingia katika Ulimwengu wa Roho)
Na hapo unaenda kua Immortal!

Nitaendelea siku nyingine kukufunulia siri ya Uungu!
Siri ambazo religion never tell you because of ignorance and lack of truth!
Accumen Mo Saad30
 
Unadhani kama Mungu yupo atakua anahitaji kuprove chochote? Unafikiri atapata hasara yoyote au faida yoyote ukimheshimu au ukimjua? No.

Kama yupo na kama amefanya yote hawezi kuhitaji chochote kwetu, zaidi sana tunahitaji kutoka kwake
Hatuhitaji chochote kutoka kwa huyo Mungu kwa vile Hayupo kutoa chochote.

Kwanza huyo Mungu hayupo kujiongelea mwenyewe ndio maana unahangaika sana kumuongelea na kumuelezea kwa vile hawezi kujidhihirisha wala kujiongelea mwenyewe.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…