Yes, na huu ni mfano tosha wa jinsi tabia na personality zetu zilivyongumu kubadilika. Nafikiri mnakumbuka kauli iliyomfanya mama kumweka benchi akizani huyu jamaa atajifunza.
Waswahili wanasema ngoma ikivuma sana hupasuka,jamaa kajiona juu baada ya baadhi ya kauli zake kubebwa kwenye social media, sasa kajaa kiburi, kajaa majivuno mpaka anafikia hatua ya kuropoka, sawa kuropka ni shida ila linakuwa tatizo kubwa sana tena sana pale unaporopoka kwenye sehemu sensitive, sehemu inayohusu maisha ya mama na mtoto. Kibaya sababu aliyotoa ni ya kitoto kabisa na hana huhakika.
Unajua hawa voingozi wanalipiwa bills zote (utilities); nyumba, mafuta, umeme na wengine mpaka chakula, kwa hiyo hawajui hustle tunayopitia sisi wananchi wa chini, Oh!! kuna siku tunasepa na mchana, kula ni usiku baada ya breakfast ya asubuhi viazi vya kukaanga, maharage na chai ya rangi ;yeye anasema tunaspend kwenye vigodoro. Shabash.