Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Kuna bodaboda anapata 20000,unadhani akifanya kazi 3 years atakua na Tsh. ngapi?
At the end of the day,utashangaa anakua na bodaboda hata 6 na zote anaajiri watu,yeye anaendelea na maisha kama kawaida,aisee pamoja na kutokua na security ya matibabu,ajira n.k,baadhi wanapata hela,humfananishi na Mtumishi,anayechukua mshahara wa Daraja A au B.
 
Ah hapa tumeelewana , kumbe unakubali kuwa akifanikiwa anahama from bodaboda kwenda kwenye hiace, sasa mimi nafanya kilimo nikifanikiwa sihami kwenye kilimo Bali naongeza kuwekeza huko, na kuongeza biashara nyingine
Khaaa wewe πŸ˜‚πŸ˜‚

Anachokifanya boda kiko ndani ya biashara ya usafirishaji.. ndani ya biashara hiyo kuna boda, tax, uber, inDriver, hiace, canter, malori, virikuu.
What’s matter ni Enough capital ambao hata weee ukiupata huko kwenye kilimo utaanza kulima kitaalamu likely uwe na tractors, acres za kutosha, masoko, pembejeo, mbegu bora na madawa.
 
Kipato cha boda boda ni kikubwa kuliko ajira nyingi za serikalini na private kila siku boda boda anapata kati ya 30k kwa 50k kwa mwezi ni 900k kwa 1.5m hamna makato au Paye, niambie graduate wangapi wanapokea hicho kiasi kama net take home ............na boda boda inako elekea vijana wa sio jielewa wata kosa wateja hamna abilia anae penda kusafiri na dereva mvuta bangi au mlevi
 
Kuna mvuvi mmoja na mwanae tukienda kurusha nyavu wanaoga waziwazi wanaangaliana matango yao.
Kuna mbaba mmoja na kijana wake wote wanapark kijiwe kimoja, sijui wana handle vipi matusi ya vijiweni
 
watumishi wa serikali ndo wanaongoza kukopa kwa mangi walipe mwisho wa mwezi mshahara ukitoka.

Unasema una guarantee ya kukopa hela nyingi kwa vile una ajira ya kudumu,mbona mtaani mmejaa stress za mikopo.
 
Ila watanzania tuna shida mahali

Ulitaka mkute benki anahudumia wateja?

Je bodaboda siyo Kaz halali nchi hii?

Je ulitaka akae nyumban TU?

Je wale wazee wa umri wa miaka 50-60 wanaoendesha magari nao unawaonaje?

KAZI ULIYONAYO LEO KESHO UNAWEZA USIWE NAYO HUIJUI KESHO YAKO UTATAMANI HATA KUBEBA ZEGE

kifupi nakuona kijana unayewaza leo bila kujua KESHO yako

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo bodaboda ni biashara ya usafirishaji,Mimi nimefanya kazi ya bodaboda as mmiliki wa pikipiki, kipindi nawapa vijana chombo kwa mkataba kipindi hicho ilikuwa ni 10000 per day, anakulipa hiyo mwaka mzima, then pikipiki inakuwa yake , na nashukuru zilinisaidia sana kufungua mashamba yangu mapya ya parachichi,so sipondi bodaboda ila nakiona ni kitu kisichokuwa na future, hivyo ukiwa kijana fanya kutafta unafuu then shift kwenda kwingine, ila kwa mzee jua ni salamu kuwa kidingi kimepoteana, nazani bodaboda inabidi ifanywe ni vijana chini ya miaka 25
 
Mtumishi mwenzio huyo.. anatunanga tusio watumishi wa hazina.
 
Of course wazee wanaondesha daladala, malori nk kwenye umri huo ni sign ya kupoteana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…