Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Inashangaza,

Kazi haina job security, risks na athari za kiafya nyingi.

Mimi kwa upande wa si kwamba naidharau ila naona ni kazi ambayo mtu anafanya baada ya kukosa options.

Umetoa mada nzuri, sema wachangiaji sijui ni kukosa uelewa, au ni unafiki tuu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Halafu wengine kama FRANCIS DA DON nilichogundua kanunua bodaboda zake anawatumikisha vijana, na hapa kaja kuwatetea.
Anasema bodaboda anajenga mjengo unamwingizia kodi ambayo huigeuza pension
 
Kazi gani inaweza kukusaidia kujikinga na kifo kisikupate muda wowote?
Ndugu kuna kifo cha kawaida na kifo kinachosababishwa na mazingira yako ya kazi.
Umewahi kusikia madaktari wangapi wamekufa kutokana na kazi zao at the point?
Walimu, manesi, wahandisi?
Kama imetokea, je, kwa % ngapi?
 
Ndugu kuna kifo cha kawaida na kifo kinachosababishwa na mazingira yako ya kazi.
Umewahi kusikia madaktari wangapi wamekufa kutokana na kazi zao at the point?
Walimu, manesi, wahandisi?
Kama imetokea, je, kwa % ngapi?
Kuna watu wanafia usingizini, vipi hao nao?
 
Mleta mada hoja yako ingekuwa bora zaidi kama ungeegemeza mjadala kwenye mazingira ya kazi ya bodaboda na umri. Kwa mfano, wachezaji mpira kuna umri ukifika uwezo na ufanisi wao hupungua sana. Askari nao umri fulani ukifika kabla ya ule wa kustaafu hawapangiwi kazi za field.

Kwa mantiki hiyo mtu wa miaka 50> inakuwa tabu kwake kuendelea na kazi za mchakamchaka kama za bodaboda. Inabidi aanze kufikiria shughuli mbadala zisizosulubu mwili sana. Kipato kipo lakini sharti kiendane na uzima endelevu wa mhusika.
 
Huwezi kumlinganisha bodaboda na mtumishi wa umma kwa namna yoyote ile labda mtumishi wa umma mlevi.
Mimi ninadhaminika, naweza kupata milioni zaidi ya kumi bila barua ya udhamini kutoka kwa mwenyekiti.
Mimi nikiugua hata miezi kadhaa nitaendelea kulamba mshahara na posho , natibiwa kwa bima n.k
Nyumba yangu sijawahi kumuona bodaboda mwenye nyumba kama yangu.
Acheni ujinga, bodaboda ni last option
Jifunze kusema kibanda Kama watu wa pwani, ukisema nyumba utaambiwa unamalingo, kujimwambafai msemo wa waukae.
 
Hao unao wanaona ni wastaafu ambao wamejiajiri ili wasipoteze nguvu ya mwili.

Ukiwa mkubwa na hauna pesa basi utadharaulika sana
 
Habari!

Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.

Najiuliza maswali yafuatayo;

1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?

NJE YA MADA

Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
Mkuu Sandali Ali; Nakushauri urekebishe kwanza kauli kwamba mtu mzima kayumba Ukubwani. Sio hivyo hata kidogo. Kama anaimudu shughuli hiyo na kwa ufanisi hoja ya kayumba ukubwani haina mashiko hata kidogo.
Hoja kwamba ataifanya hiyo kazi mpaka lini ni yeye atakapoona basi imetosha au haiwezi tena. Naomba nikuulize kidogo; Bodaboda vijana wataifanya kazi hiyo mpaka lini huku wakiendesha bila kuzingatia Sheria za barabarani, wakibugia ze Kick na moEnergy bila kusahau lile jani pendwa na mwendo kasi vile??? (tumezika wangapi na ww ni shahidi). Kwa ni Mpaka lini jibu ni Popote pale kadri atakavyo jaliwa.
Kama unadhani utayumba uzeeni basi kama ww ni bodaboda fanya hivi:
1.Epuka kuendesha pikipiki kwa mwendo/mafuta mengi eti Umalize kisahani(Speed limit 140 km/h
2. Acha kabisa mbwembwe uwapo barabarani au hata unapokuwa kijiweni. Zingatia matumizi ya Indicators na upigaji honi bila sababu eti unastua abiria mtarajiwa.
3.Acha unywaji/matumizi ya kilevi uwapo kazini- heshimu hiyo kazi yako( hiyo Ndio Ofisi yako mjomba.)
4. Jiepushe na au punguza kufukuzia na matumizi ya hovyo kwa mademu. Kumbuka hakuna mashindano mwisho wa siku eti ni nani alitembeza rungu zaidi. Ni ujinga uliokubuhu na umewaponza wengi si vijana si wazee.
5. Waheshimu sana abiria wako ukizingatia kwamba hao ndo Waajiri wako/Matajiri wako- ndio wanaokupa pesa. Abiria akikwambia e.g. usikimbie, Tii amri hiyo chap! Bila shuruti.
6. Kuwa nadhifu na msafi muda wote na kuwa na nidhamu - acha lugha za kihuni-huni au matusi hata kama ni kijiweni.(kwani usipotema cheche za matusi utaacha kuitwa Boda?)
7. Hakikisha chombo chako kipo vizuri, imara na mafuta yapo ya kutosha kwenda na kurudi kwa safari uliyopewa na Usi-overload.
NB: Inaonekana vijana kazi hiyo mnazembea ndo maana Wazee wanaingia kati ili kuwafundisha mnachotakiwa kufanya. Hiyo kazi sio lazima ukavunjike miguu, kupasuke kichwa au kupata ulemavu wa kudumu. Ikitokea basi iwe ni ajali kama ajali zingine.
Mwisho bodaboda usijiingize kwenye kazi isiyo halali(Haramu) e.g. Kusafirisha madawa ya kulevya, Nyara za Serikali, Wizi na Ujambazi au Usafirishaji wa Wahamiaji Haramu n.k.
Ni hayo tu Mkuu. Nawapenda sana Bodaboda....😂😂
 
Kuna mbaba mmoja na kijana wake wote wanapark kijiwe kimoja, sijui wana handle vipi matusi ya vijiweni
Mbona Kuna wanasiasa pia unakuta wote Ni wafamilia moja na wanasongesha tu maisha Pamoja na changakoto za Siasa
 
Kwani ukiendesha boda boda ndio umeyumba kimaisha ? ni kazi kama kazi nyingine cha umuhimu anapata hela ya mahitaji yake
Mtu anaweza akawa ameingiza kiinua mgongo million kadhaa wakati anatafakari namna ya kuzitumia anaamua kuchukua bodaboda apate za kula na matumizi mengine huku akitafakari namna ya kuziwekeza milioni zake
 
Kama bodaboda wangelipia kodi kama wasafirishaji wengine,
Hii inchi ingeingiza hela sana,
Hela ndefu inapotea pale
 
Habari!

Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.

Najiuliza maswali yafuatayo;

1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?

NJE YA MADA

Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
mshahara wa professinal Tanzania analipwa un professional hapo kenya tu. tuendelee kuvaa tshirt siku za may mosi
 
Kwahiyo nyinyi mnaosema bodaboda anamzidi mwalimu mshahara mnaweza washauri wadogo zenu waache ualimu waendeshe bodaboda?

Bodaboda ni kazi yenye mazingira magumu kwa mtu wa miaka zaidi ya 50. Changamoto ni nyingi pamoja na kwamba kuna kipato. Haitokaa itokee nimuone bodaboda wa umri huo niseme amefanikiwa maishani. Namuona looser kwa kiasi fulani. Wala simaanishi nina hela ila twende kwenye uhalisia.

Kati ya options zote zilizopo mtaani ukikutana na mtu ambaye alikuwa mtu mzima zaidi ya miaka 32 iliyopita leo hii career yake ni kuendesha bodaboda usitafune maneno. Kuna shida mahala kwenye kujipanga kwake
 
Kuna mzee mmoja yule ako na 50s Kama sikosei..yeye na vijana wake watatu wote bodaboda miaka nenda Rudi..dah
Vipi na wee mke mtarajiwa nikununulie boxer tupige kazi pamoja
 
Back
Top Bottom