Habari!
Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.
Najiuliza maswali yafuatayo;
1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?
NJE YA MADA
Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
Mkuu
Sandali Ali; Nakushauri urekebishe kwanza kauli kwamba mtu mzima kayumba Ukubwani. Sio hivyo hata kidogo. Kama anaimudu shughuli hiyo na kwa ufanisi hoja ya kayumba ukubwani haina mashiko hata kidogo.
Hoja kwamba ataifanya hiyo kazi mpaka lini ni yeye atakapoona basi imetosha au haiwezi tena. Naomba nikuulize kidogo; Bodaboda vijana wataifanya kazi hiyo mpaka lini huku wakiendesha bila kuzingatia Sheria za barabarani, wakibugia ze Kick na moEnergy bila kusahau lile jani pendwa na mwendo kasi vile??? (
tumezika wangapi na ww ni shahidi). Kwa
ni Mpaka lini jibu ni Popote pale kadri atakavyo jaliwa.
Kama unadhani utayumba uzeeni basi kama ww ni bodaboda fanya hivi:
1.Epuka kuendesha pikipiki kwa mwendo/mafuta mengi eti Umalize kisahani(Speed limit 140 km/h
2. Acha kabisa mbwembwe uwapo barabarani au hata unapokuwa kijiweni. Zingatia matumizi ya Indicators na upigaji honi bila sababu eti unastua abiria mtarajiwa.
3.Acha unywaji/matumizi ya kilevi uwapo kazini- heshimu hiyo kazi yako( hiyo Ndio Ofisi yako mjomba.)
4. Jiepushe na au punguza kufukuzia na matumizi ya hovyo kwa mademu. Kumbuka hakuna mashindano mwisho wa siku eti ni nani alitembeza rungu zaidi. Ni ujinga uliokubuhu na umewaponza wengi si vijana si wazee.
5. Waheshimu sana abiria wako ukizingatia kwamba hao ndo Waajiri wako/Matajiri wako- ndio wanaokupa pesa. Abiria akikwambia e.g. usikimbie, Tii amri hiyo chap! Bila shuruti.
6. Kuwa nadhifu na msafi muda wote na kuwa na nidhamu - acha lugha za kihuni-huni au matusi hata kama ni kijiweni.(kwani usipotema cheche za matusi utaacha kuitwa Boda?)
7. Hakikisha chombo chako kipo vizuri, imara na mafuta yapo ya kutosha
kwenda na kurudi kwa safari uliyopewa na Usi-overload.
NB: Inaonekana vijana kazi hiyo mnazembea ndo maana Wazee wanaingia kati ili kuwafundisha mnachotakiwa kufanya. Hiyo kazi sio lazima ukavunjike miguu, kupasuke kichwa au kupata ulemavu wa kudumu. Ikitokea basi iwe ni ajali kama ajali zingine.
Mwisho bodaboda usijiingize kwenye kazi isiyo halali(
Haramu) e.g. Kusafirisha madawa ya kulevya, Nyara za Serikali, Wizi na Ujambazi au Usafirishaji wa Wahamiaji Haramu n.k.
Ni hayo tu Mkuu. Nawapenda sana Bodaboda....😂😂