Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Kuibuka kwa bodaboda wazee, kijana unajifunza nini?

Kama hajaja kukulilia shida hata siku moja mwache na Maisha yake, nawewe ishi yako.
 
Kipato cha boda boda ni kikubwa kuliko ajira nyingi za serikalini na private kila siku boda boda anapata kati ya 30k kwa 50k kwa mwezi ni 900k kwa 1.5m hamna makato au Paye, niambie graduate wangapi wanapokea hicho kiasi kama net take home ............na boda boda inako elekea vijana wa sio jielewa wata kosa wateja hamna abilia anae penda kusafiri na dereva mvuta bangi au mlevi
Bodaboda hawahawa wanyoa viduku na Kula viroba ASUbuh
 
Dunia tambara bovu. Aliekuwa Mkuu wa shule sasa ni boda boda baada ya kutumbuliwa na Jiwe.

Aliekuwa Mayor wa Jiji la Dar nae anauza Mayai.

chunga sana ishi vizuri na walimwengu
 
Kuna mzee mmoja yule ako na 50s Kama sikosei..yeye na vijana wake watatu wote bodaboda miaka nenda Rudi..dah
Na hawajawahi kumuomba mtu support!! Tuache kudharau Kazi za watu, by the way matumizi mengi ya surplus money ni pamoja na michango mingi ya kijamii, ukijitenga nayo mbona Kipato Cha bodaboda kinatosha kabisa kuendesha maisha ya Raha Mustarehe!!!
 
Laiti ungejua bodaboda anaingiza sio chini ya 15 kwa siku baada ya 15 ya tajiri na mafuta, basi usingeongea huu utumbo wako wa kusema mtunameyumba maisha.

Sasa Kama mtu ananunua boda kwa milioni mbili na nusu, na akaendesha mwenyewe Ina maana kwa mwezi ana uhakika wa kuingiza so chini ya laki Tisa ukitoa matengenezo madogo labda laki Saba na nusu au Saba utamfananisha na mwalimu wako?

Hapo anafanya kazi kwa masaa kadhaa hana pressure ya kusaini kitabu Cha maudhurio na anapata misosi yake Kama kawaida na bia nne jioni anakunywa.

Hii dharau ya vitoto vidogo ndio mnakuja kukosa kazi wakati zipo tu. Nimemnunulia dogo wa brazangu pikipiki kaishia kuiharibu na hesabu haleti wakati tulikubaliana baada ya miezi 18 pikipiki itakuwa yake .

Na akaacha kuendesha nae akampa kijana mwingine awe anaendesha ampe hesabu, nimenyang'anya natamani hata mie ingekuwa Sina kazi ningeendesha.

Nimepeleka bush ikae shambani tu, vijana wanadhani kukaa kwenye AC ndio umefanikiwa sana, Kuna watu wanalala mashambani mtu ana heka 1000 analima anakaa msimu mzima shamba akitokea mjini anauza mazao anaweka kibindoni sio chini ya milioni 400 na anarudi zake porini kuandaa shamba upya kwa msimu ujao , Sasa kamtembelee shambani ndio utamjua ana nini.

Unakuta jamaa anaendesha landrover Ila shambani ana trekta za kulima John Deere tractor Kama sita na harvester za kutosha ukipiga hesabu utatamani kulima Ila ndio kilimo hakihitaji uvamie .
 
Hao wana hela Sana
Kuna dogo ngosha anakesha usiku anakwambia mpaka asubuhi ana 40,000 tatizo Starehe.
Ujinga wa vijana wengi wa boda ni kama walivyo wachimbaji madini Yani wanaamini mgodi upo tu. Same as boda anaamini boda zipo tu .

Wanajisahau sana wanapeleka pesa kwenye umalaya na pombe mwisho wa siku wanakuwa addicted au wanapata magonjwa na inakuwa mwisho if not ajali au ulemavu.
 
Bodaboda si kama kazi nyingine.
Na ni ujinga kulinganisha bodaboda na ualimu au udaktari, hizi ni noble professions.

Bodaboda linganisha na Machinga na Mamantilie huko.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna Bodaboda ambaye ni mwalimu ?

Tatizo sio hivi nguvu kazi bali ni jamii / demand and supply kutokuona umuhimu / uhitaji wa hizo profession kwahio mwisho wa siku ili mkono uende kinywani its all about putting bacon on the table....
 
Kwamba ulitaka afanye shughuli gani mkuu? Au alipaswa akae tu au alitakiwa awe na kampuni labda?
 
Habari!

Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.

Najiuliza maswali yafuatayo;

1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?

NJE YA MADA

Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
FB_IMG_1651836350811.jpg
 
Wengine ni wale ambao enzi za ujana wao hawakuwa na proffession yeyote hivyo anazeeka bila kuwa na maandalizi yeyote.
 
Habari!

Binafsi ninapomwona bodaboda mtu mzima mwenye miaka 50-60 napata mshituko kidogo na kuanza kuiogopa kesho yangu.

Najiuliza maswali yafuatayo;

1. Kayumba ukumbwani mpaka kaamua kuingia kwenye kazi za vijana wanaoishi vijiweni kutwakutwa kwa utani na matusi?
2. Atafanya hiyo kazi mpaka lini, na siku akiacha ataenda kufanya kazi gani?
3. Je, Mimi nikiyumba uzeeni nitafanya kazi gani?

NJE YA MADA

Vijana tijifunze kuwekeza kwenye shughuli ambazo zitaleta matunda baadaye na si kuangalia leo tu.
It's a good thing but with mixed interpretations
 
Back
Top Bottom