Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Fanya ujinga wote na ujuaji wote , lakni swala la kujenga halipingiki , tena Jenga mapema kabisa iwezekanavyo ,
 
Waajiriwa tunawaza kujenga na kununua gari tu. Hapo tunaona malengo tumetimiza...then tunasubir kufa.. watoto watapambana wenyewe kivyao
Uko sahihi. Ukihesabu pesa inayopita mkononi mwa waajiriwa halafu tunastaafu kwa nyumba na gari na makelele mengi eti watoto wetu hawana ajira ni umbumbumbu. Kama wazee wetu walishakosea inabidi kizazi hiki kibadilike kitambue asset (vitegauchumi) ni nini na liability ni nini.
 
Ni kweli,ingekua rahisi hivo ukiwekeza unapata wafanyabiashara kariakoo wasingekua wanalia vile km ni rahisi

Mtu akipata pa kuhifadhi familia kwanza inasaidia kupata akili ya Mambo mengine
Tatizo ni pale unapomaliza kujenga geto kali la 25M na kibarua kikaota nyasi wakati mwenzako alitumia 10M kununua ekari 5 na kufuga mbuzi/ kondoo/kitimoto halafu na yeye kibarua kikaota nyasi. Kuna mtu atalia kimoyomoyo ila kuna mwingime atapiga yowe.
 
Yaani ndugu una akili kubwa sana na unaona mbali sana.
Huu ndo uwekezaji sasa, kamwe huwezi juta.
 
Yaani acha tu, akili zetu naona kama haziangalii mbali. Tuna shidwa kuwekeza ili vizazi vijavyo viendeleze uwekezaji na kujikwamua kwenye uchumi hapo baadae, tunaendekeza kuridhika na nyumba na gari.

Ukimuangalia MO na baadhi ya matajiri wengine, utaona kuwa utajiri wao sio wa siku moja, walisha anzishiwa misingi na wazazi wao mda mrefu, wao wanaendeleza na kuitanua zaidi.
 
Fanya ujinga wote na ujuaji wote , lakni swala la kujenga halipingiki , tena Jenga mapema kabisa iwezekanavyo ,
Hatujakataa ila jenga ukiwa umeshafanya uwekezaji wa kutosha. Mfano umeajiriwa, umechukuwa mkopo na ukajenga au umejichanga kwa miaka 5-10 ukajenga baada ya kumaliza kazi au kuachichwa kazi lazima tu hiyo nyumba utaiuza/kuikopea mkopo ujikimu, mwisho wa siku maisha yako yanakuwa yanarudi pale pale kwenye hali ya utumwa.

Kujenga siyo kwamba umemaliza matizo yote ila unajenga na akiba unakiasi gani, je hiyo akiba inajizalisha au inasubiri itokee tatizo itumike, tujitafakari lakini ndugu zangu.
 
Ardhi huwa haiongezeki thamani ila pesa hupungua thamani tu.

Kiwanja tupu siyo uwekezaji ni kutupa hela kwa mategemeo ya kuiokota baadae.

Kununua ardhi bila kuiboresha na kuwa chanzo cha pesa ni sawa na kumkopesha hela mtu asiye na uwezo wa kulipa.
Unaweza ukasema hivyo ndugu lakini kuna watu walinunua mashamba mvuti, msongola na maeneo mengine miaka 5 - 8 iliyopita wakati huo ilikuwa poli, lakini huwezi kuamini leo hii mashamba hayo yalikatwa katwa vipande vidogo vidogo, kila kipande Milioni 2.5, mtu anaheka zake tatu kila heka katowa vipande 8 na kila heka moja aliinunua laki 1, leo hii kapata faida nyingi sana.

Baadhi ya viongozi duniani wanawekeza sana kwenye ardhi, si kwamba wajinga ila wanajuwa kibaruwa kikiota nyasi basi ardhi itakuwa suluhisho la kusonga mbele.

Tunatolea mfano ardhi kwa sababu unaweza kufanyia mambo mengi, unaweza usiize ila ukawa unalima mihogo, karanga, kufugia na n.k, pia ni uwekezaji.
 
Hili nilishaliona kitambo, nikalifanyia kazi.
 
Kuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.

Ardhi haipandi thamani bila kuboreshwa bali kinachotokea ni pesa kushuka thamani tu.
 
Umesema vyema sana
 
Kuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.

Ardhi haipandi thamani bila kuboreshwa bali kinachotokea ni pesa kushuka thamani tu.
Kuwekeza kwenye siyo kununua ardhi pekee mpaka ardhi husika iboreshwe ndiyo utakuwa uwekezaji.

Ardhi haipandi thamani bila kuboreshwa bali kinachotokea ni pesa kushuka thamani tu.
..mkuu upo sahihi kama umenunua maeneo yanayochelewa..lakini tumeshuhudia watu wakiuza plots zaidi ya 2B kariakoo miaka ya karibuni ambayo ilikuwa kwa miaka ya 1990 walinunua kwa malaki tu...maeneo kama mbweni miaka ya 2000 yalikuwa mapori watu wakinunua kwa 1-2m ila leo kiwanja kinaenda hadi 250m....so ni kununua maeneo ambayo unaona kuna potential inakuja ndani ya 10yrs lazima upate faida kubwa sana kwenye ardhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…