Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Kama hauna familia sawa anza kufanyabiashara ila kwa wakina sisi tulioanzaga mchezo mbaya mapema tulijikuta tupo chuo mwaka wa pili tu tayari tuna mke na mtoto.
Hadi unakuja kupata kazi unajikuta familia inakuforce uwe na nyumba ukicheki kupanga nyumba nzima ni gharama sana inakubidi uanze kujenga maana kuishi kwenye chumba na sebule ni udhalili.
Nakumbuka nilijimeki within 6months nikanunua plot, kisha tukafunga mkanda kuanza ujenzi ilikuwa kila mwisho wa mwezi naenda kulipia tofali hardware to make story short.
Ndani ya miaka mitatu mfululizo nilikuwa nishamaliza boma kupaua na fence kusema kweli baada ya kupachika grills plasta na floor nilihamia kwangu mambo ya finishing nilifanya nikiwa humohumo maana nilijiapizaga kuwa sitaki kuanza kusomesha hukunikiwa nyumba ya kupanga.
Ushauri kwa vijana kujenga sio matumizi ya hovyo ya pesa maana nyumba ni pumziko, heshima, utulivu, kituo cha kudumu cha familia yako, kitunza dhiki na shida zako.
Mwenye macho na aone na mwenye masikio asikie😊
 
Hizi principles za kuwekeza kwenye bonds na vipande vya UTT nimezisikia tangia 2003., nikiwa graduate tayari Kabla ya hapo sikuzijua. Lakini sijawahi zifuata. Ila mleta mada namsapoti lakini dah ni ngumu kuzitekeleza ktk umri mkubwa na majukumu mengi. Nashauri vijana mzifuate. Jambo baya ninaliliona ktk jamii zetu ni watu kujenga kwa kutafuta misifa. Kuna sababu gani kijana ndio umeoa au kuolewa, mtoto wenu ndo ana umri chini ya mwaka. Unajenga nyumba ya vyumba vitatu au vinne vyote self na servant quarter! Compound nzima inagharimu Mio kama TZs 80! Wakati Kipato chako kinakuwezesha kulipa kodi ya TZS 150 kwa mwezi? Ukiangalia hiyo compound ukataka kuikodisha, gharama yake ya pango ni TZS 500,000 hadi TZS 600,000 kwa mwezi! Kwa nini usijenge nyumba inayolingana na uwezo wako wa kulipa kodi, hiyo nyingine ukawekeza ktk ardhi?
 
Unapojenga nyumba faida yake na umuhimu wake utakuja kuuona miaka kadhaa mbele usipigie hesabu za leo.
Kwa mfano sasa hivi kwa vile una mtoto mmoja mdogo kwa hiyo haitakiwi kujenga nyumba kubwa?lakini kumbuka baada ya miaka 10 huyo mtoto atakuwa anakaribia miaka 15 na atakuwa na wadogo zake wawili kwa hiyo ukiwa na nyumba kubwa haitakupa stress ya kuanza kujenga upya nyumba nyingine na pesa utakayokuwa unaipata utaamua ufanyie miradi gani.
Pili umesema kwa vile unafanya kazi na una uwezo wa kulipa kodi ya laki 2 kujenga hakuna umuhimu?Kumbuka hiyo kazi unayofanya sasa hautafanya milele kuna kufukuzwa kazi,kuna kuugua,kuna ajali so haya yakitokea kazini watakuchoka na kukuachisha kazi na pia vile vile baba mwenye nyumba atakuchoka pia maana anahitaji kodi yake na wewe uwezo wa kulipa hautakuwa nao.
Lakini ukiwa na nyumba yako itakusitiri hata kama uko jobless mke wako anaweza kuanzisha kibiashara kidogo tu nyumbani kwako hata cha kuuza barafu na Ice cream mnapata hela ya kula maisha yanasonga.
 
Unatak tushindee balaaa na Kulaaa mbunyeeee...!!
 
Kukopa niwew tubkulipa unaweza lipa ata mkopo wako miaka 20 hasa kwa wafanya kazi si kuna dada alikopaga 40m kumbe alimkopea ki ben ten chake kilivopewa mkwanja kikapenya kijamaa na mzigo wote dada bado analipaga tu mwaka wa saba huu
 
Ukikopa mil 100, ukaiweka UTT , baada ya miaka 5 unakua na zaidi ya mil 300. lakini ukijenga nyumba ya mil 100 baada ya miaka 3 nyumba hiyo itakua na dhamani ha mil 50
wewe mtu emu muogope mungu mfuko gani wa UTT Amis unatoa return kubwa kiasi hiko................
 
hizo tunaita rat Race.... tafuta kazi oa chukua mkopo jenga chukua mkopo nunua gari anza kulipa mikopo yako ..ukiimaliza watoto washakuwa anza kulipa ada....lipwa kiinua mgongo kufa baada ya miaka mitano
Na pia watoto na wao waanze kujitafuta kivyao...hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu. Ndo maana ni vigumu sana kuvunja Generational Poverty cycle.,umaskini unarithishwa kizazi hadi kizazi. unless tuanze kubadili Mindset zetu.
 
kwanini usimshauri aipangishe?
 
Na hapa ndipo vijana tunapopotelea. Kuna intake yangu wamekopa pesa bank wakaenda kujenga, unakuta 30 milion inakata na nyumba haijaisha wakati huohuo mshahara unakatwa, anaishi kwa madeni.
 
Na hapa ndipo vijana tunapopotelea. Kuna intake yangu wamekopa pesa bank wakaenda kujenga, unakuta 30 milion inakata na nyumba haijaisha wakati huohuo mshahara unakatwa, anaishi kwa madeni.
kwa ujenzi wa sasa ,30m ni ndogo sana ,hapo lazima waishi kwa madeni,angalau ukiwa hujatumia mkopo unaweza kujivuta kwa savings zako ukamalizia finishing taratibu.
 
Elimu nzr,umepita mulemule. Ila nipo pale nasubiri
 
Nmekuleta site kwangu uone hatua niliyofika umekuja kutangaza huku

Sasa elimu ya biashara sina ulitaka ifilisike uje kunicheka tena huku

DAH
πŸ˜€ πŸ˜€ ndio mana sipeleki rafiki site kwangu hata siku moja hata ndugu hawafiki seuse rafiki
 
πŸ˜€ πŸ˜€ ndio mana sipeleki rafiki site kwangu hata siku moja hata ndugu hawafiki seuse rafiki
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Yani mtu anaona biashara ni ya kila mtu anaweza kufanya tu
Yani nikose vyote biashara na makazi bora nibaki na hilo hilo boma
Kuliko kuja kuweka million 30 halafu niishie kutajirisha watu tu
Ashasema mtu anafanya kazi posta alitaka biashara isimamiweje
Kuna muda unaona bora tu ninune kiwanja nijenge kitakuja nistiri baadae.

Halafu vijamaa snitch kama hao unakuta anaandika andika JF na bado mkikutana anakulamba mzinga wa Bia. Jokes
 
Na pia watoto na wao waanze kujitafuta kivyao...hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu. Ndo maana ni vigumu sana kuvunja Generational Poverty cycle.,umaskini unarithishwa kizazi hadi kizazi. unless tuanze kubadili Mindset zetu.
naamini umaskini ni mind set... jamii nyuingi zina mdudu huyu kichwani ubinafsi ujinga unaoshindwa kujua which is which..aset and liability.... mtu anamaliza hela kwenye home housing anasota kukopa mtaji benk alipe kwa riba na ile nyumba imekuwa colateral...home housing is liability and no one agree...
 
Kabisa mkuu,nini kifanyike ili watu waanze kufikiri tofaut.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…