Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

Kujenga nyumba na kununua magari ni sababu mojawapo ya Umasikini

naamini umaskini ni mind set... jamii nyuingi zina mdudu huyu kichwani ubinafsi ujinga unaoshindwa kujua which is which..aset and liability.... mtu anamaliza hela kwenye home housing anasota kukopa mtaji benk alipe kwa riba na ile nyumba imekuwa colateral...home housing is liability and no one agree...
Assets [emoji117] Something that puts money in your pocket.
Liability [emoji117] Something that takes money out of your pocket.

But to keep in mind; Both assets and liabilities are economic concepts that are clearly stated. But, Info-prenueurs always gives their own perspectives.
 
Kua na kwako sitatizo ilawengi wanajenga iliwasifiwe na sio kukimbia kodi ili usave ujenge nyumba ya ndoto yako nakuweza wekeza mambo mengine hapa wengi ndio hukwama haiwezekani nyumba ya kwanza tu miaka 10 unajenga hio sio nyumba nimateso
 
Ardhi huwa haiongezeki thamani ila pesa hupungua thamani tu.

Kiwanja tupu siyo uwekezaji ni kutupa hela kwa mategemeo ya kuiokota baadae.

Kununua ardhi bila kuiboresha na kuwa chanzo cha pesa ni sawa na kumkopesha hela mtu asiye na uwezo wa kulipa.
Sure mkuu ardhi sio ya kuwekeza..km kichwan huna mkakati wa kuifanyia ....
 
Uzi murua sana huu. Nimechelewa tu kuuona. Nilichogundua kupitia comments wengi tunasumbuliwa na kukosa elimu ya biashara ndio maana wengi hawaoni kama swala zuri kutokujenga na kufanya uwekezaji.

Tukija kwenye uwekezaji kuna swala Risk Taking hapo ndio wengi hatuna ule moyo wa kurisk mitaji na muda wetu kwa ajili ya kufanya uwekezaji.
 
Na pia watoto na wao waanze kujitafuta kivyao...hili ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu. Ndo maana ni vigumu sana kuvunja Generational Poverty cycle.,umaskini unarithishwa kizazi hadi kizazi. unless tuanze kubadili Mindset zetu.
Sahihi kabisa
 
Haya ni mawazo nadharia yaani theoretical..

1. Hizo Mil 100 za kuweka UTT anapata wapi ??

2. Fine, umesema anakopa hizi Mil.100..Je, anapata wapi dhamana ya kukopa Mil.100??

3. Sawa, Akikopa Mil.100, anakuwa na jukumu la kurejesha riba around 15 ~ 18% kwa mwaka.Let's say ni 15%, hapo anakuwa analipa 2.3Mil rejesho (na hii ji kwa redusing balance). Rejesho hili linalipwa na hela ipi ??

4.ROI kwa UTT ni around 10~13% kwa mwaka na at best wanalipa semi annually..so miezi 6 unapewa 6,500,000.Hapo una marejesho ya around Mil.13.8 kwa kipindi hicho hicho..Ukikurupuka utajua hujui..

Anyway..hizi mambo ukiwa kwenye karatasi ni rahisi sababu ni theory tuu ila uhalisia unahitaji utoshelezi wa mapato na umakini wa hali ya juu sana...Kutoboa at minimum ni kuwa na njia mbadala za mapato zaidi ya 2.
Uko vizuri kichwani
 
Kupanda na kushuka katika maisha ni jambo lipo of course lipo na kujenga katika maisha katika nchi kama yetu hii ni muhimu Sana pindi unapo kuwa na Nafasi Ama katika swala la kuwa mtu akijenga amefanya jambo la hovyo hiyo sio kweli maana moja katika ya vitu vinavyo mtambulisha mtu kuwa anahali nzuri ya kiuchumi ni kumiliki vitu kama hivyo...

tatizo lililopo apa nikwamba asilimia kubwa ya watu wanaojenga na mwishoe uchumi wao kuzolota Nikwamba Hujenga ili niamie na kujitoa katika cheni ya kulipa kodi za nyumba hii dhana ndo shida kubwa lakini kama watu watakuwa na malengo ya kujenga nyumba kama asset katika maisha yake Hawezi kuwa na pupa za kumpelekea kuacha jambo la Leo ili apeleke kiasi kile site ilo kwake halitokuwepo kabisa...

Asset inakuwa ni future lakini ww chunguza mtu akiwa na ujenzi kwanza akikaa anawaza ujenzi yani mpaka Ile nyumba inaisha anakuwa ameshakuwa fundi [emoji23][emoji23] Lakini watu wa namna hiyo pia Ni katika malengo Yao makubwa yani wakati anajenga Hakuna anacho waza baada ya ujenzi ule ambacho atakuwa na pupa nacho kama swala lake la kujenga hivyo kila mmoja anafanikiwa kulingana na Ile image Nation yake ikigota kwenye kumiliki tuuy nyumba apo ndo basi

Nawasilisha.
Hii hali inasababishwa na nini mkuu..mtu kuwa na ndoto ya kumiliki nyumba na gari pekee..hapo anajiona kamaliza maisha..kinachofuata kubangaiza kusomesha watoto..halafu na wao wakibahatika kupata kazi wanapita njia ile ile ambayo baba yao alipita.
Hii inaitwa generational poverty Cycle.

Kuivunja inabidi ianzie kwenye mind,
 
Sure, but aaaah... Unajua hii hali kwa mtazamo wangu binafsi naona kuwa Ni janga katika Familia za kiswahili 90% tunazo tokea, maana Ata ukifikiria ww ku kutana na mzee wako siku moja kwa maana ya MZAZI wako (sorry kama ametangulia) alafu ukimshirikisha kuwa huku unawazo la biashara alafu huku unawaza kuanza ujenzi 85%atakuwa katika upande wa ujenzi fact zake oooh... ushakuwa mkubwa una Familia inakutazama na vitu kama hivyo kwaiyo kuondokana na iyo nature sio swala dogo inataka maandalizi ya muda mrefu kila mmoja Katika Familia yake.
Hakika mkuu. Hata maeneo yetu ambayo tunafanya kazi sijawahi kubahatika kukutana na mtumishi mwenzangu anaye waza tofauti na nyumba..ni nadra mnoo aisee.
Na point zao ni zile zile kwamba biashara ni hasara, kwamba unaweza fukuzwa kazi na hauna sehemu ya kuweka familia.

Watu watafute elimu za biashara na uwekezaji..

Mfano mtumishi anaweza chukua mkopo,pesa akawekeza katika hisa za kampuni ama UTT ama dhamana za serikali (government bonds). Ambako ni safe asilimia 100. Siyo lazima ufanye biashara za kubangaiza.

Watu hawana elimu
 
Nimenunua Tressury Bonds, na nimewekeza mfuko wa uwekezaji (UTTAMIS) faida milioni 1 na laki nne kila mwezi bado nipo kazini mshahara unalipa kodi ya nyumba nilikopanga, mafuta ya gari, vocha na chakula na hii faida ninayopata kwenye uwekezaji ndio naipeleka kujenga sina presha yaani maisha murua kabisa.
 
Umenunua bond za mil ngapi mpaka faida upate pesa hiyo kwa mwezi?
 
Umenunua bond za mil ngapi mpaka faida upate pesa hiyo kwa mwezi?
Nimenunua Treasury bond za milioni 104 na Bond fund ya UTT ya vipande vya Milioni 104, huku UTT natumiwa faida kila mwezi ile ya BOT natumiwa kila baada ya miezi 6 katika mwaka. chanzo cha fedha hizo zote niliuza shamba kubwa la miti iringa kwa wazungu walilitaka nimehamia dar ila nimepanga katikati ya mji.. mtoa mada yupo sahihi..
 
Habari,

"Tafuta kiwanja, Jenga, Oa/Olewa, nunua mkoko", njia hii na mawazo haya yamekuwa kwa vijana wengi wanaoanza maisha, hususani waliobarikiwa kupata ajira au biashara zao binafsi ambazo zinawapa kipato flani cha kuendesha maisha yao. Kwa uzoefu wangu hii imekuwa kati ya sababu moja kubwa zinazosababisha watu kuwa maskini na kushindwa kufikia uhuru wa kifedha.

Lakini tujiulize swali la msingi, kwanini watu wengi wameamua kuchagua njia hii ya maisha. Nimefanikiwa kuwahoji watu wengi kidogo kuhusu hili na majibu niliyoyapata mengi yalikuwa kama ifuatavyo:

  • Gharama ya kupanga nyumba ziko juu sana, ni bora kujenga ya kwako.
  • Nyumba ni asset.
  • Usafiri ni shida sana eneo niliko jenga ni bora kuvuta gari yangu.
  • Mama/baba mwenye nyumba ana gubu sana.
  • Nikiwa na kwangu nakuwa na uhuru mkubwa sana.
  • Siku nikifukuzwa kazi au biashara ikiyumba nibaki na pakulala na familia yangu.

Sababu hapo juu nyingi ni za maana kabisa ila tatizo ni kwamba njia zilizotumika kutatua hizo changamoto zinaongeza changamoto zaidi, kivipi?. Ngoja tujadili mambo machache kuhusiana na maisha ya watu wengi hususani mijini (e.g. Dar):

- Wengi wananunua viwanja maeneo ya mbali kutoka mahali wanapofanyia shughuli zao zinazowapa kipato.
- Baadhi ya hayo maeneo yana changamoto za miundombinu ya maji, umeme, barabara na hata kiusalama.
  • Wengi wanajenga kwa kuunga unga sana, unaweza jenga nyumba hata miaka sita au zaidi. Kuna msemo wanasema "nyumba haiishi".
  • Nyumba nyingi wanazojenga watu kukaa zinakuwa ni kubwa na za kifahari bila kukumbuka lengo la mwanzo lilikuwa ni makazi tu na sio jengo la maonesho (Hapo utajibiwa kuwa tunajenga mara moja ya kuzeekea)

Kuzingatia hizo hoja hapo juu, yafuatayo yanakuwa ni matokeo ya gharama za maisha baada ya huyu mtu kuhamia kwake:

  • Gharama za usafiri au mafuta zinakuwa juu ukilinganisha na awali.
  • Mazingira yanakuwa sio rafiki kwa familia kuishi, maana nyumba nyingi zinakuwa bado hazijaisha (Wengine wanasema unakuwa unaishi site).
  • Kama una gari, gharama za matengenezo zinakuwa juu kwa sababu ya pengine barabara kuwa mbaya, lakini kwa kuwa unasafiri umbali mrefu kila siku, basi hata service ya gari utafanya mara nyingi zaidi.
  • Pia kama una gari utalazimika kuendesha gari umbali mrefu kila siku, hii si nzuri kwako kiafya.
  • Gharama za umeme na maji pia zinaweza kuongezeka kwa kuwa nyumba ni kubwa sasa na pengine maji hayajafika.
  • Maeneo mengine hata watu hawajahamia wengi hivyo hata usalama unakuwa hatarini.
  • Mara nyingi unaweza ukajikuta mbali na huduma bora za kijamii ikiwemo hospitali, shule, n.k.

***NOTE: Gharama zinaweza kuongezeka ukilinganisha na mwanzo.

Kwanini kuna hofu ya kuwekeza hizo pesa?

Tujiulize swali hili la msingi. Ni kweli baadhi ya watu wanatamani sana kuffanya biashara, lakini wengi wanasema, BIASHARA HAZITABIRIKI. Ni kweli kabisa, lakini ukweli ni kwamba hilo sio tatizo la watu kutokuwekeza.
SHIDA KUBWA NI WATU KUTOKUWA NA ELIMU YA FEDHA. Hili ni jambo la muhimu sana kwa vijana kupata elimu. kwanza kabisa sio kweli kwamba ukitaka kuwekeza ni lazima ukafanye biashara fulani kama kuuza nguo, vinywaji au duka la mangi. Unaweza ukafanya uwekezaji kwa njia nyingi sana ambazo hazitahitaji your active time kuweza kusimamia ila mwisho wa siku ukaja kuwa na uchumi mkubwa kabisa. Uwekezaji huu ni kama mifano ifuatayo:

  • Kununua viwanja na mashamba (Kumba muda unavyokwenda ardhi inapanda thamani lakini nyumba inashuka thamani)
  • Kununua hisa za makampuni
  • Tressury Bonds and Bills
  • Mifuko ya uwekezaji ya pamoja (e.g. UTTAMIS)
  • Fixed deposits accounts
  • Kuwekeza kwenye elimu (Hii sio lazima zile za darasani, inaweza kuwa hata kujiendeleza katika fani flani)
  • N.k.

La muhimu ni kupata elimu sahihi ya mambo ya fedha ili ujue jinsi ya kufanya maamuzi ni vipi utumie pesa yako.

Ngoja nitoe mfano halisi mmoja ulio hai kabisa kwa lengo la kupata uhalisia wa ninacho kisema:

Mwaka 2013 niliajiriwa mahali na tulikuwa kama waajiriwa sita wapya katika hiyo kampuni, mwenzetu mmoja alikuwa na uelewa mkubwa sana wa mambo ya fedha, na mara nyingi alikuwa anatushauri kuhusu haya mambo lakini tulikuwa tunamuona kama kachanganyikiwa: Mimi na wenzangu wengine wa tano tulikwenda mahali tukanunua viwanja na kuanza kujenga kwa kasi sana na badae tukachuku na mikopo kuongeza kasi hiyo. Kwa haraka haraka kwa wastani tuliweza kutenga kama milioni moja kwa mwezi kila mmoja wetu kwa ajiri ya miradi ya ujenzi. Mungu si athumani baada ya miaka mitatu paka minne wote watano tukawa tumehamia kwenye site zetu huku tukiendelea na finishing.

Jamaa alikuwa kila mwezi anaweka milioni moja kwenye mfuko mmoja wa uwekezaji wa pamoja na alikuwa anapata average interest kama ya 11.85% kwa mwaka. Badae akawa ananunua na bond za serikali pamoja na mambo ya kununua mashamba mbali kidogo na mji yakichangamka anakata na kuyauza. Kiufupi jamaa ana zaidi ya milioni 200 kwenye mfuko anaoweka pesa pamoja na kuwa na asset ya viwanja na mashamba na benki ana pesa chafu.

Turudi kwetu tuliojenga na sasa tuna mikoko yetu, umbali wa kwenda na kurudi nyumbani ni 50 Km kila siku. Na pia siwezi pata picha ile hofu ya kwamba nikiachishwa kazi bado ipo maana siwezi nikala nyumba.

Kwa ajili ya muda niishie hapa kwa leo, nipate mawazo ya watu wengine pia. Kiufupi mimi naona kuna mitaji mingi ya biashara na uwekezaji inapotea kwa huu mwamvuli wa kujenga na kununua hii mikoko.

Ahsanteni!!!
Wewe jamaa una matatizo.
Matatizo yspo wapi nashindwa kueleza.
Bottom line, ukitaka kuokoa gharama za maisha, acha kuisi.
Cost zako zitakuwa zero.
 
Nimenunua Tressury Bonds, na nimewekeza mfuko wa uwekezaji (UTTAMIS) faida milioni 1 na laki nne kila mwezi bado nipo kazini mshahara unalipa kodi ya nyumba nilikopanga, mafuta ya gari, vocha na chakula na hii faida ninayopata kwenye uwekezaji ndio naipeleka kujenga sina presha yaani maisha murua kabisa.
Wewe ndo una akili mkuu. Huwa nashangaa kwa nini watu wengi hawana ufahamu wa haya mambo
 
Wewe ndo una akili mkuu. Huwa nashangaa kwa nini watu wengi hawana ufahamu wa haya mambo
Kweli mkuu Nilipopiga mshindo wa kuuza shamba langu la miti nikaona hapa nikikaa na hii pesa ntakufa mapema maana hata mahali nilipokuwepo usalama ulikuwa mdogo wahuni wangekuja kunidandia niwape mpunga
 
Familia ya Trump imetajirika kwa kujenga majumba, kujenga nyumba ya kuishi sio chanzo cha umaskini, hata matajiri kama Mo na bakheresa, GSM wote wanaishi, kwenye ma mansion ya kibabe,
Kinacholeta umaskini kwa watu weusi, au bongo ni kutokuwekeza, kutegemea ajira na mshahara kwa kila kitu, unasemaje kununua magari ni chanzo cha umaskini, wakati shabiby anamiriki mabasi zaidi ya 200+! Unaweza, ukawa na gari, ukitoka kqzini unapitia kwenye maduka yako kama 10 ya mpesa,stationary, unapitia kwenye karakana yako ya fanicha, harafu ndio unaenda nyumbani kibaha!
Sasa, hapo bila gari hiyo mizunguko utaifanya kwa boda!?
Wanaojipa umaskini, ni wale ameajiliwa, kajenga nyumba, kanunua gari ya kupigia misele!maintenance ya gari kila kitu kinabebwa na mshahara!! Ajira ikiisha, na umaskini uleeeee
 
[emoji123][emoji736]
 
Nadhani utakuwa umesoma heading pekee,,hujasoma kilichomo ndani.
 
Back
Top Bottom