Kujifungua kwa operesheni kuna punguza uke wa mwanamke

Kujifungua kwa operesheni kuna punguza uke wa mwanamke

Sisteri kasome zaidi kuhusu taarifa za afya, hii ndio njia salama zaidi ya kujifungua haswa kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa tatu. Kujifungua kawaida kuna complications nyingi sana. Hao watu maarufu unaowaongelea wana access na the best health care tofauti na majority.

Hii njia pia imepunguza vifo vingi vya akina mama na watoto.
Upo sahihi kabisa ni njia bora na salama,mke wangu watoto watatu alijifungua kwa njia ya kawaida ila mtoto wa nne njia ilifunguka vizuri kabisa sema mtoto huyu wasasa ilibidi afanyiwe Op baada ya njia ya kawaida kufeli mtoto alikua mkubwa kushinda ndugu zake na pia alitangulia vibaya katika kumtoa ni Mungu tulimuona live katika usaidizi na ndiyo wakabadili gear angani wakatumia op sahivi mama na mtoto wapo salama namshukuru Mungu sana, tena OP za siku hizi ni za kisasa kweli panachanwa padogo na baad ya Op hutaweza kuamini kisu kimepita mke wangu yupo poa na mstari unafutika kuna dawa anapaka alipewa hospital inafuta alama
 
Nilijifungua big baby mpaka akapata erb's palsy huwa nasema ningejua kama nitazaa mtoto bonge basi ningeenda CS
erb's palsy nilikua siijui mpaka nilipo google kumbe ni hatari hivi hii ndiyo hali aliipata mke wangu

Sababu Kuu za Erb's Palsy
Uharibifu huu hutokea pale neva za juu za bega (hasisani neva za C5 na C6) zinapovutwa kwa nguvu, kuraruka, au kukatika kabisa:
  • Uzazi mgumu: Wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida, kichwa cha mtoto kinaweza kuvutwa upande mmoja kwa nguvu wakati bega lake limekwama kwenye mifupa ya nyonga ya mama (hali inayojulikana kama shoulder dystocia).
  • Mtoto kuwa mkubwa sana: Watoto wenye uzito mkubwa (zaidi ya kilo 4) wako hatarini zaidi kukwama mabega wakati wa kuzaliwa.
 
Hahaha jamani 😅 Nimeelewa uchungu wako hapo.

Lakini ngoja tuweke facts mezani kidogo maana hii topic imejaa sana hadithi za mitaani:

1. "Operesheni haina maumivu"
Hapana wakuu 😂. C-section ni upasuaji mkubwa kabisa. Unaumia wakati wa kupona, unashonwa tabaka 7 za ngozi na nyama. Maumivu ya kwanza wiki 2-6 ni balaa. Unacheka, unakohoa, unainuka kitandani = unahisi kushonwa upya. Huo ukweli.

2. "Operesheni inapunguza uke"
Hii ndio myth kubwa zaidi. C-section HAIGUSI uke kabisa. Mtoto hatoki njia ya uke, anatoka kwa kukata tumbo. So uke unabaki vile vile ulivyo. Ule msemo wa "kupunguzwa cm" sio kweli kisayansi.

Kitu kinachoweza kubadilisha uke ni:
  • Kujifungua kawaida - ndio hapo uke unatanuka, ila mwili una mechanism ya kurudi baada ya muda na mazoezi ya kegel
  • Umri + uzazi wa mara nyingi - misuli inalegea naturally
  • Kutofanya mazoezi ya nyonga baada ya kujifungua

3. "Wanawake wanapenda op"
Mtu gani anapenda kukatwa tumbo bure? 😂 Wengi hufanya op kwa sababu za kimatibabu: mtoto mkubwa, mtoto kalala vibaya, BP ya mama, nk. Ni kuokoa maisha ya mama na mtoto. Hakuna mtu anaamka asubuhi aseme "leo nataka op".

Ukubwa wa uke baada ya kuzaa:
Mwili wa mwanamke ni wa ajabu. Uke una uwezo wa kutanuka na kurudi. Baada ya kuzaa kawaida, inaweza kuchukua miezi 6-12 kurudi sawa. Mazoezi ya Kegel yanasaidia sana kurudisha misuli.

Kwa C-section, hakuna "kupunguzwa" kwa sababu njia haikutumika. Ila kovu la tumbo, maumivu ya mgongo, na hatari ya op nyingine ndio changamoto zake.

Bottom line: Kila njia ya kujifungua ina changamoto zake. Muhimu ni mama na mtoto wawe salama. Na hapana, hakuna mtu anapunguziwa "uchumi" kwa op 😂

Wewe umesikia wapi hii story ya "kupunguzwa cm"? Kuna mtu alikudanganya vibaya sana mkuu 😅
 
erb's palsy nilikua siijui mpaka nilipo google kumbe ni hatari hivi hii ndiyo hali aliipata mke wangu

Sababu Kuu za Erb's Palsy
Uharibifu huu hutokea pale neva za juu za bega (hasisani neva za C5 na C6) zinapovutwa kwa nguvu, kuraruka, au kukatika kabisa:
  • Uzazi mgumu: Wakati wa kujifungua kwa njia ya kawaida, kichwa cha mtoto kinaweza kuvutwa upande mmoja kwa nguvu wakati bega lake limekwama kwenye mifupa ya nyonga ya mama (hali inayojulikana kama shoulder dystocia).
  • Mtoto kuwa mkubwa sana: Watoto wenye uzito mkubwa (zaidi ya kilo 4) wako hatarini zaidi kukwama mabega wakati wa kuzaliwa.
We acha tu! Stress unazopata mzazi ni kubwa nilikua najipa moyo bora kapata erb's palsy kuliko ingekua cerebral palsy
 
We acha tu! Stress unazopata mzazi ni kubwa nilikua najipa moyo bora kapata erb's palsy kuliko ingekua cerebral palsy
Poleni wakina mama na ndiyo maana laana ya mama hufika haraka maana changamoto mnazipitia ni kubwa na za uchungu sana
 
Upo sahihi kabisa ni njia bora na salama,mke wangu watoto watatu alijifungua kwa njia ya kawaida ila mtoto wa nne njia ilifunguka vizuri kabisa sema mtoto huyu wasasa ilibidi afanyiwe Op baada ya njia ya kawaida kufeli mtoto alikua mkubwa kushinda ndugu zake na pia alitangulia vibaya katika kumtoa ni Mungu tulimuona live katika usaidizi na ndiyo wakabadili gear angani wakatumia op sahivi mama na mtoto wapo salama namshukuru Mungu sana, tena OP za siku hizi ni za kisasa kweli panachanwa padogo na baad ya Op hutaweza kuamini kisu kimepita mke wangu yupo poa na mstari unafutika kuna dawa anapaka alipewa hospital inafuta alama
Poleni na hongereni sana mkuu.
 
DJ HIZI NYIMBO NI ZA CHAKULA MBN SISKII KINA TARIMO NA NKYA MKALE BUFFET LA KUSHOTO 🤔🤔🤔
 
Mpumbavu mwingine katika kubrand ujinga wake, C/S na uke kupungua how how...🗑️
 
Jamani yani upasuliwe tumbo chini kutanuke?? Hii imekaaje...
Au sisi wa kupush ndo chini kuna ziba tumbo linatanuka....🤣🤣🤣🤣
 
We acha tu! Stress unazopata mzazi ni kubwa nilikua najipa moyo bora kapata erb's palsy kuliko ingekua cerebral palsy
Dooooh pole sana....ulishindwa kupush au mtoto aligoma kupita?
 
Back
Top Bottom