Shanily
JF-Expert Member
- Nov 4, 2024
- 856
- 1,662
- Thread starter
- #121
Hiyo staha imekuja baada ya wewe kusema hawavunji sheria.Na wewe kuna watu wanasema unapost sana huna staha.
Point ni kwamba, habari nzima ya staha iko subjective.
Kama mtu hajavunja sheria, ukimwambia asijipost anakosa staha ni kama unamhubiria mtu dini yako wakati yeye haiamini hiyo dini.
Haki ya wewe kuhubiri dini yako unayo, lakini hilo halimaanishi dini yako ina fact, una ukweli, ina maana.
Kuna watu watakwambia hata hatujakuomba ushauri wako we mzee huijui dunia.
Halafu sijasema wasijipost, nimesema kujipost Kila siku mitandaoni napo ni utumwa.
Wapo waliokubali na wapo waliokataa. Ninachopingana na wewe ni kusema kwamba "nimewapangia Cha kufanya", sijampangia mtu Bali hayo ni mawazo yangu.
Uhuru wa kutoa maoni, kama unaona kujipost Kila siku kwako ni sawa hzo ni fikra zako hulazimishwi kufikiri wanavyofikiri wengine.
Lakini hatuwezi kuacha kutoa maoni kisa maoni yetu yatakuwa ni kuwapangia watu.
Kujipost mtandaoni Kila siku napo ni utumwa.
Epuka kuwa mtumwa wa mtandaoni.