Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

Kujipost mitandaoni Kila siku napo ni utumwa

Kuna watu wapo kwaajili ya showoffs.
Kuna watu wanapost ili wapate recognitions.

Kuna watu wanapost ili kujifurahisha.

Kuna watu wanapost kama sehemu ya ku-socialize.

Kuna watu wanapost ili kujulikana.

Kuna watu wanapost ili kuwakera watu wenye tabia kama yako ya kufuatilia mambo yasiyowahusu.

Kuna watu wanapost kuringishia mafanikio Yao au uzuri au majaliwa waliyojaliwa.

Kuna watu wanapost hawajui kwa nini wanapost

Yote kwa yote. Kama havunji Sheria ya nchi. Hamvunjiu mtu yeyote heshima.
Hajapost picha yako Wala Mali yako yoyote. Kinachokuwasha ni roho chafu na Mbaya.
 
If it makes them happy, let them be. Humu duniani kila mtu ana kitu cha kustaajabisha anafanya, whether kwa uwazi au kwa kificho. Kwa akili za kawaida unashangaa, mtu anatikisa makalio akijirekodi na kutuma..ila ndio hivyo tena.

Kuna watu humu Internet ikikata kwa dk5 tu wanakuwa wehu, wanachanganyikiwa kabisa, huo nao si ukichaa!
Ndo utumwa huo, u can't be happy by publishing your daily life, happiness cames within nor by seeking validation from people.
 
Kuna watu hawezi kupitisha siku bila kujipost mtandaoni. Anajaza status weeee utasema analipwa na WhatsApp.
Hana siri kila kitu hadharani kwenye mitandao, yaani huna hata haja ya kupeleleza habari zake , ukizitaka tu unazipata mtandaoni.

Akiachwa, akiwa na huzuni, akiwa na furaha vyote ni kupost tu kwenye mitandao.

Amekuwa kama msanii Kila hatua ya maisha yake lazima watu waijue. Wasanii wanapata pesa angalau, sasa mwenzetu unapata nini!?, Zaidi ya like na comments ambazo hazina faida yoyote Ile katika maisha yako.

Huu ni utumwa vilevile. Kataa kuwa mtumwa wa mitandao.
Kama starehe za watu zinakukera, jitenge mbali nao. Waache wafurahie ulimwengu wao
 
Kujipost, Kuna post zingine za biashara huwezi kuacha kupost.
Yaani ukiwa beach unatupia vipicha, mara unaamka asubuhi " wadau ndo naamka" nani kakuuliza🤒
Kwenye business au deal za pesa Ni sawa kabisa kupost,Ila kupost kila kitu Ni tatizo.
Kuna mmoja Ni mke wa mjeshi,Sasa anavyopost picha zao wakiwa pamoja,naona aibu aisee.
Sijui km jamaa anaangaliaga watsup status za wife wake,labda angempigq stop.
 
Back
Top Bottom