Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Kukoroma usingizini: Fahamu chanzo na tiba yake

Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na

kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna

ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao. Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
Mzee huyu

aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine

kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.

Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.
 
Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma huzidi kwa kadri umri unavyoongezeka na asilimia 54 ya watu wazima hukoroma baadhi ya wakati huku asilimia 25 ya wengine wakiwa na tabia ya kukoroma kila wakati.

Kukoroma baadhi ya wakati kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji. Hata hivyo kukoroma huko sio tu kwamba huharibu usingizi wa anayekoroma bali pia huwasumbua na kuwakeresha wanaolala karibu na mkoromaji. Wale wenye tabia ya kukoroma, hukoroma kila wanapolala na mara nyingi huchoka wanapoamka, na watu wa aina hii hushauriwa kumuona daktari na kushauriwa kuhusiana na tatizo hilo. Lakini kabla hatujaendela mbele ni bora tujue kukoroma hasa ni nini au hutokea vipi?

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile:

• Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

• Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

• Kuwa na misuli minene ya koo. Hii ni kwa wale watu wanene ambao hata nyama zao za koo pia hunenepa na kupanuka na suala hilo husababisha kukoroma, Pia watoto wenye tonsesi kubwa na adenoids baadhi ya wakati hukoroma.

• Kuwa na kilimi kikubwa ni mojawapo ya sababu zinazosababisha kukoroma. Kilimi kirefu kinaweza kuzuia koo na pale kinapotikisika wakati hewa inapita kwa msukumo husababisha kukoroma.

• Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka. Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake. Kukoroma pia kunaweza kuwa ni tatizo la kurithi. Pombe, kuvuta sigara na matumizi ya baadhi ya dawa pia husababisha misuli ya koo ilegee na hivyo hupelekea mtu akorome. Kulala vibaya pia husababisha kukoroka kama vile kulala kichalichali, kwani hufanya nyama za koo zilegee na kuziba hewa.

Je, Dawa ya kukoroma ni nini?

Swali hilo limeuliwa sana na mimi katika kulijibu ningependa kusema kuwa, kujua sababu inayosababisha mtu akorome na kuitatua au kuiondoa sababu hiyo ndiko kunakotibu kukoroma. Sote tunajua adha inayotokana na kukoroma, na sauti hiyo inavyosumbua hasa iwapo anayekoroma ni mtu wako wa karibu kama vile mumeo, mwenzi wako au yoyote yule inayekubidi ulale naye karibu au katika kitanda kimojana hata chumba kimoja. Kukoroma pia huathiri usingizi wa mkoromaji kwani anayekoroka humbidi aamke mara kadhaa usingizini akijua au bila kujua kutokana njia zake za hewa kufunga kwa sekunde kadhaa ambapo usingizi pia hukatika. Wanaokoroma pia hushindwa kulala vizuri suala linalopelekea asubuhi wawe wamechoka na kutofanya majukumu yao vyema, na pia wale wanaolala nao karibu hupatwa na matatizo kama hayo. Vilevile tunapaswa kujua kuwa kukoroma kuna athari za kiafya za muda mrefu kwa mtu anayekoroma hivyo si jambo la kufanyia mzaha na ni tatizo ambalo linapaswa kushughulikiwa na kutatuliwa.
Wataalamu wanatuambia kuwa ili kujua kukoroma kwako kunasababishwa na nini ni bora ushirikiane na mwenzi wako au yoyote unayelala naye ili akuchunguze pale unapolala na kujua jinsi mwili wako unavyokuwa pale unapokoroma. Ni bora aandae orodha na kuchunguza yafuatayo:

1. Kufunga mdomo na kukoroma kunaonyesha kuwa kuna matatizo ya ulimi.
2. Kufungua mdomo na kukoroma kunaonyesha unaweza kuwa na tatizo katika misuli au nyama za koo.
3. Kukoroma unapolala kichalichali kunaonyesha kuwa pengine kwa kubadilisha namna unavyolala kukoroma nako kunaweza kwisha.
4. Kukoroma wakati unapolala kwa kila mlalo kunaonyesha kwamba tatizo lako ni kubwa na pengine kunahitajia tiba kubwa zaidi.
Iwapo umebadilisha namna unavyolala na haikusaidia, unashauriwa ujaribu yafuatayo:

 Punguza uzito
 Safisha njia yako ya hewa. Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma. Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
 Wacha kuvuta sigara.
 Lala mapema na pata usingizi wa kutosha kila mara huku ukijiepusha na kuchoka sana. Kunyanyua kichwa kwa nchi 4 huweza kupunguza kasi ya kupumua na kusaidia ulimi na taya kwenda mbele hali ambayo hupunguza kukoroma. Fanya hilo kwa tumia mito maalum ya kupunguza kukoroma au lala bila mto.

Wataalamu pia wanasema kwamba unaweza kupunguza kukoroma kwa kutokula baadhi ya vyakula au dawa kabla ya kulala ambavyo huongeza kukoroma. Vitu hivyo ni kama vile
o Kutokula mlo mkubwa kabla ya kulala.
o Kutokula vyakula vinavyotokana na maziwa au maziwa ya soya.
o Kutokunywa pombe kabla ya kulala.
o Kutotumia dawa aina ya antihistamines.
o Kutotumia vyakula au vinjwaji venye kafeini.

Vilevile wanaokoroma wanashauriwa kufanya mazoezi ya koo ambayo ni pamoja na kuimba, kusoma kwa kurudia rudia voweli (a,e,i,o,u) kwa nguvu kwa dakika tatu mara kadhaa kwa siku, kuweka ncha ya ulimi chini ya meno ya mbele na kurudisha ulimi nyuma kwa dakika 3 kila siku au huku mdomo ukiwa wazi pelekea taya yako upande wa kulia na wacha ibakie katika hali hiyo kwa sekunde 30. Huku mdomo ukiwa wazi, kaza misuli ya nyuma ya koo na rudia kitendo hicho kwa sekunde thelathini. Unaweza kutizama kwenye kioo na kuona jinsi kilimi kinavyokwenda juu na chini.

Iwapo kukoroma hakutoisha kwa kutumia njia hizo tofauti zilizoelezwa, usife moyo jaribu kumuona daktari na akupe ushauri wa kitiba kuhusiana na tatizo hilo. Madakatari wataalamu wa magonjwa ya pua, masikio na koo au ENT wanaweza kukusaidia zaidi kutatua tatizo hilo. Siku hizi kuna vifaa mbalimbali vinavyotumiwa mahospitalini ili kuondoa kukoroma kama vile kifaa kinachowekwa kwenye meno, CPAP, kidude kinachowekwa mdomoni au hata kufanyiwa operesheni ili kuondoa tatizo hilo.

Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na

kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna

ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao. Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
Mzee huyu

aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine

kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.

Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.
Mzizimkavu hii umeitoa Michuziblog iliwekwa kule na mjombangu mwaka juzi ni vizuri ukitumia maandishi ya mtu basi mtaje au sema umetoa wapi.
Ulivyoiandika umejifanya muhusika mkuu sio vizuri.Pia imesaidia watu wengi sana.
 
mi nikinywa pombe kali ndo nakoroma zaidi yani kama tractor
 
Mzizimkavu hii umeitoa Michuziblog iliwekwa kule na mjombangu mwaka juzi ni vizuri ukitumia maandishi ya mtu basi mtaje au sema umetoa wapi.
Ulivyoiandika umejifanya muhusika mkuu sio vizuri.Pia imesaidia watu wengi sana.
mimi sikutoa kwenye Michuzi Blog wewe ungetafuta huko kwenye Michuzi Blog ukaweka na ya kwako kisha ukaweka source yake hatupo hapa kushindana tupo hapa kuwasaidia watu wenye matatizo ukitaka mambo ya mashindano nenda kule kwenye jukwaa la Mambo ya Siasa ukashindane na mambo ya Siasa kama una mawazo ya kuwasaidia watu hapa ndipo jukwaa la mambo ya kuwasaidia wagonjwa usilete pumba zako hapa tafadhali.
 
Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na

kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna

ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao. Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma

na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
Mzee huyu

aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine

kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.

Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.
Shukrani mkuu kwa maelezo yako na ushauri uliokwenda shule. Nimeona posts nyingi tu juu ya hili tatizo, nadhani utakuwa umewasaidia wengi.
 
..wadau kuna mtu ameweza kutibu au anajua matibabu ya tatizo la kukoroma usingizini. Nina tatizohili na ni kubwa msipime mpaka mtu unogopa kuhudhuria shughuli za halaiki!!! Msaada plz.
 
Bora ww ulejikubali! Wengine hawakawii kukwambia"nna ndugu yangu anatatizo......" pole wataalamu watakusaidia
 
soma hili na tekeleza,

NAMNA YA KUMALIZA TATIZO LA KUKOROMA
Habari za kazi mheshimiwa Michuzi,nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka.Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia.Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao.Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20. Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake. Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.Mdau Ibrahim,D'salaam.
 
..wadau kuna mtu ameweza kutibu au anajua matibabu ya tatizo la kukoroma usingizini. Nina tatizohili na ni kubwa msipime mpaka mtu unogopa kuhudhuria shughuli za halaiki!!! Msaada plz.
kuhudhuria halaiki??? Kwani unalala hata mchana kama wasirra na mrema??
 
Inawezekana una ugonjwa unaojulikana kama sleep apnea.....kama wewe ni mnene loss 10 percent of your weight....trust me itaisha.....sleep apnea is a very dangerous desease it may cause heart attack.
 
Pole sana mwana JF, kwanza waone wataalam. Lakini pia kama ni mnene sana jitahidi kufanya mazoezi,punguza unene a epuka vyakula vyenye mafuta mengi
 
Jaribu kuweka plaster across the noze, inasaidia na ni cheap solution. weka kama hapo kwenye picha
12.jpg
 
Back
Top Bottom