Wengine tumekulia mazingira hayo watoto wa nyumba hio wao wanakula cakes na mayai asubuhi nyie mnakula magimbi. Wanalia sahani nyie mnapigwa kwenye sinia chini! Nyama za baba tu japo baba kanunulia familia nzima ile ila anapikiwa yeye na wanae nyie mwendo wa kabichi na maharage tu. Siku za shopping ya vyakula watoto wake wananunuliwa chocolates na pringles wanalia chumbani na kupangusa midomo mtakutana na maganda tu. Alfajiri uamke ufagie kiwanja na banda la mbuzi kisha unaenda shule hata chai hujanywa hupewi hata sh.100 utembee wao wanapandishwa school bus na buku ya kuspend on break time hapo washakula cakes, mayai na chai asubuhi! I don’t wanna remember that life aisee...Siwezi ruhusu mtoto wa mtu apitie ile hali akiwa kwangu! I rather not take him/her.