Kuliko kuajiri mfanyakazi wa ndani tuwe na utaratibu wa kuchukua watoto wa ndugu kwa nia ya kuwaendeleza

Ndugu anaejielewa yupoje na asiyejielewa yupoje? Kwani ndugu anakuwa hajui purpose yake ya kuja hapo ama mnakuwa hamjawaweka wazi anapotoka huko anabebwa kama kiroba?
Purpose ya kuishi kwako unaijua wewe, sio yeye.
 
Sawa sijakataa mi nalalamikia ile fairness! Kwani wangevaa woolworth wasingesoma hadi kupata kazi?

Turudi kwenye dhamira ya mlezi wao, hatujui uwezo wake lakini tumeona wamefanikiwa…. wala haijawekwa wazi kama familia ilishirikiana au ni mjomba aliwasomesha kwa siri.

Kwanini tumhukumu mke kwa maronya bila kujua dhamira yake, kila kitu ni PENGINE…..[emoji276]
 
Ndugu ni changamoto, hasa wa ukweni, akiwa wa kiume mbeleni mtadharauliana, akiwa wa kike mwisho wa picha atakutega umle yani ni varangati vangu vangu y
 
Hahahahah sasa umuangalieje kama anakula na kiinua mgongo anapata daily!😅😅😅 mwambie bandogo aache uchizi. Well, hopefully humsimangi simangi tu maana misaada ya masimango inakera!

Chuo mtu hasimamiwi anajisimamia mwenyewe.
Wala simsemi mia namtizama tu akija anakula na 5000 yake nampa anaondoka
 
Tatizo hao watoto wa ndugu wakija kwako nao wanajiona wako kwa ndugu hawataki kufanya kazi
 
Wapo ndugu wengi hawaamini hili ! Lazima watataka mshahara tu, na hapo ndipo utagundua unapigwa Mara mbili na utaona bora kutafuta mfanyakazi rasmi
 
You are right mambo kwani unaweza kuleta kibaka toka kijijini kama mfanyakazi wa ndani na unamgharamia kila kitu, mwishowe mtu wa nyamba ya pili anamrubuni ili tu apate kujuwa siri zako aanze kuwambia wenzake mtaani. Ni bora kumchukua ndugu na kumsaidia kuliko hawa vibaka wa vijijini wasiokuwa na akili timamu tena wengine wachawi.
 
Hii inanihusu kabisa
 
Sawa sijakataa mi nalalamikia ile fairness! Kwani wangevaa woolworth wasingesoma hadi kupata kazi?
Hawa wanawake wana roho mbaya sana tena huyo ndugu ataish vizur tu kama ni wa upande wake ila kama ni wa upande wako ndo hata kuangalia Tv atakatazwa kukanyanga sebuleni itakua marufuku labda we mwenyewe uwepo ndo watajidai wanamuita aje mle pamoja
Ndugu ukimchukua mchukue kwa nia moja tu kwa maelewano ya kuja kufanya kaz na kumlipa au kwa maelewano ya kumsaidia kumuendeleza, haiwezekan awe anatoka shule alaf anapiga kaz had saa 6 usk alaf alfajr saa 11 umeshamuamsha huku watt wako wamelala kiukweli hayo ni manyanyaso hakuna msaaada hapo
 
Heri wewe umenielewa maana hicho ulichokieleza ndio hasa mimi nilikipitiaga exactly
 
Bonge la idea hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kudai anateswa sana

Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Pata Mirinda bariiiidi maana umegusa penyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…