Kuliko kuajiri mfanyakazi wa ndani tuwe na utaratibu wa kuchukua watoto wa ndugu kwa nia ya kuwaendeleza

Mi sitaki hata kuishi na ndugu, sitaki lawama na mtu dada wa kazi anatosha....
 
Mwenyezi Mungu atusaidie na atuongoze. Atuondolee Roho ya Umasikini. Maana hata ukimiliki ulimwengu mzima, ila ukawa na Roho ya Kimasikini.. Hakika utakuwa mtu wa kuhangaika na kutaabika tu.
 
Piga kubao hilo limwanamke
 
Ni jambo jema na la msingi kabisa kuwasaidia ndugu lakini umakini unahitajika ili kuhakikisha hakuna tuhuma za kujirudia kuhusu manyanyaso japo kwa asilimia kubwa ile fair treatment inakuwa na dosari fulani na ni wachache wanaoweza kubalance hasa kwa upande wa akina mama kupendelea zaidi wanae nadhani ni nature

Anyway saidia sana tena uhakikishe unayemsaidia anafanikiwa ili kuwa reference tosha

Say no to umaskini
 
Huyo mumalawi ulimpatia wapp?
 
Not always the case---mimi nishaishi na kijana in his 20's---elimu ya darasani ilimshinda siku nyingi huko kijijini,hivyo akaja mjini kutafuta alternative---mwanzoni alitamani biashara---lakini kila pesa anayopata anaenda kupiga mtungi.
Tukapambana akapata leseni ya udereva--anapata fair treatment ya kila kitu--na amekuwa dereva backup ili akishazoea barabara aweze kuajiriwa/kujiajiri kwa njia ya gari---hela ya mafuta yenyewe anaenda kununua K-vant---watu kama hawa unawasaidiaje sasa.
 
Huyo mumalawi ulimpatia wapp?

Nafikiri swali ingekua hao wamalawi hua nawapata wapi?

Kuna Dada Mmalawi ameolewa huku na ameshaishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 15, hua tunamtumia yeye kwa sababu anafahamiana na wenzao pia inakua guarantee yetu akituletea yeye
Nimeshakua nao zaidi ya watatu na sijawahi kujuta.
 
Huyo anazingua bange unampiga chini tu
 
Haswa swali lililenga hapo maana wamalawi ndo watu Wana watumia sikuhizi na ninaskia hawasumbui kabisa
 
Ukimtetea kwamba unamtaka
Ndio hivyo mkuu,, kuna wakati naona hii sio sawa! Ukijaribu kusawazisha mambo wife anabadilika, anaona kama kuna benefits napata lakini wapi mtoto wa watu namuonea tu huruma halafu pia naangalia malezi ya wanangu kama kuwalemaza hivi!!

Unakuta binti yangu haingii jikoni kwa muda mrefu eti kisa tuna ndugu msaidizi wa majukumu ya nyumbani. Hii sio sawa, wake zetu mnalemaza watoto wetu kisha badae muanze kulialia ooh mwanangu ana mikosi hakai na mwanaume n.k kumbe mchawi ni wewe na malezi yako mabovu kwa wanae ukidhani unawajali sana kwa kuwatoa kwenye majukumu yao ya msingi... Mnazingua wake zetu, mnafeli sana hapa

Kudadeki nimetema nyongo huku mafichoni nadhani soon ntapata relief.. Hahahaaa
 
Hahahahahah kupata relief ni kuwafurusha hao binti zako waende kufanya shughuli za jikoni
 
Mkuu upo wapi nikupongeze hata kwa bangi nyepesi, maana umeongea kitu ambacho ni true kabisa bwashee
 
Tusipangiane maisha bhana, kwani hao ambao si ndugu au wa kijijini kwenu hawastahili kuendelezwa.....watanzania wote ni ndugu..
 
Ila mdau unaonekana uliathiriwa sana kisaikolojia na hizi mambo yaan vile unavyoongea tu....
Kifupi usitegemee kupata raha au uhuru ukiwa kwa mtu hata kwa wazazi wako. Uhuru na starehe ni pale unapokuwa kwako, ukijijengea hii mentality utaishi kwa yoyote bila hata shida.
Mie niliwahi kukaa na ndugu yangu haikua rahis kwa kweli ila nilijipa moyo tu kuwa pale napita na wala hakunipa shida.
 
True story
 
Ile ilikuwa experience nzuri sana kwako na mshukuru huyo mmama kwa kukufanyia hivyo. I am sure by now utakuwa umerealize lile lilikuwa somo la kutafuta vyako mapema na uwekeze mapema ili wanao wasije kupitia kitu kama hiyo. Kama hujalearn by now, hujachelewa. Tunapaswa kuwashukuru watu wote (wema au wabaya in our perspectives) kwa kuwa wote waliaacha alama katika maisha yetu.

Swali la kizushi: Vipi maisha ya sasa ya wale madogo waliokuwa wanagonga cakes, mayai na pringles wakati wewe ukigonga magimbi au ukipiga pasi ndefu mpaka mchana? Haitoshangaza kusikia baadhi yao wana hali tete sasa hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…