Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kwaiyo unataka kutuambia msafara wote ule wa mama ni security details? Acha ushamba pale waliojaa wengi sio watu wa usalama
 
Hivi kama mtu hujui kitu ukinyamaza utafariki? Ngoja kwanza nikaushe watu wajiliwaze wasahau shida ya dunia
 
Director wa PSU nadhani alikuwa mlinzi wa Nyerere enzi zile lazima mtazamo wake uwe wa karne ile wa kulinda mgongo bega kwa bega na ma tavor makubwa makubwa wakati Dunia ya sasa imeendelea sana.
 
Wote ni watz na ni vijana wa PSU ukitaka kuwaona nenda mzena hospital..
 
Wa Magufuli naona ulikuwa na uafadhali maana nakumbuka hata helikopita ilikuwa ni moja ila huu wa mama una helikopita zaidi ya mbili.

Sijajua kwanini wanafanya aerial surveillance huu ulinzi unastajabisha kwa kweli?
Mkuu, kifupi nafikiri wataalam wa ulinzi kikosi rais wameshauri hili na limetekelezwa unavyoliona baada ya wao wataalam kuona kuna uhitaji wa hicho ukionacho.
Shika lako waache na yao.
 
Ni ulimbukeni na ushamba ndani yake, kutokujiamini na kujihami, njia nyepesi ya wasaidizi kupiga mpunga kwani maduhuri yanakuwa mengi zaidi, ni kutokuwa sensitive na kujali maisha ya watanzania walio wengi ambao wako duni sana, mimi si mtumishi wenu bali ni mfalme wenu kwani mm ni kila kitu? Au yote hayo na mengineyo?
 
Sijui inatoa picha gani kwa mataifa ya wenzetu ambao huwa tu awacheka kuwa kwao hawana amani.
 
Wakati sisi walipaji tunatokwa jasho na damu wao ndiyo kwanza wanaagiza mapangaboi

Halafu Polepole kwenye zile porojo zake akiongelea parallel/deep state anaona kama ni mambo ya Angola huko na sijui wapi kwingine. To be frank uongozi wetu ni parallel state live bila chenga. Huna hata vyumba vya kutosha vya madarasa ya primary schools after 60 years of political independency unatoa wapi jeuri ya msafara na ulinzi kama ule? Hao wanaokupa msaada msafara wa Rais wao hayazidi magari matano. Hii kama si deep state ni kitu gani kingine?
 
Inashangaza sana kiongozi
 
Ukiona hivyo basi wewe si mlengwa so ulitakiwa ulipite kama hujaliona mkuu.
Bobby, kama ndivyo basi, ungemtumia mlengwa wako kwa WhatsApp au text message au FB..!

Nadhani hujui Terms & conditions za kupost mada humu JF. Otherwise una bahati tu kwa uzi wako huu kuendelea kuishi hadi dakika hii...!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…