Kulipa mamilioni kusomesha 'Generation Z' ni kama kucheza kamari!

Kinaitwa kizazi Cha siku za mwisho kisichomjua Mungu chenye sifa zifuatazo.
. wabinafsi
. uwezo mdogo wa kufikiri
.wapenda starehe na anasaka
.Wagomvi
.Utii na heshima sifuri
.kinataka harusi na Sio ndoa
.wajuani lakini hawana wajuacho
.hakina uvumilivu Wala uhimilivu
. Mafanikio ya Shortcut na miujiza
.
 
Wewe generation Z, uko na akili kumzidi mleta mada.

It's a simple fact, kila kizazi kinachofuatia ni matokeo ya vizazi vilivyopita. Generation Z wanaendeleza yale waliyokuta Millenials na generation X wanafanya.
Nakubali kanizidi akili ila na wewe takuwa amekuzidi zaidi. Kijana mejenga hoja zake bila kukashifu wala kukejeli jambo ambalo wewe limekushinda
 
Sahihi
 
Kinaitwa New age movement.wazee wa suti wamefaulu kutengeneza watu bandia kizazi robot kisichokuwa na ubunifu wowote
Sio kweli. Kadri muda unavyozidi kwenda, ndivyo ubunifu unazidi kuongezeka. Ndio maana teknolojia inakua, na mambo mengi yanarahisishwa. Ni wazi kwamba kila kizazi kipya kinakuja na ubunifu kuliko kizazi kilichopita!

Kama ungewaambia wazee wa miaka ya themanini kwamba ipo siku kutakua na treni za umeme zenye kusafiri Dar to Mwanza kwa masaa manne, wangekuona mwehu!

Juzi kuna dogo wa miaka 13 kashinda world championship kucheza FIFA video games. Prize ilikua zaidi ya dola laki mbili. Hiki ni kizazi cha kumake money while having fun. Everything is computerized!

Mimi ugomvi wangu na hawa generation Z ni low EQ. Hawa madogo wako na roho za plastiki. Ndio maana unaona suicide rates na depression ziko kwenye record high. Ni kama bloilers vile hawawezi kumudu nyakati ngumu!

Hapo ndio unakuta wako tayari kuachia marinda ili wapate maisha. Ni sababu hawana roho ngumu. Sio watu wa mtumba, ni watu special made in China!

[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Nakubali kanizidi akili ila na wewe takuwa amekuzidi zaidi. Kijana mejenga hoja zake bila kukashifu wala kukejeli jambo ambalo wewe limekushinda
Sijakejeli, nimetania. As a matter of fact, dogo yuko smart. Hata uandishi wake unaonyesha. Kwenye hiki kizazi chao, ukitaka kujua kama yuko na kitu kichwani au ni mtupu, mwambie aandike maelezo paragraphs nne tu, utajua!

My apologies in case you're offended!
 
Accepted
 
6. Ndio kizazi kinachofaulu zaidi mitihani ya NECTA.
Ndio kizazi hakijui nini maana ya GIZA grid ipo nchi nzima na taa za solar
Ndio kizazi wanaanza kuajiriwa mapema zaidi kuliko wakati wowote
Ndio kizazi kina uelewa wa mambo ktk umri mdogo. Wewe uelewa at 20s wenyewe at 13+
Mengine upo sawa. Pamoja debwe debwe.
Hawachezi mpira, kikapu nk.
Wanabet sana.
They don't care.
Mda mwingi wanasikiliza mziki badala ya kusoma vitabu na kusikiliza documenrary.
 
Hayo mambo peleka (au yaache) huko kwa waMarekani.

Sie Tanzania hatuna hizo classification za Gen X, Y, Z na Boomers
 
Mtoa mada kabla ya kutulaumu, ungeangalia kwanza nyinyi kama wazazi mliaandaa mazingira gani vijana wasifike hatua hiyo.
 
Hapo kwenye documentary na vitabu mengi ni theory hayana uhalisia hizi vitabu vya hadithi na uchumi?
Nishaacha kusoma vitabu na kiangalia documentary.
Wewe unaangalia documentary kuhusu Nyerere, baadae itakusaidia nini? Siyo mwalimu, utajua kinachofuata?
Vitabu vingine hata havieleweki unasoma vya kazi gani?
Unaangalia documentary na unasoma vitabu, hapo haujui hata kuinstall windows kwenye computer. Simu yako hata kubadilisha password hujui. Unaenda kwa jirani.
Hata extension cable ikiungua hauna hata uwezo wa kuangalia tatizo nini. Unaenda kutupa jalalani.
Baada ya kugundua hayo, sasa hivi nakula zangu pesa tu.
 
Mkuu hata kizazi Cha miaka ya 80s kurudi nyuma kinaonekana Cha kistaarabu kwasababu tu hakukuwa na utandawazi Kama wa Leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…